Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Weka picha yake hapa tumuone basi.Una uhakika gani kwamba Mola haonekani ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Weka picha yake hapa tumuone basi.Una uhakika gani kwamba Mola haonekani ?
Kwanini asiumbe ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea ?Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea ni contradiction.
Kwa nini kaumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea na hakuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani hakuna contradiction.Kwanini asiumbe ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea ?
Angeumba ulimwengu ambao hakuna mabaya yoyote,, bado kuna watu wangejitokeza kuhoji ( logically ) kwanini Mungu hajaruhusu mabaya kutokea ?
Kwahiyo kutoumba ulimwengu ambao hakuna mbaya ndo inathibitisha kuwa hakuna Mungu ?
Contradiction ipo wapi hapo ?
Huo ni ufinyu wako wa kufikiri, lakini sio contradiction
Lete hoja nyingine !!
Thibitisha kwamba anaonekana.Kwahiyo kama hakuna picha yake inathibitisha kwamba haonekani ?
[emoji16][emoji16] nimependa sana kwa namna ulivyompa huo ufafanuzi sijui kama atakuelewa?Najua na nimefanya makusudi. Kwanini iwezekane kila mtoto akizaliwa awe ni muislam ila baadaye abadilishwe na dunia? Kama ukristo ulikuwapo kabla ya uislam na Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote,kwanini na Muhamad asiwe miongoni mwao. Sijui kama utaelewa mantiki ya niandikayo.
Kama ni habari za kweli vipi hatupaswi kuziamini na kuzifanyia kazi ?Fikra za utumwa ni wewe kuamini miungu ya waarabu ngano zao na mapokeo ya kale ya jamii hizo na kuzipractice katika maisha halishi ya Sasa
Shida yako huja hoja na hutetei unachokiamini,unaishia kulalama jaribu kujenga hoja.Kama sio ujuha na uwendawazimu ni nini Kama sio ugonjwa wa akili ingali wewe ni mtu mweusi Wala huna
Sasa unaniamsha vipi wakati wewe umelala usingizi wa PONO,amka kwanza wewe kisha tujadiliane jambo hili kwa uadilifu na uwazi bila jazba za kipuuzi.Ndio maana nasema amka ewe mtu mweusi utoke katika fikra mfu za hizo jamii zao!
Lengo siyo kukushawishi na sipo hapa kwa ajili hiyo,nipo hapa kwa ajili ya kufikisha na wenye haki na wa kweli muwajue na ukweli wenyewe muujue.Kama hinielewi endelea kua mtumwa wao daima ila Mimi hunishawishi kama mtu mweusi wa huku nyumbanitu!
Safi kabisa,sasa tuambie huu ulimwengu na sisi binadamu imekuwaje tukawa hivi tulivyo,je tumejiumba wenyewe au tumetokea pasi na chochote ? Hili swali huwa unalikimbia.Kwanza kabisa, kitu kuwa na mtengenezaji wake si lazima mtengenezaji wake awe Mungu.
Omyesha ukichaa wake uko wapi ?Pili, dhana nzima ya kusema Mungu asiyeonekana yupo, kwa sababu kika kinachoonekana kina mtengenezajinwake ni kichaa cha aina fulani.
Vipo visivyo onekana ila vinauashiria wake kwa vinavyo onekana kuonyesha uwepo wake. Akili huioni wewe ila mwenye akili unamuona na asiyekuwa na akili unamuona kadhalika. Yaani Allah haonekani Ulimwenguni ila kuna muda tutamuona kama vile tunavyo jua la utosi,lakini kwa kuwa kwa sasa haonekani ila kuna ishara zinaonyesha uwepo wake akili,mazingira,ufunuo na mfano wa hivi huonyesha uwepo wake.Yani ni bora ungesema habari ya vitu vinavyoonekana kuhalalisha uwepo wa Mungu anayeonekana.
Kadhalika visivyo onekana vinamtengenezaji wake na yeye ni Allah mtukufu na akasema yeye ndiyo mjuzi wa yale ya dhahiri na yale yaliyofichikana.Zaidi, kudai kila kitu kinachoonekana kinq mtengenezaji wake, hujaongelea visivyoonekana.
Quantum Physics ni nadharia tu ambazo hata wakubwa zako hawakuweza kuzithibitisha.Na unaonesha hujasoma Quantum Physics ambayo inavunja cause and effect.
Hivi ushawahi kufundishwa somo la ukosoaji maana hapa hujagusa hata kile alichokiandika uliye "mquote" mwisho wake una dai kwamba umeonyesha ujinga wake ? Kwenye nini mantiki au falsafa au hiyo Quantum Physics ?Umeonesha ujinga wako.
