Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

mi najua, na nimekujibu kua Mungu ni dhana ya kufikirika, niambie wewe maana ya mungu ni nini?
Ni dhana ipi hiyo? ile ya kuamini ukifa utazaliwa upya na kuja kuishi tena duniani au ya kuamini ukimfanyia mtu ubaya na wewe utakuja kutokewa na jambo baya? au unzungumzia zile dhana za kuhusu Freemason na Alien?

Mungu ni dhana ipi sasa mbona haiweki wazi ili nijue unazungumzia dhana gani?
 
Akili za Kiranga hazichunguziki mkuu, huyu ni miongoni mwa watu wenye uelewa na uwezo mkubwa sana wa kuchambua na kuelezea mambo kwa marefu na mapana, huku yote yakiwa kwa ufasaha.
Usimpe nafasi ya uungu.

Ukidhani anajua sana lakini kumbe hajui lolote, anasindikiza wengine tu[emoji1787][emoji1787]
 
Mungu ni nini? hilo ndio nataka kulijua kwanza kutoka kwako.
Nimekuambia Mungu ni dhana ya kufikirika isiyo na uhalisi nje ya ulimwengu wa dhana tu.

Kama unabisha, taja Mungu yeyote ambaye yupo nje ya ulimwengu wa kufikirika tu.

Ukiniuliza dhana gani ya kufikirika, itabidi unitajie Mungu gani, kwa sababu kila Mungu ni dhana tofauti ya kufikirika, na hivyo swali la dhana gani ya kufikirika bila kumtaja Mungu halina mantiki.

Sasa jibu swali.

Taja Mungu ambaye yupo nje ya dhana ya kufikirika tu.

Ukishindwa, umeshindwa kukanusha kwamba Mungu ni dhana ya kufikirika tu.
 
Mungu ni dhana ya kufikirika, hiyo ndio tafsriri yangu niliyokupatia una hoja diffensively inayooelezea maana ya mungu kinyume na hapo?

Iweke hapa
 
Mungu ni dhana ya kufikirika, hiyo ndio tafsriri yangu niliyokupatia una hoja diffensively inayooelezea maana ya mungu kinyume na hapo?

Iweke hapa
Kwamba hili neno la kiswahili "Mungu" lina maana ya dhana ya kufikirika? kwamba mfano naweza kusema kuwa uwepo wa Superman ni mungu?
 
Sasa nitakutajia kitu gani maana haujasema Mungu ni kitu gani zaidi ya kusema ni jambo la kufikirika ila hujaeleza?

Ok kwakuwa uelewa wako umekuwa mzito kuelewa katika hili acha niende kwa vile unavyoelewa, jibu la swali lako ni Beyonce,jua,sanamu,miti.

Haya nishajibu swali lako.
 
Kwa nini Beyonce, jua, sanamu, miti ni Mungu, na si dhana tu kwamba ni Mungu?
 
Kwa nini Beyonce, jua, sanamu, miti ni Mungu, na si dhana tu kwamba ni Mungu?
Umeniambia nikutajie Mungu asiyedhana ya kufikirika, ndio nimekutajia Beyonce ambaye yupo kwa hakika halina ubishi na pia nimekutajia jua miti sanamu ni vitu ambavyo vipo kweli si vya kufikirika.

Sasa kama na hivyo ni vya kufikirika wewe ndio ueleze sasa.
 
Umeniambia nikutajie Mungu asiyedhana ya kufikirika, ndio nimekutajia Beyonce ambaye yupo kwa hakika halina ubishi na pia nimekutajia jua miti sanamu ni vitu ambavyo vipo kweli si vya kufikirika.
Nimekuuliza unajuaje kwamba habari ya kwamba Beyonce, jua, miti ni Mungu si dhana ya kufikirika tu?

Hujajibu.

Kumbuka, sijapinga kwamba Beyonce yupo, jua lipo, miti ipo.

Nahoji uwepo wa Mungu.

Usichanganye mambo.

Sasa unahakikishaje Beyonce ni Mungu, na habari ya kwamba Beyonce ni Mungu si dhana tu ya kufikirika?
 

Haiwezi kuwa dhana ya kufikirika kwa sababu ni vitu ambavyo vipo kweli si dhana tu,mungu Beyonce ni kweli yupo si kitu cha kudhania tu kwahiyo kama unahoji uwepo wa mungu basi Beyonce yupo kweli jua lipo kweli..sasa utasemaje ni vitu vya kufikirika? kumbuka umeniambia nikutajie mungu ambaye si wa kufikirika.
 
Hujathibitisha Beyonce ni Mungu.

Thibitisha.
 
Hujathibitisha Beyonce ni Mungu.

Thibitisha.
Wewe umeishia kusema Mungu ni dhana ya kufikirika hukueleza Mungu ni nini? sasa unapotaka nikuthibitishie uungu wa Beyonce unategemea kutatumika vigezo gani?
Nikikwambia Beyonce ni mungu kwa sababu nimwiimbaji maarufu utakubali kuwa kweli Beyonce ni mungu?
 
Kwa hiyo sifa ya Mungu kwako ni kuwa muimbaji maarufu?
 
Kwa hiyo sifa ya Mungu kwako ni kuwa muimbaji maarufu?
Unaniuliza mimi tena sifa ya Mungu? mimi muda wote nakuuliza Mungu ni nini unajibu ni jambo la kufikirika na kuniambia kama naweza nikutajie Mungu ambaye si dhana tu.

Hujajibu nikikwambia Beyonce ni mungu kwa sababu ni mwiimbaji maarufu utakubali uungu wake?
 
Ndio nataka kuelewa kutoka kwako ndio maana nauliza vizuri, kwamba nikisema Supermani ni mungu nakuwa namaanisha Superman ni dhana?
Unataka kuelewa kutoka kwangu alafu ukieleweshwa unakataa, nikueleweje?

We ni atheist?
 
Nimekuuliza sifa ya Mungu ni kuwa muimbaji maarufu?

Uimbaji maarufu una uhusiano gani na kuwa Mungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…