Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Nimekuuliza sifa ya Mungu ni kuwa muimbaji maarufu?

Uimbaji maarufu una uhusiano gani na kuwa Mungu?
Sasa hapo ndio tunarudi kwenye lile swali langu la msingi la Mungu ni nini?

Mimi nishakwambia Beyonce ni mungu kwa sababu ni mwiimbaji maarufu, wewe kama unapinga eleza sifa za Mungu ni zipi au Mungu anatakiwa aweje ili tuweze kujua Mungu ni ni ni hasa?
 
Natumia plan B kukuelekeza

We ni muumini wa dini gani?
Unielekeze nini ambacho unadhani nashindwa kukuelewa?
Hoja kuu ni Mungu, huko kwenye dini kila dini ina maelekezo yake sasa tukiingia huko hatutaelewana maana wewe hata dini yenyewe hauamini pia.
 
Unielekeze nini ambacho unadhani nashindwa kukuelewa?
Hoja kuu ni Mungu, huko kwenye dini kila dini ina maelekezo yake sasa tukiingia huko hatutaelewana maana wewe hata dini yenyewe hauamini pia.
Ngoja nikubadilishie swali naona hilo linakubana sana

Hiyo elimu ya uwepo wa mungu umejifunzia kupitia marejeo gani?
 
Ngoja nikubadilishie swali naona hilo linakubana sana

Hiyo elimu ya uwepo wa mungu umejifunzia kupitia marejeo gani?
Mbona unazunguka sana kijana? hebu eleza unachotaka kueleza, nishakwambia hoja kuu hapa ni Mungu na unajua sio wote wanaoamini Mungu ni kwamba wanaamini na dini.
 
Mbona unazunguka sana kijana? hebu eleza unachotaka kueleza, nishakwambia hoja kuu hapa ni Mungu na unajua sio wote wanaoamini Mungu ni kwamba wanaamini na dini.
Nazunguka kwasababu unanizungusha kwa kutojibu maswali, jibu swali ili niweze nikueleweshe maana ya mungu ambayo huijui

Kwa hiyo wewe leo unakana kua huna dini?

Maarifa ya mungu umeyapata kupitia source gani?
 
Nimekwambia habari kuu hapa ni Mungu huko kwenye dini kila dini ina maelekezo yake na wengine hawana dini, nimeweka wazi kuwa sihitaji kujibu habari za mimi na dini hivyo sio kwamba nakuzungusha.
 
Nimekwambia habari kuu hapa ni Mungu huko kwenye dini kila dini ina maelekezo yake na wengine hawana dini, nimeweka wazi kuwa sihitaji kujibu habari za mimi na dini hivyo sio kwamba nakuzungusha.
Hata hii ni sehemu ya habari kuu, kuongelea ongelea habari kuu bila ku focus kwenye maswali nayo kuuliza yenye mlengo wa kukuelewesha kunaonesha wazi kua kuna kitu unakikwepa

Kwanini unogopa kujibu habari za wewe na dini wakati dini inafungamana na habarinza mungu?

Kwa hiyo leo unakiri kua hauna dini?

Au una dini ila hautaki kukubali kwasababu unajua kukubali kwako kutakuweka matatani kwenye mjadala?
 
Nimekwambia kuna watu hawana dini ila wanaamini Mungu, sasa sijaelewa wewe ni kipi hicho ambacho unashindwa kunieleza hadi tuzungumzie masuala ya dini wakati hoja kuu hapa ni Mungu na si dini?

Swali la Mungu ni nini umeshindwa kulielewa ndio maana uliishia kusema Mungu ni dhana kitu ambacho si jibu la swali lililoulizwa, sasa hatujaelewana hapo unataka kuingiza mjadala wa dini. Wewe kama hilo swali la Mungu ni nini limekushinda ni bora ukasema tu kuliko kutaka kujizungusha huko kwenye dini.
 
Sasa mimi nauliza nataka kujua kama nawewe ni miongoni mwa hao watu wanao amini mungu bila dini au la ili niweze kujua na dili na mtu wa namna gani

Kwa hiyo wewe una kiri kwamba hauna dini?
 
Sasa mimi nauliza nataka kujua kama nawewe ni miongoni mwa hao watu wanao amini mungu bila dini au la ili niweze kujua na dili na mtu wa namna gani

Kwa hiyo wewe una kiri kwamba hauna dini?
Hiyo ni mada mpya kabisa, kama unakubali tujadili masuala ya dini ambayo ni mada mpya sawa mi nipo radhi.
 
Hiyo ni mada mpya kabisa, kama unakubali tujadili masuala ya dini ambayo ni mada mpya sawa mi nipo radhi.
Mada ya huu uzi ni "Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?"

Wewe umekuja na mada mpya ya kuuliza mungu ni nini lakini hatujakataa tusiijadili kwa kusema hiyo ni mada mpya

Jibu swali, wewe ni muumini wa dini gani? Au unakiri kwamba wewe hauna dini?
 
Kwamba hili neno la kiswahili "Mungu" lina maana ya dhana ya kufikirika? kwamba mfano naweza kusema kuwa uwepo wa Superman ni mungu?

Mimi sina uwezo mkubwa wa kuelewa mambo, ila haya majibu unayotoa, afadhali uje ujadiliane na mimi, Kiranga na wenzake ni kama unawasumbua, huna uwezo wa kujibu hoja zao.

afadhali ubishane na mimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…