Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten

Kipindi cha TV, Kutoa Elimu ya Katiba, Sheria na Haki, Kuanza Jumapili Hii Kupita Channel Ten

Mkuu Bejamini Netanyahu, sina project yoyote na Halima Mdee, ila namkubali sana Halima Mdee, Esta Bulaya, Esta Matiko na Upendo Peneza. Ninacho taka ni watendewe haki, hata kama ni kufukuzwa, wafukuzwe kwa haki na sio huku kufukuzana kikangaroo!.

Kiukweli mimi sio mtu wa maana hata kidogo, mimi ni mtu wa hovyo sana na kama mwandishi wa habari, maswali yangu huwa ni maswali ya hovyo, hadi anayeulizwa badala ya kujibu alichoulizwa, anatoa tafsiri ya jina la mtu!. Baadhi ya hoja zangu za hovyo, zinapelekea mimi kuitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge.

LL.B yangu nimeisomea UDSM, miaka ile!, tena ni LL.B hons!.
P
hahaha nimecheka sn, ni changamoto hizo, mfano Halima angekuwa amefukuzwa CCM ungeandika hiki?
 
Mkuu Bejamini Netanyahu , mtu kuwa wakili ni ile tuu kusomea sheria, kuhitimu LL.B, enzi zetu ni ku petition na kuwa wakili, sasa ni kwenda LS na kupasi unakuwa wakili, hivyo mimi ni wakili!.

Kuwa wakili sio lazima kwenda mahakamani, wako mawakili wa mahakamani kuendesha kesi, hawa wanaitwa mawakili wa litigations na tupo mawakili wa legal opinions, mimi sijawahi kwenda mahakamani kuendesha kesi yoyote, sio wakili wa litigations, ni wakili wa legal opinions na sasa ndio nakwenda ku revolutionise fani ya uwakili kwa kuwa wakili mtangazaji, kuwasaidia watu kupata haki zao kupitia kipindi cha TV.

Kiukweli watu wana shida sana kupata huduma za kisheria, mimi natoa huduma hizi bure online na kupitia TV, nitasaidia watu wengi zaidi kuliko hata kama ningekuwa ni wakili wa litigations.

P
Mkuu mimi na wewe tunapishana padogo sn, simama kwenye msitari kama zamani
 
Wanabodi
Nijitambulishe tena na tena, kuwa japo mimi Paskali Mayalla, ni mwandishi tuu wa Habari wa kujitegemea kwa kujitolea, na mtangazaji wa kujitegemea, mimi pia ni mwanasheria na wakili wa kujitegemea kwa kujitolea, hivyo kupitia uasanasheria wangu, nina mamlaka ya kuikosoa mahakama kwa kutotenda haki, na nimekuwa nikiandika sana makala kutoa elimu ya katiba, sheria na haki kupitia safu yangu ya kwa Maslahi kwa Taifa, sasa safu hii haishii kuandika tuu magazetini na mitandaoni, safu hii sasa inakwenda hatua moja mbele, inakwenda hewani kupitia kipindi cha TV cha "Kwa Maslahi ya Taifa", kitakuwa kinarushwa hewani kila siku za Jumapili Saa: 3:00 usiku na marudio siku za Jumatano Saa 9:30 alasri kupitia Channel Ten, ni kwa kuanzia tuu, baadae kipindi hiki pia kitarushwa na TBC, ITV, Star TV, na Azam TV, ili elimu hii ya Katiba, Sheria, Haki na Wajibu, iwafikie Watanzania wengi zaidi.
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=uSiW3_dfU58l3B-V

Kipindi cha kwanza ni mahojioano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Jaji Elieza Mbuki Feleshi kuhusu uwezo wa Mahakama zetu kutenda haki.

Siku za nyuma niliandika makala 5 mfululizo za kilio cha Haki, na miongoni mwa hoja zilizoniibua kumtafuta Mwanasheria Mkuu, Jaji Feleshi, ni baada ya moja ya makala hizo ku challenge uwezo wa Mahakama zetu kutoa uamuzi wa haki. Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Mtamsikia wenyewe AG, Jaji Feleshi akijibu, ila hii hali ya Mahakama zetu kutotenda haki kwa kitu kinachoitwa legal technicalities, kinaendelea! na mfano mzuri wa haki kutotendeka kwa legal technicalities ni hii hukumu ya kina Halima Mdee na wenzake 18!

Kwa kawaida kesi ikiwa inaendelea Mahakamani, hairuhusiwi kujadiliwa ili kuepuka kuingilia uhuru wa Mahakama, lakini baada ya hukumu kutoka, ni rukhsa kuijadili kesi husika.

