Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Lakini ukitizama sana na kwa undani watu wengi sana hawaamini katika Mungu hasa. Japo wengi kwa sababu za kutaka kuzikwa au kupata kukubalika na jamii hawawezi kusema ukweli huo. Ila ukitizama matendo na fikra zao halisi ....za wazi na za sirini, ni wazi hawaamini katika Mungu na hata uwezo Mungu. Hata wale wanaokwenda au kushinda katika nyumba za ibada. Deep down hawamuamini Mungu.
 
Wanaadamu wengi Sio waamini wa Mungu ila wanajiforce kuamini kwa hofu ya kiama ama adhabu zilizoandikwa kwenye vitabu..

Kusingeorodheshwa hukumu sizani kama kuna mtu angemwamin Mungu aiseee... Fumbo la umauti ndio linaforce kuamini Mungu kilazima maana hakuna namna
 
Write
your reply...kuna mengi ya kujua kuhusu@kiranga

one day tumfanyie hard talk hapa jamvini kama ilivyokuwa zamani kwa baadhi ya members
 
Misquoting jesus and jesus interupted by bart ehrman hakuna mkristo free thinker atasoma hivi vitabu bado akaamini katika biblia maana ni fact tupu zipo hapo ..lakini pia kingine ni misgoded and goded by lawrence brown....vinajaribu kuelezea the fact behind bible japo vinasapoti quran lakini biblia humo imechambuliwa kiasi cha kutosha na kwa evidence nyingi .
 
Mara nyingi nimekuwa nikiwaza huyu member hapa JF atakuwa alikutana na incident iliyomfanya akamchukia Mungu.

Hapa anaeleza namna alivyokuwa anasali na Nyerere pale St Peters




My take, huyu anahitaji kuombewa ili amrudie muumba wake.
Mshana Jr
My take, huyu anahitaji kuombewa ili amrudie muumba wake.[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Bart Ehrman nimemsoma, ukiwa na upeo wa kusoma waandishi kama huyu ukawaelewa bila kuleta figisu zile za ushabiki haya mambo ya imani za kidini utayaangalia kwa jicho la uelewa wa juu sana.

Tatizo hapa utataka mjadala na watu wengi ambao hawajasoma vitu kama hivi na jina kama la Bart Ehrman ndiyo kwanza wanalisikia.

Mimi mtu akinitajia kwamba kasoma waandishi kama hawa namuheshimu sana upeo wake, yani si lazima tukubaliane kila kitu, hata kama anatetea uwepo wa Mungu na Ukristo/Uislamu, akitetea kwa level ya kuweza kukanusha hoja zilizomo kwenye vitabu kama vya Ehrman anakuwa level tofauti na wafia dini wa kawaida wa JF ambao wamekaririshwa aya wanazipigania kwa identity tu hata kuzitetea kwa mantiki hawawezi.

Umenifurahisha sana kunitajia Bart Ehrman. Jamaa kasoma Princeton Theleogical Seminary, anaichambua Biblia kwa umakini wa mtu aliyesoma Priceton Theological Seminary, halafu anaikosoa.

Huyo Lawrence Brown sijamsoma nitamtafuta.
 
Mara nyingi nimekuwa nikiwaza huyu member hapa JF atakuwa alikutana na incident iliyomfanya akamchukia Mungu.

Hapa anaeleza namna alivyokuwa anasali na Nyerere pale St Peters




My take, huyu anahitaji kuombewa ili amrudie muumba wake.
Mshana Jr
Kiranga ni mlemavu, alizaliwa mzima baada ya kupata ulemavu ndio akamchukia Mungu. Nasikia hata jicho lake anagawa.
 
Mara nyingi nimekuwa nikiwaza huyu member hapa JF atakuwa alikutana na incident iliyomfanya akamchukia Mungu.

Hapa anaeleza namna alivyokuwa anasali na Nyerere pale St Peters




My take, huyu anahitaji kuombewa ili amrudie muumba wake.
Mshana Jr
Kuna maswali mengi yanaweza kufanana mantiki yake. Mojawapo ni hili: Judas Iscariot alikuwa mmoja wa mitume 12 wa Yesu, ilikuaje akamkana Yesu.
 
