Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Heheeeee taratibu mbona maswali mengi

Haya tulia nikupe majibu

-kuhusu malaika tafadhali acha kuniuliza vitu ambavyo ni vya kufikirika, sijawahi ona huyo kiumbe, na siamini kama kweli anaexist kwa ulimwengu huu AMBAO UPO REAL. jomba yaani ni sawa na kuniuliza kusud la kuumbwa babu chrismass au tooth fairy

-sitatofaitisha kati ya malaika na mwanadamu, nitatofsutishaje na kitu cha kufikirika, ivi ulikiwa wawaza nini kuuliza swali kama hilo. Yaani ni sawa na mtu anayeuliza tofauti ya john cena na thano.... Upo

-huwezi kuja kichwa kichwa unakuja na kuniuliza swali ambalo toka enzi na enzi halina jibu juu ya dhumuni la uwepo wetu hapa duniani ukitegemea ntakupatia jibu, ivi unafikiri jibu la hilo swali linaweza kuenea kwenye server za jamii forum, xiiu
- asiruhusu ..... Hayo tafuta sentensi zako acha kuparamia na kugeuza sentensi UNAFIKIRI NAFANYA MZAHAAA HAPAA
Kwanini huamini uwepo wa malaika kwasababu hujawahi kuwaona ? Seriously mkuu ? Ebu nipe sababu nyingine sio hii !!

Ni sawa na kusema huamini uwepo wa electricity ( umeme ) kwasababu hujawahi kuuona !!

Una uhakika gani kuwa hilo swali halina jibu tokea enzi na enzi ? Je, Hujawahi kupewa jibu kabisa ? Au, ulipewa jibu ila halijakuridhisha ?
 
Sawaa, ila hujajibu swali la kwanza kbs, ambalo ndo main question.

Kwanini Mungu asiruhusu yatokee hayo ?
Hilo swala nimeshaainisha mbona ukisoma vizuri maelezo yangu nilisema mambo mema na maovu ni kwa macho yetu na uelewa wetu sisi wanadamu

Ukija kwa muumba hakuna jema wala baya yote ni yake na ameruhusu yatokee kwenye ulimwengu wake

Yeye hana kazi kulinda au kuepusha majanga kwa mwanadamu bali yeye ni kulinda sheria za asili za ulimwengu, sheria zinazofanyiza uwepo wa huu ulimwengu wanasayansi wameona baadhi ya hiz shria kama kanuni ya pythagoras na nk
 
Kwanini huamini uwepo wa malaika kwasababu hujawahi kuwaona ? Seriously mkuu ? Ebu nipe sababu nyingine sio hii !!

Ni sawa na kusema huamini uwepo wa electricity ( umeme ) kwasababu hujawahi kuuona !!

Una uhakika gani kuwa hilo swali halina jibu tokea enzi na enzi ? Je, Hujawahi kupewa jibu kabisa ? Au, ulipewa jibu ila halijakuridhisha ?
Umeme hahahaaa ukishika nyaya inanasa

Wewe umewahi kuwaona hao malaika embu niambie wanafananaje
 
Kwasababu wakatoliki wanaabudu masanamu

Ukiwa muumin wa dini zinazo kufuru mwisho wa siku utasema tu hakuna Mungu maana ulikua unaishi ndani ya upotofu kwa muda mrefu
 
Umeme hahahaaa ukishika nyaya inanasa

Wewe umewahi kuwaona hao malaika embu niambie wanafananaje
Anhaa kumbe kitu kinachokufanya uamini uwepo wa umeme ni baada ya kushika nyaya ( lakini haujauona )... Huoni kwamba unajiContradict na ile statement yako kwamba huwezi kuamini uwepo na kitu ( mfano malaika ) kwasababu hujawahi kuwaona.... Is that logically correct ? Je, ni sahihi mtu kusema haamini uwepo wa kitu kwasababu hajakiona ?

Mm sijawahi kuwaona malaika,, lakini hii hainipi nafasi ( logically) kusema kwamba malaika hawapo !!
 