Jana Mahakama Kuu imetoa uamuzi kuridhia uamuzi wa Kamati Kuu ya Chadema kuwafuta uanachama wa wabunge wake 19 wa viti maalum wa Chadema kwa kosa la kughushi kujiteua. Ila Mahakama imewakubalia kwa kupinga uamuzi wa Baraza Kuu, Chadema kuridhia uamuzi wa CC ya Chadema huo hivyo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiitishwe upya kusikiliza rufaa zao.

Uamuzi wenyewe ni huu
1. The Prerogative Order of Certiorari is granted to quash the decisionpassed by the Governing Council of the 1st respondent on the 11thday of May 2022 and formally published on the 12th May, 2022.
2. The Prerogative Order of Mandamus is granted to compel the 1strespondent to observe the due process and Principles of NaturalJustice in determining questions/matters affecting the applicants'rights.
3. No order is made as to costs. Right of appeal is fully explained

Kwa maoni yangu, uamuzi huu wa Mahakama sio uamuzi wa haki hata kidogo! kwasababu msingi wa wabunge hao kufungua shauri mahakamani ni kupinga kufutwa uanachama, kinyume cha katiba, sheria, taratibu na kanuni. Baada ya kikao cha Baraza Kuu Chadema kuridhia uamuzi wa CC ya Chadema kuwatimua, ndipo wabunge hao wakakimbilia mahakamani kutafuta haki kwa kupinga uamuzi wa Baraza Kuu Chadema kuridhia uamuzi wa CC Chadema kuwatimua!.

Japo Mahakama imepindua uamuzi wa Baraza Kuu Chadema,
Mahakama ni kama iimewapa ushindi Chadema, kuwa CC ya Chadema imewatimua kina Mdee kihalali!. Na kuwa wabunge hao hawakupinga uamuzi wa CC wa kuwatimua bali wamefungua kesi kupiga uamuzi wa Baraza Kuu kuridhia uamuzi and CC ya Chadema kuwatimua, mahakama imebatlisha uamuzi wa Baraza Kuu, kuridhia uamuzi wa CC ya Chadema hivyo wengi kuwaona kina Mdee kama washindi wakati mahakama ni imebariki kutimuliwa kwao!. Sababu Mahakama ilizotoa kupindua uamuzi wa Baraza Kuu Chadema, ni very silly reasons!. Kwa mujibu wa katiba ya Chadema iliyoridhiwa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, wajumbe wa CC ya Chadema ni wajumbe halali wa Baraza Kuu Chadema na wabunge halali wa Mkutano Mkuu Chadema!, Mahakama haina uwezo kuwapangia Chadema wajumbe wa vikao vyao halali kwa mujibu wa katiba yao!

