Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kiranga ni mtu smart sana,ila katika haya mambo yake ya kutoamini kama Mungu yupo si m support.

Nina imani siku moja takuja kuamini kama Mungu yupo.

Ni swala la muda tu.
Unaelewa kwamba tatizo langu na suala zima la kuwepo kwa Mungu si kuamini?

Unaelewa kwamba kwenye kuamini naweza kuamini Mungu yupo na akawa hayupo?

Unaelewa kwamba ninachoamini mimi si muhimu sana, muhimu zaidi ni ukweli wa mambo?

Kwa nini unajikita kwenye ninachoamini au nisichoamini mimi, badala ya kujikita katika ukweli ulivyo?
 
Kwahiyo ukweli ulivyo ni kwamba hakuna Mungu?ukiambiwa uthibitishe hayo madai yako unasema mwenye kutakiwa kuthibitisha yule anayesema Mungu yupo, yani ni full vituko.
 
Kwahiyo ukweli ulivyo ni kwamba hakuna Mungu?ukiambiwa uthibitishe hayo madai yako unasema mwenye kutakiwa kuthibitisha yule anayesema Mungu yupo, yani ni full vituko.
Mungu ni nini na unajuaje yupo kweli na habari za kuwapo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu?
 
Mkuu acha maneno mengi, nipe majibu kama unayo
 
Hajasema bado hivyo vitu hajui vilitokea vipi, naona unamjibia.
 
Una uhakika gani kwamba kuna namna vilitokea tokea?

Siyo unaniuliza vilitokeaje wakati wewe mwenyewe hujui kama vilitokea ama vilikuwepo tu kabla ya ujio wa muda.

Unaweza kuthibitisha kwanza kwamba kuna namna vilitokea ili swali lako la kuitafuta hiyo namna liwe na uhalali!?
 
Asante kwa kunielewa Mkuu,

Tatizo la huyo jamaa ameshajiwekea ka uhakika ka upande fulani halafu na sisi analazimisha tuwe huko huko bila kwanza kutuambia kwa nini tuwe huko.

Na nimejitahidi sana kumwelezea ili aone msimamo wangu uko wapi, kwamba hadi sasa sijui kama dunia ilianza, ilikuwepo muda wote au ilitoka mahala.

Kwa kuwa yeye tayari ana uhakika kuwa ilianza ndipo namuomba na mimi huo uhakika ili nitoke hapa njia panda niwe upande wake na kwa pamoja tumsake huyo muanzilishi.

Sasa kuniambia nimwambie tu muanzilishi wakati bado swali la msingi hajalitolea ufafanuzi ni zaidi ya kutaka anishikie akili zangu.

Huko aliko ataendelea kuwa peke yake tu na mimi nitaendelea kusubiri hapa njia panda ya ilianza, haikuanza ama ilitokea mahala pamoja na vyote vilivyomo!.
 
Sihitaji kuwa na idadi yoyote kufahamu watu wote wenye akili timamu(sio wanasayansi tu) wanafahamu uhai ulianza katika kipindi fulani hapa duniani.
Kama huna idadi ya wote huo uhakika wa kusema wanasayansi wote wanasema vile unautoa wapi?
 
Nina uhakika chochote(Matter) kilichopo kwenye ulimwengu(Space) huu tunaoishi unaoonekana kwa macho ni lazima kiwe na muda(Time) kilichoundwa na muundaji.

Hakuna chochote kinachoweza kuwepo bila kuundwa na muundaji katika ulimwengu huu unaoonekana kwa macho. Nakupa mfano tena wewe Emmanuel ni (Matter) una muda ulioundwa(Time) na aliekuunda amekuandalia mazingira rafiki uishi katika sayari hii dunia(Space). Vivyo hivyo na vitu vingine vyote (living and non living things)

Hivyo ninachokuuliza nina uhakika nacho, naomba unipe majibu niliyokuuliza kama haufahamu au hauna majibu pia niambie.

NB:Naendelea kusubiri majibu niliyokuuliza.
 
Haya maelezo haukunipa Mkuu, hukuniambia kama haujui formation ya hivyo vitu ndio maana nimeendelea kutaka majibu. Hivyo kwa maelezo yako haya itoshe kusema umekiri kwamba haujui hivyo vitu vimetokeaje?(formation) si ndio?

Ili tuendelee na mada.
 
Una uhakika upi kwamba kuna namna vilitokea tokea na wala si pengine vilikuwepo tu kabla ya ujio wa muda?
Nina uhakika hakuna chochote(Matter) kinachoweza kutokea katika muda(Time) husika na kuwepo katika ulimwengu(Space) unaoonekana kwa macho bila kuwa kimeundwa na muundaji.

Hakuna gari/pikipiki/juice/baiskeli n.k(Matter) linaloweza kutokea katika muda(Time) husika na kuwepo sehemu(Space) bila ya gari/pikipiki/juice/baiskeli n.k hiyo kuundwa na muundaji
 
Tupe huo uhakika na sisi tuone,

Maana kama hoja yako ni muda nimeshakwambia si kila mahala kuna muda,ndani ya huu Ulimwengu kuna sehemu nyingi tu muda haupo kabisa.Mambo yankuwepo yakiwa hayana jana,leo na kesho.

Weka huo uhakika wa kwamba vitu hivyo kuna namna vilitokea ili sisi tutafute majibu ya swali lako.
 
Haya maelezo haukunipa Mkuu, hukuniambia kama haujui formation ya hivyo vitu ndio maana nimeendelea kutaka majibu. Hivyo kwa maelezo yako haya itoshe kusema umekiri kwamba haujui hivyo vitu vimetokeaje?(formation) si ndio?

Ili tuendelee na mada.
Ndiyo maana Kiranga amekuweka kwenye ignore list,
Kwa sababu ni kama una kaujinga fulani hivi.

Wapi niliposema sijui formation? Kwa nini unanimezesha maneno ya formation wakati nimeshakwambia hizo habari sina uhakika nazo?

Kuna mahala umenithibitishia kuwa kila kitu kina formation ili niseme sijui formation ya vitu hivyo?

Unaweza kuthibitisha kuwa dunia na vilivyomo iliumbwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…