Mkuu Kiranga watu wanapenda kujua maisha yako binafsi, maana unawachanganya unajua mambo mengi kiundani na huwa huyumbishwi,

Watu wanatamani kujua historia ya elimu yako, ilikuaje ukawa atheist, ilikuaje ukaingia kwenye dini ya buddhism n.k

All in all watu wanatamani kuwa kama wewe na huo ndio msingi wa huu uzi, kama hutojali waeleze hata kwa kuweka codes
 
Ebu nenda kamsome huyu bwana ndo uje kwangu Rene descartes - meditation on first philosophy
Ila anza kwanza na huyu emanuel kant - criticue of pure reason

Labda waweza kuelewa ngoma nayocheza
 
Heheeeee taratibu mbona maswali mengi

Haya tulia nikupe majibu

-kuhusu malaika tafadhali acha kuniuliza vitu ambavyo ni vya kufikirika, sijawahi ona huyo kiumbe, na siamini kama kweli anaexist kwa ulimwengu huu AMBAO UPO REAL. jomba yaani ni sawa na kuniuliza kusud la kuumbwa babu chrismass au tooth fairy

-sitatofaitisha kati ya malaika na mwanadamu, nitatofsutishaje na kitu cha kufikirika, ivi ulikiwa wawaza nini kuuliza swali kama hilo. Yaani ni sawa na mtu anayeuliza tofauti ya john cena na thano.... Upo

-huwezi kuja kichwa kichwa unakuja na kuniuliza swali ambalo toka enzi na enzi halina jibu juu ya dhumuni la uwepo wetu hapa duniani ukitegemea ntakupatia jibu, ivi unafikiri jibu la hilo swali linaweza kuenea kwenye server za jamii forum, xiiu
- asiruhusu ..... Hayo tafuta sentensi zako acha kuparamia na kugeuza sentensi UNAFIKIRI NAFANYA MZAHAAA HAPAA

Aisee!!! Mnatabu sana enyi viumbe mliopotea, pumzi inawahadaa, mnaongea vitu sivyo kabisa. Sasa mjomba ee, subiri kifo kikukute, huko hakuna wa kukusaidia si kiranga, baba wala mama yako, wewe na matendo yako. Kwa maana ukiwa "umeshasilimu na kuwa Muislamu"
 
Mi najua kama kuna pepo kweli basi kiranga ataingia unajua kwanini?
Wengi wanafata dini lakin hawafati yaliyomo ktk dini that's why watu wengi no waislam na wakrtso na wayahud na wabudha lkn wizi dhuluma kuua kuiba kubaka kutapeli duniani haya mambo hayaishi
Lakin mtu kama kiranga na wengine wasioamni wanakuwa na utu na kuthamini wenzao

Ibilisi mtoto wa shetani, Endelelea tu kumpoteza ndugu yako, mtakutana pamoja Fii naari jahannam, mtakua kuni za motoni.,.
 
Mkuu Kiranga watu wanapenda kujua maisha yako binafsi, maana unawachanganya unajua mambo mengi kiundani na huwa huyumbishwi,

Watu wanatamani kujua historia ya elimu yako, ilikuaje ukawa atheist, ilikuaje ukaingia kwenye dini ya buddhism n.k

All in all watu wanatamani kuwa kama wewe na huo ndio msingi wa huu uzi, kama hutojali waeleze hata kwa kuweka codes

Sijui mjinga gani huyo atatamani kuwa kama ma-atheists
 
Shida kubwa ya mambo yote haya, ni kwa sababu ya kushindwa au kutafuta kujibu maswali magumu na msingi kama haya:

Nini mwanzo wa vitu, nini hatima ya vitu? Kwanini duniani kuna ubaya, unatoka wapi?

Licha ya maarifa ya sayansi lakini bado hakuna majibu wazi ya maswali hayo. Haifahamiki bado waziwazi.

Katika maswali hayo, suala sio Mungu lakini tunafafanuaje "Mungu."

Swali la msingi hapa ni Mungu maana yake ni nini?

Msingi wa yote ni Mungu. Hivyo kuzingatia biblia au maandiko matakati bila kujua maana ya Mungu ni nini hakuna maana.

Huyu tunaeita Mungu au hiki tunachoita Mungu ni nini? Hili ndilo swali msingi linalotangulia yote.

Hatuwezi kujua kama Mungu yupo au hayupo kama hatujajua Mungu maana yake ni nini. Bila hili tunajidanganya.

Wengine watasema hakuna haja ya hilo, ila kwa kuwa na imani tu. Swali ni lile lile imani ni nini?

