Kipi unafanya ili kujituliza wakati unapitia magumu?

Kipi unafanya ili kujituliza wakati unapitia magumu?

Sote kuna wakati tunapitia hali au wakati mgumu kimawazo, kihisia na kimwili lakini kila mtu ana njia tofauti za kukabiliana na nyakati hizo.

Member mwenzenu akili ime stack, depression na hofu imenijaa, naombeni mnipe mbinu za kukabiliana na hali hii kabla sijafika pabaya because there is riot inside my heart and mind.
Fanya kilicho ndani ya uwezo. Kilicho nje ya uwezo potezea.
 
Mtu ninaye mwamini sana ni Mzazi wangu, ila siwezi mueleza kwani nahisi akijua hofu itamjaa na mimi sikuzote namuaminisha mambo yanaenda vizuri ili tu awe na amani.
Huenda neno lake ndilo likawa faraja Kwa kipindi hiki unatafuta kutuliza akili
Kuwa na subra maisha hayajawah kuwa rahis
 
Hata sitamani kuona sura yangu, i feel shame and guilty.
Yan kwa sasa unavojihisi mimi nilishawahi kata tamaa nikatamani kujinyonga, lakn nlifikiria ndo nlkua nmepata kitoto kidogo dem wangu alikua ameshajifungua, niliwaza sana nikijinyonga mwanangu ataishi maisha gan hapa duniani na ukizingatia ni mtoto wa kike, nlipiga moyo konde nikanyanyuka kwenda kupambana, chanzo ni mzazi wangu kutokunizingatia baada ya kufail form 4, nkaamua kutoka home na kwenda kupambana mbali na nyumbani, mpaka sasa mambo yangu yamenyooka wala siwazi tena , kipindi kigumu nlkua namuomba sana Mungu usku na mchana sipati usingizi, Mungu alishusha neema yake, nikapata connection ya kazi nzuri mpaka sasa nakula maisha,
So never give up ✊
 
Mkuu ni maswala ya financial tu, japo ni mambo ya kawaida lakini nimegundua kuna muda mtu anaweza tamani asiishi tena kwenye ulimwengu huu.
Kama umepanga nakushauri badilisha mazingira, hamia mtaa mbao hawakufahamu kabisa hata mtu mmoja then ukifika anza ukurasa mpya,
Hivyo ndivyo nilivoishinda depression
 
Mimi huwa natembea mile 10000 kwa siku baada ya hapo akili inakaa Sawa na hii ni kila siku, maana mwili unatoa jasho njiani unakutana na vituko mbalimbali pia umakini barabarani concentrated kwenye kuepuka magari unajikuta ume - relief

By the way, 🤣piga punyeto moja huku unamwaga mbegu chini kushukuru mababu
 
Hongera! Hatua ya kwanza umefunguka vile unavyojisikia, haupo peke yako. Ingekuwa watu tunatembea na screen zinaonyesha yale yaliyopo akilini na mioyoni mwetu basi kila mmoja angemuonea huruma mwenzie.

Kuishi ni moja ya kazi ngumu kwelikweli, ufahamu, utashi na hisia za binadamu zinatufanya kuwa viumbe tunaobadilika kila mara. Kila binadamu anatamani kuishi maisha yake yote yakiwa yamejaa furaha tele: ila ni wachache wanaoujua ukweli mapema na kuukumbatia, ukweli ni kwamba zipo siku utaanguka na usijue utawezaje kusimama tena. Matumaini yetu yanabebwa na kesho yetu tusiyoijua, kitu kikubwa cha kukumbuka: haupo peke yako.

Umefanya uamuzi mzuri kuandika uzi huu, sasa tafuta mtu unayeweza kumshirikisha kile unachopitia ana kwa ana, ubongo wako kwa sasa unahitaji msaada wa nje kuweza kuona kwamba bado ipo nafasi au njia nyingine sahihi na bora kutatua changamoto uliyonayo.
 
Mimi nikiwa katika hiyo Ngumu kimawazo napenda, kujifungia ndani na kusikiliza mziki aina ya Rege hasa Nyimbo za lucky dube na Senzo.. Baada ya muda akili hupata uhai na kutafuta njia ya kuvuka.

Pole sana Mkuu wa changamoto unayopitia Ila kwa kuwa bado upo hai Amini kuna namna ya kuvuka katika hilo.

Jua linapochomoza huchomoza na tumaini Jipya...
 
Usikae mpweke, mawazo ya kujiua huwa yanawapata watu wanye stress wanaojitenga na kuwa wapweke. Toka nyumbani, nenda kakutane na watu.

Usiingie kwenye uraibu wa kitu chochote, pombe, sigara au bangi au kamari.

Mwisho: Endelea kupigana mtoto wa kiume.
 
Chanzo ni maisha tu mkuu, siwezi kueleza hapa lakini kuna kitu nime loose na sijui nitapata vipi tena.

Ombi langu ni msaada wa kimawazo kwa namna gani naweza fanya kuondokana na depression na majuto makali niliyonayo moyoni mwangu.
Ishi maisha ya kiroho yote hayo yatapita
 
Back
Top Bottom