white wizard
JF-Expert Member
- May 18, 2011
- 8,566
- 13,770
Kipindi kile yalipofikia 1780, mbona nauli zilibakia pale pale tu?!!watu walilalamika kuwa mbona nauli hazishuki, wakajibiwa huo ni unafuu wa muda tu, hata sasa hilo ni ongezeko la muda, usijari.Wakuu hivi hii hali inaelekea wapi? Kulingana na bei mpya kuna baadhi ya mikoa lita ya petrol imefika 2480. Ni kweli huko duniani mafuta yamepanda au hapa kwetu tu tunakomoana.
Je, ni halali nauli kuendelea kubaki pale pale? Au tutegemee ongezeko huko mbeleni?
Huko tunakoenda nadhan kuna watu wataenda kupaki magari yao, mimi leo 20k nimeambulia lita 8 na point nikabaki nashangaa kumbe bei zishapaa.