Imani kwa ufupi, ni kuwa na uelewa wa kina wa mambo, maarifa na elimu ya vitu. Kinyume chake huna imani.

Nafahamu kidogo mafundisho ya Kanisa katoliki.

Mafundisho ya imani na maadili ya kanisa katoliki (Katekisimu ya Kanisa Katoliki) yanafafanua vizuri maandiko matakatifu, mapokeo matakatifu, imani, maadili na Mungu.

Ukisoma vizuri Katekisimu ya Kanisa Katoliki hutaona tu mwanzo wa vitu, hatima yao lakini pia mwanzo wa ubaya na hatima yake.

Utaona pia sheria ya maadili na sheria ya maumbile (The moral law and The Natural moral law).

Muhimu zaidi utaona kuwa Mungu bado ni fumbo; hajawa wazi kwetu bado. Hapa haina maana kwamba kazi zake hazionekani.

Ukichagua kuwa mtu wa kujifunza na kutafuta ukweli huwezi kupingana na mafundisho ya imani na maadili ya Kanisa katoliki.

Unaweza kutotambua au kupinga makrelo lakini huwezi kujitenga na Kanisa lifundishavyo.

Ukani --- Mungu umekuwepo wakati wote wa historia ya mtu. Mara zote hoja zimekuwa na zinaendelea kuwa zile zile.

Kuna sababu nyingi kwa nini Ukani ---Mungu lakini sababu kuu ni kufafanua "Mungu" (What is the definition of God).

Ukishindwa kufafanua Mungu huwezi kuthibitisha uwepo wake. Tunaweza kuthibitisha uwepo wa kitu au kutokuwepo kwake pale tunapoweza kufafanua hicho kitu.

Nirejee hapa andiko la James Kugel ---"In How to Read the Bible", madai yake dhidi ya masimulizi matakatifu ya biblia, kwa mfano simulizi la Adamu na Hawa na waandishi wa vitabu vingine vya biblia yamefafanuliwa vizuri na Kanisa katoliki.

Kama anavyobainisha Prof. Kugel, Kanisa katoliki linafundisha kuwa Adam na Hawa ni majina yanayowakilisha watangulizi wetu.

Hakuna anayefahamu kwa hakika kwamba mtu wa kwanza kuumbwa alikuwa Adamu na mwingine Hawa. Hii ni kwasababu hakuna anayejua kwa hakika dunia ilianza lini. Yote hayo ni masimulizi na makisio.

Watu wanaokana uwepo wa Mungu wamechagua kutokujifunza. Lakini hatahivyo, katika kuishi kwao watakiri uwepo wake.

Watu wanaodai kwamba dini (hapa nataka kuweka wazi kuwa kuna dini ya uongo kwa hiyo, wajibu wa mtu ni kujuwa dini ipi ni dini ya uongo, na ipi ni dini ya kweli) ni ujanja wa watu fulani (hapa mara nyingi wanarejelewa wazungu) walioanzisha kwa sababu za kiuchumi na utawala; madai hayo ni ya watu wasio jua historia yao na historia ya mtu.

Mambo haya ya dini na imani hayajaanza leo; si mambo ya watu fulani, ni ya watu wote lakini yenye kasoro nyingi.
 
Ibilisi mtoto wa shetani, Endelelea tu kumpoteza ndugu yako, mtakutana pamoja Fii naari jahannam, mtakua kuni za motoni.,.
Ndugu yangu kwani mm nasema uongo au jiulize kwanini wengi wenu pamoja na kwenda kanisani na msikitini lakin mna fanya maovu mengi au dini ndio zinazosema mfanye hayo.
Kiranga ni mtu safi kama pepo ipo atakaa karibu na yesu na Muhammad
 
uki
Aisee!!! Mnatabu sana enyi viumbe mliopotea, pumzi inawahadaa, mnaongea vitu sivyo kabisa. Sasa mjomba ee, subiri kifo kikukute, huko hakuna wa kukusaidia si kiranga, baba wala mama yako, wewe na matendo yako. Kwa maana ukiwa "umeshasilimu na kuwa Muislamu"
Na wewe subiri ukikute kifo ndo utaeleza kwa nini ulikiwa watishia watu kifo wakati hata wewe mwenyewe hukijui unadanganya watu kama unakijua
 
Back
Top Bottom