Ahsante sana mkuu kwa kutunza kumbukumbu.
Nilipata miito miwili kwa wakati mmoja, kuchagua kuwa Buddhist Monk milima ya Himalaya, au kwenda Wall St. kupiga dola.
Hapo nilikuwa natafsiri "
The Dhammapada" na rafiki yangu Andy Nyerere kwenda Kiswahili.
Nikamuachia mikoba Andy mimi nikakwea pipa.
Mpaka leo sijui kama Andy alimaliza ile kazi, maana nilipotezea mawasiliano na Africa kwa muda fulani.
Kwa waliopenda kujua kwa nini niliamua kuacha kuamini uwepo wa Mungu, nitaweka kitabu kilichonishawishi mara ya mwisho kabisa, kinaitwa "The Philosophy of Religion: An Anthology".
Hususan kuna sehemu wanaongelea "the problem of evil".
Ni kitabu kizuri sana kina arguments nzuri na nyingi za kutetea uwepo wa Mungu na kupinga uwepo wa Mungu, ni falsafa pana sana.