Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Siku ukipata majanga ya kidunia ndo utamkumbuka Mungu huku ukiwa umepiga magoti ukimlilia lakini itakuwa too late....

Sent using Jamii Forums mobile app
Majanga ya kidunia ni uthibitisho kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye upendo wote na uwezo wote hayupo.

Angekuwepo, asingeumba dunia ambayo viumbe wake wanaweza kupata majanga.

Kwa hivyo, nikipata majanga ya kidunia, hayo majanga nayo yatakuwa ni sehemu ya uthibitisho kwamba Mungu huyo hayupo.
 
Unauliza swali halafu ukijibiwa unalazimisha jibu lako unalotaka wewe?

Kwa nini unaogopa sana kumtaja huyo Mungu wako tumjadili?

Unamuonea aibu?

Unajua ukimtaja huwezi kutetea uwepo wake?
 
Unauliza swali halafu ukijibiwa unalazimisha jibu lako unalotaka wewe?

Kwa nini unaogopa sana kumtaja huyo Mungu wako tumjadili?

Unamuonea aibu?

Unajua ukimtaja huwezi kutetea uwepo wake?
Mimi sijalazimisha ujibu navyotaka mimi, nimekuuliza Mungu ni nini unakazana kusema ni dhana tu basi ndio tumeishia hivyo sasa sijui hapo cha kujadili ni nini wakati ushamaliza mjadala kwa kukomaa kusema Mungu ni dhana tu.
Sasa sijui unataka nikueleze nini tena cha ziada?
 
Hatuwezi kujadiliana kwa sababu wewe unamuonea aibu Mungu wako.

Hutaki hata kumtaja yukoje.

Sasa tutajadiliana vipi kuhusu Mungu ambaye hutaki hata kumtaja?
 
Hatuwezi kujadiliana kwa sababu wewe unamuonea aibu Mungu wako.

Hutaki hata kumtaja yukoje.

Sasa tutajadiliana vipi kuhusu Mungu ambaye hutaki hata kumtaja?
Wewe umesema Mungu ni dhana, sasa nimtaje Mungu gani tena mwengine wakati ushamaliza kuwa Mungu ni dhana?

Nilikwambia ueleze Mungu ni nini ila ukashikilia tu kusema kwamba ni dhana tu kwamba ni jambo la kufikirika tu hukutaka tujue Mungu ni kitu gani, sasa unaanzaje kuniambia nikutajie Mungu wangu wakati hujaeleza huyo Mungu ni kitu gani, nitakutajia nini sasa maana dhana ziko nyingi na wewe umeishia kutuambia Mungu ni dhana sasa sijui nikutajie dhana ipi.
 
Huna hoja, kubali huna pa kutolea umebanwa kote
 
Unayeamini Mungu yupo ndiye mwenye wajibu na ndiye unayepaswa kusema Mungu ni nini. Kuwasukumizia hili swali watu wasioamini yupo ni kupoteza muda kitoto tu.
 
Unayeamini Mungu yupo ndiye mwenye wajibu na ndiye unayepaswa kusema Mungu ni nini. Kuwasukumizia hili swali watu wasioamini yupo ni kupoteza muda kitoto tu.
Tofauti ni ipi kati ya anayeamini Mungu(anasema yupo) na anayesema Mungu hayupo/hakuna?

Maana wote wawili wanakielewa hicho kitu ndio maana mmoja anadai hicho kitu hakipo na mwengine anadai kipo, sasa hapo inakuaje mmoja tu ndio awe na wajibu wa kukielezea hicho kitu? huo wajibu umejengeka kwa msingi gani? hebu tujaribu kuelewa muache kukariri tu.
 
Nikisema mungu ni dhana ya kufikirika nitakua nimejibu swali lako?
 
Nikisema mungu ni dhana ya kufikirika nitakua nimejibu swali lako?
Bado hujajibu kwa sababu mimi sijauliza kama Mungu ni jambo la kufikirika au kitu halisi,sasa ukiishia tu kuniambia kuwa Mungu ni dhana bado nakuwa sijaelewa Mungu ni kitu kitu gani hasa ni Superman au Alien?
 
Bado sijajibu ina maana jibu sahihi unalijua?

Unaweza ukaliweka hapa ili tuone kama lina pishana na jibu langu?
 
Bado sijajibu ina maana jibu sahihi unalijua?

Unaweza ukaliweka hapa ili tuone kama lina pishana na jibu langu?
Ah kwahiyo kama nikikuuliza rais wa Marekani ni nani halafu ukajibu ni Magufuli kisha nikakataa maana yake lazima nitakuwa najua rais wa Marekani nani ndio maana nimekataa Magufuli(ambaye ni marehemu) kuwa ndio rais wa Marekani?
 
Siwezi kukurupuka kujibu swali bila kupata ufafanuzi wa swali lako kwanza

Raisi wa marekani, ni finctional au realistic?

Marekani ipo au haipo?

Tunaweza kuthibitishika uwepo wake?

Tukimaliza hapo tutarejea kwenye swali lako ili tuone kwa njia hizo hizo tulizotumia hapo juu kama tunaweza kuthibitisha huyo mungu yupo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…