Nimeisoma hukumu,
1. Mahakama zetu zinarudia makosa yale yale ya ukosefu wa kutenda haki kwa sababu ya legal technicalities, kuwa Mahakama haiwezi kutoa uamuzi wa kitu ambacho hakikuombwa!.
2. Wabunge hawa 19 wa Chadema, walivuliwa uanachama wao kinyume cha katiba ya JMT na kinyume cha haki kwa kutokusikilizwa, kinyume cha katiba ya Chadema kwa kukiuka sheria, taratibu na kanuni!.
3. Kikao cha CC ya Chadema, kilichowatimua kilikaa kama a kangaroo court na kutoa maamuzi ya kikangaroo!. Niliuliza humu Je, wabunge 19 wa CHADEMA walijiteua? Je, CC ya CHADEMA ni Kangaroo Court? Je, Baraza Kuu litabariki ukangaroo ule?
4. Katiba ya Chadema inasema mwanachama kabla hajafutwa uanachama, kwanza atatumiwa hati ya mashitaka kwa maandishi by despatch, kisha atapewa siku 14 za kujibu mashitaka. Chadema hawakuandaa hati zozote za mashitaka!. Hili Mahakama ilipaswa ilione!.
5. Baada ya watuhumiwa kupewa hati ya mashitaka, ndipo kikao cha CC kinaitishwa kama mamlaka ya nidhamu, kusoma majibu ya mashitaka, na ndipo kinawaita washikiwa na kuwasikiliza. Hili halikufanyika!.
6. Baada ya wabunge 19 wa Chadema kuapishwa, hapa Chadema waliposwa kufanya kitu kinachoitwa a due process ya nidhamu na sio zile Zimamoto za kikangaroo!. There was no emergency of whatsoever!. Mahakama ilipaswa ilione hili!.
7. Uthibitisho wa hakukuwa na any emergency ya kuitisha CC, ni the time taken, kuitisha kikao cha Baraza Kuu!.
8. Baada ya kuitishwa kikao cha Baraza Kuu, kitu cha kwanza kwa Baraza Kuu Chadema kuangalia ni uhalali wa kikao cha CC, pili jee katiba, sheria, taratibu na kanuni za mamlaka ya nidhamu ya Chadema zilifuatwa?. Hili pia niliuliza humu A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?
8. CC ya Chadema ni mamlaka halali ya nidhamu ya wabunge wa Chadema, lakini CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Halima Mdee ambaye ni Mwenyekiti wa Bawacha!, Mamlaka yake ya nidhamu ni Baraza Kuu!, CC ya Chadema ilipata wapi mamlaka ya kumtimua Halima Mdee?!. Kikao cha Baraza Kuu kilipaswa hili kukuona!. Hapa nilimpongeza Halima, "Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji
9. Japo kikao cha Baraza Kuu Chadema kiliitishwa kihalali kama mamlaka ya rufaa ya wabunge wa Chadema, lakini kitendo cha kikao hicho kubariki uamuzi wa CC kuwatimua bila kufanya mapitio yoyote, ni uthibitisho wa Chadema bado ni chama kichanga, mfano kingechukua nchi ile 2015!, it would have been disastrous!.
10. Kitendo cha Baraza Kuu kubariki maamuzi ya kikangaroo ya CC ya Chadema, kilifanya niyaite maamuzi yale pia ni ya kikangaroo, na kitendo cha Mahakama Kuu kuyabari maamuzi ya kikangaroo, "Mzoea vya kunyonga vya kuchinja Haviwezi". Hongera Halima Mdee na Makamanda wote kwa kugomea wito wa kienyejienyeji, Jee kitendo cha Mahakama Kuu yetu nayo has joined the team of Kangaroos?.
A Way Forward
1. Kwa vile Chadema imefanikiwa kuwatimua hao 19 sasa Chadema isikate tena rufaa, kupinga uamuzi huu, bali iitishe kikao cha Baraza Kuu , ASAP, kifanye a due process, hili la wabunge 19 liishe, wabunge hao 19 wavuliwe ubunge wao, Chadema wapeleke majina 19 mengine, wateuliwe waapishwe, tuwe na Bunge la vyama vingi!.

2. Chadema wakifanya tuu dillydalling kukaa rufaa, inakula kwao!. By the time rufaa inasikilizwa, ndipo kifuate kikao cha Baraza Kuu, I'm afraid the time left before the next election is too little too late, ikibaki muda wa chini ya miezi 12 kabla ya muda wa uhai wa Bunge kuisha, hakuna uchaguzi wowote wala uteuzi wowote wa wabunge wapya!.
3. Tena nashauri kikao hicho cha Baraza Kuu, pia sasa ndio kimtimue Halima Mdee, kikifuatiwa Mkutano Mkuu kuthibitisha. Hapa najua changamoto ni fedha!, kule kwenye kile chungu, zilikopatikana zile fedha za kugharimia Baraza Kuu lile, kile chungu bado kipo, kitagharimia vikao vyote viwili, na Chadema inaweza kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa mtu kupumzishwa kwa heshima na dereva mpya kupatikana!.

Paskali.



Andiko la hovyo kama author wake.
 
Kuendesha kipindi bora cha talk shows kama Oprah, Larry King, Tim Sebastian, or hata Jeff Koinage, ni vitu viwili 1. Talent 2. Resources. Tanzania tunazo hizi talents za kutosha tuu, tatizo ni resources, hivyo naungana na wewe, usitegemee kipindi bora!.

Japo hili ni kweli ila sio wote, baadhi ya wakweli tupo and its time that will prove this!.

Mimi japo kwa sasa pia ni kada, ila ukada wangu ni wa kutanguliza mbele maslahi ya taifa. Mfano mzuri ni zisikilize hoja zangu hapa
View: https://youtu.be/Qr6j25jFGyI?feature=shared kama mpaka hapa bado huioni neutrality yangu, then naomba tuu niheshimu mawazo yako.

This TV program sio program ya anything serious, ni program ya uhabarishaji na uelimishaji umma kuhusu katiba, sheria, na haki, walengwa sio watu wa calibre yako ambao mnaijua katiba, sheria na haki zenu, walengwa ni watu wa chini kabisa ambao hawaijui katiba, hawazijui sheria na hawajui haki zao, hawa ndio kipindi kitawasaidia
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=Ir97ZpO8_yWjW7Ia So my broda just relax don't expect anything serious from me and my programs at all, kwasababu the program is not for all!, wako watu ambao kipindi hiki kitawafikia na kitawasaidia!.