Akili za Kiranga hazichunguziki mkuu, huyu ni miongoni mwa watu wenye uelewa na uwezo mkubwa sana wa kuchambua na kuelezea mambo kwa marefu na mapana, huku yote yakiwa kwa ufasaha.
Kama hivyo ndivyo, basi angekuwa na uwezo mzuri wa kuweza kumwelezea Mungu "kwa uwezo mkubwa sana wa kuchambua na kuelezea mambo kwa marefu na mapana, huku yote kwa ufasaha". Badala ya kufanya hivyo, yeye anasema "Mungu hayupo" - yaani anakana kuwepo kwa Mungu.
 
Mkuu, umeongea kitu muhimu sana.

Watu wengi matendo yao hayaoneshi kwamba wanaamini Mungu, na ironically, mara nyingine sisi tusioamini Mungu ndio tunaotenda matendo yanayoendana na imani za kuamini Mungu.

Nitakupa mfano mmoja mdogo tu.

Nilikuwa katika kundi moja, mtu mmoja akawa analalamika anaumwa katika hilo kundi.

Wale watu wa kwenye hilo kundi wote wanajinasibu na imani ya Mungu.Kila mmoja akawa anasema "tutakuweka kwenye maombi", na "Mungu atakusaidia".

Mimi siamini katika maombi wala Mungu kumsaidia mtu mwenye matatizo, kwa sababu siamini Mungu yupo. Nakwenda kwa falsafa za kwamba, matatizo ya mtu yatamalizwa na mtu, maombi ni kujiliwaza tu na Mungu hayupo.

Nikaguswa sana na kilio cha yule mtu, ni dada wote tunamjua, hana uwezo, na pale kwenye kikundi kuna watu wana uwezo wa kumsaidia wanajibalaguza kumuombea kwa Mungu.

Mimi nikatembeza muamala chapchap yule dada asaidiwe, nikamtumia rafiki yetu mwingine alikuwa Dar alikuwa na wasaa wa kuweza ku organize mgonjwa apelekwe hospitali.

Kuna rafiki yetu mwingine daktari aka arrange hospitali yule dada apokewe.

Ndani ya muda mfupi ule muamala wangu ukawa umeshawezesha yule mgonjwa akatiwe bima, aanze matibabu.

Huku wengine waliojikita kumuombea mgonjwa kwa Mungu wakawa kama wameona aibu, ukatembea mchango kusaidia mgonjwa.

To make a long story short, wale watu wanaoamini Mungu waliofundishwa usamaria mwema na kusaidia watu wenye matatizo wote walikuwa wanaangaliana wakati mwenzao, rafiki yao waliyemjua kwa miaka mingi anakaribia kufa. Na ninaposema anakaribia kufa si utani.Yule rafiki yetu daktari alikuja kutuambia kwamba pale tungechelewa kidogo tu habari ingekuwa tofauti sana.

Nikatokea gubegube tu hata siamini Mungu yupo, lakini kwa sababu siamini Mungu yupo hilo ndilo limenipa wajibu mimi kufanya kazi ya kusaidia mwenyewe bila kumsukumizia mzigo huo Mungu, kwa sababu najua Mungu hayupo. Nikaanzisha msaada chapchap.

Sasa hapo utaona wasioamini Mungu wanafanya usamaria mwema kirahisi kama vile wanaamini Mungu, wanaoamini Mungu wameendekeza ubinafsi.

Hii dunia kama watu wangekuwa kweli wanaamini Mungu yupo kama wanavyodai, maovu mengi sana yangetoweka.

Watu wanaiba mpaka misikitini. Waziri Mkuu katudanganya msikitini kwamba rais mzima anapiga kazi.

Halafu utaambiwa huyo naye anaamini Mungu.

Ni kweli anaamini Mungu?

Bora hata mimi nimesema siamini Mungu na sijadanganya msikitini kama yeye!
 
Unaweza kuthibitisha kimantiki kwamba Mungu yupo?
 
Bila shaka Mr kiranga alisoma kitabu kinacho itwa doctrines. Na hayo ndio majibu alio pata. (Thibitisha mungu yupo). Ukimuendekeza kufuru huwezi ikwepa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…