P

Samahani mkuu kwa swali la kizushi, huwa naona mkono wako wa kushoto kama una shida au ni macho yangu tu? pole kama ulipata ajali sisi wote ni binadamu sina nia mbaya lakini natamani tu kujua. Asante
 
Mkuu Tindo , lazima mnipe heshima yangu, mtu yoyote aliyesomea sheria level ya LL.B na kupewa uwakili ni mwanasheria!. Hivyo mimi ni wakili!

Hapa naomba kuyaheshimu mawazo yako.

Ni kweli

Ni kweli ila siasa zangu, sio siasa za kupiga blah blah ni siasa saidizi zenye kuleta matokeo chanya!.

Hiki ndicho kipindi hiki kinakwenda kufanya, kuwafundisha katiba, sheria na haki Watanzania wote, na wale masikini wa kutupwa ambao wamekosa haki kutokana na umasikini wao, tutawashika mkono na kuwasaidia kupata haki zao.
P
TBC na Channel 10 hawatakubali
 
hahaha nimecheka sn, ni changamoto hizo, mfano Halima angekuwa amefukuzwa CCM ungeandika hiki?
Mimi najihesabu ni mtetezi huru wa haki, CCM ilipomtimua Sofia Simba, nilimtetea! Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma

Siku CCM ilipomtimua Hassan Nasor Moyo, nilipandisha uzi huu Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?

Siku Benard Membe alipotimuliwa CCM, nilipandisha bandiko hili Membe, Japo Umeonewa, Usifanye Kosa la Lowassa!, Ila CCM ya Ajabu!, Uamuzi based on Illegal Evidence ni Void Ab Initial!.

Ukiwa ni mtetezi kweli wa haki, utamtetea yeyote.

P.
 
Mkuu Mzalendo Uchwara , asante, ni kweli kwenye line up yangu, nitawatafuta waalimu wangu wawili wa sheria nilipokuwa Udsm, hawa ni Dr. Tulia Akson na Prof. Ibrahim Juma. Halafu kuna mama mmoja macho mazuri fulani, pia nitamtafuta!. The program will be good!.
P

Nilikuwa nakuunga mkono ila ulipomtaja Tulia Akson nikaona kipindi hakina maana.
 
Mimi najihesabu ni mtetezi huru wa haki, CCM ilipomtimua Sofia Simba, nilimtetea! Rais Magufuli, Waliomchagua Wanajuta!, Wasiomchagua Wanamshangilia!. Akishika Chama, Watakoma

Siku CCM ilipomtimua Hassan Nasor Moyo, nilipandisha uzi huu Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano?

Siku Benard Membe alipotimuliwa CCM, nilipandisha bandiko hili Membe, Japo Umeonewa, Usifanye Kosa la Lowassa!, Ila CCM ya Ajabu!, Uamuzi based on Illegal Evidence ni Void Ab Initial!.

Ukiwa ni mtetezi kweli wa haki, utamtetea yeyote.

P.
Unatetea watu walifoji signature ya KM? Sipo pamoja na wewe
 
Unatetea watu walifoji signature ya KM? Sipo pamoja na wewe
Wewe ndio hujui, wenyewe wanajua hakuna forgery yoyote, ndio maana hawajaripoti police, forgery ni kosa la jinai, amini nakuambia majina yalipelekwa NEC na bona-fide genuine legit documents, ila ni kweli hazikusainiwa na KM, but zimesainiwa na office bearers!. Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?
P
 
Wewe ndio hujui, wenyewe wanajua hakuna forgery yoyote, ndio maana hawajaripoti police, forgery ni kosa la jinai, amini nakuambia majina yalipelekwa NEC na bona-fide genuine legit documents, ila ni kweli hazikusainiwa na KM, but zimesainiwa na office bearers!. Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?
P
Ndiyo utaratibu? polisi wanasubiri maelekezo toka juu, kesi ya Lissu wanasubiri apone atoe ushahidi sijui angekufa kusingekuwa na uchunguzi.
 
Wakati nikiwa mwanafunzi wa Shule ya msingi nilikuwa sikosi kuangalia kipindi ulichokiendesha wakati huo Cha Kitimoto. Naamini hili pia kitakuwa na ubora ule ule. Kila la heri mkuu. Jumapili nitakuwa pamoja nawe karibu ya TV yangu kuangalia umahiri wako.
 
I have always been a biker maisha yangu yote, nimeishi UK niki ride big bikes, nimeishi Italy, Swiss, Sweden na US, ndio nikarudi nayo home. Ukiwa bike lover its some sort of madness. Hili nililizungumza humu, Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo! Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?
P
Barabara za wenzetu ni tofauti na hizi zetu sn tu, nakubali lakini mazingira yetu ni hatari sn maana madereva wengi wa magari ni vichaa. yote kwa yote tumshukuru MUNGU bado tupo pamoja na wewe.
 
Back
Top Bottom