Umezitoa halafu huwezi kuzitetea unakimbia kimbia mwisho unakuja kuleta tarjama ya Qur'aan ya Yusuf Ali kwa ujinga wako una dai kuwa ndiyo Tafsiri ya Qur'aan,kisha ukaweka kitabu cha historia sasa sijui kinajibu nini katika Tafsiri ya Qur'aan kwa dhati ya aya,kadhalika huenda hata vile vitabu ulivyo weka sura yake ya nje hukuvisoma,sidhani kama ungevisoma ungeleta hizo unazo dai kuwa ni Cotradictions.Hizi ni za kumpa officialboy , zinaweza kumsaidia.Mimi nishazitoa sana hapa.
Za kutoka Quran na Biblia, hata wiki hii nimeziweka hapa.
Ukristo lini uliwahi kuwepo kabla ya Uislamu labda kabla ya Uislamu huu aliokuja nao Mtume wetu ila kwa Uislamu wa ujumla hakuna mtume ambaye hakuwa Muislamu,welaketofautiana sheria tu ila imani yao wote ni moja.Najua na nimefanya makusudi. Kwanini iwezekane kila mtoto akizaliwa awe ni muislam ila baadaye abadilishwe na dunia? Kama ukristo ulikuwapo kabla ya uislam na Yesu alikuja kuwakomboa wanadamu wote,kwanini na Muhamad asiwe miongoni mwao. Sijui kama utaelewa mantiki ya niandikayo.
MkuuMkuu, umeongea kitu muhimu sana.
Watu wengi matendo yao hayaoneshi kwamba wanaamini Mungu, na ironically, mara nyingine sisi tusioamini Mungu ndio tunaotenda matendo yanayoendana na imani za kuamini Mungu.
Nitakupa mfano mmoja mdogo tu.
Nilikuwa katika kundi moja, mtu mmoja akawa analalamika anaumwa katika hilo kundi.
Wale watu wa kwenye hilo kundi wote wanajinasibu na imani ya Mungu.Kila mmoja akawa anasema "tutakuweka kwenye maombi", na "Mungu atakusaidia".
Mimi siamini katika maombi wala Mungu kumsaidia mtu mwenye matatizo, kwa sababu siamini Mungu yupo. Nakwenda kwa falsafa za kwamba, matatizo ya mtu yatamalizwa na mtu, maombi ni kujiliwaza tu na Mungu hayupo.
Nikaguswa sana na kilio cha yule mtu, ni dada wote tunamjua, hana uwezo, na pale kwenye kikundi kuna watu wana uwezo wa kumsaidia wanajibalaguza kumuombea kwa Mungu.
Mimi nikatembeza muamala chapchap yule dada asaidiwe, nikamtumia rafiki yetu mwingine alikuwa Dar alikuwa na wasaa wa kuweza ku organize mgonjwa apelekwe hospitali.
Kuna rafiki yetu mwingine daktari aka arrange hospitali yule dada apokewe.
Ndani ya muda mfupi ule muamala wangu ukawa umeshawezesha yule mgonjwa akatiwe bima, aanze matibabu.
Huku wengine waliojikita kumuombea mgonjwa kwa Mungu wakawa kama wameona aibu, ukatembea mchango kusaidia mgonjwa.
To make a long story short, wale watu wanaoamini Mungu waliofundishwa usamaria mwema na kusaidia watu wenye matatizo wote walikuwa wanaangaliana wakati mwenzao, rafiki yao waliyemjua kwa miaka mingi anakaribia kufa. Na ninaposema anakaribia kufa si utani.Yule rafiki yetu daktari alikuja kutuambia kwamba pale tungechelewa kidogo tu habari ingekuwa tofauti sana.
Nikatokea gubegube tu hata siamini Mungu yupo, lakini kwa sababu siamini Mungu yupo hilo ndilo limenipa wajibu mimi kufanya kazi ya kusaidia mwenyewe bila kumsukumizia mzigo huo Mungu, kwa sababu najua Mungu hayupo. Nikaanzisha msaada chapchap.
Sasa hapo utaona wasioamini Mungu wanafanya usamaria mwema kirahisi kama vile wanaamini Mungu, wanaoamini Mungu wameendekeza ubinafsi.
Hii dunia kama watu wangekuwa kweli wanaamini Mungu yupo kama wanavyodai, maovu mengi sana yangetoweka.
Watu wanaiba mpaka misikitini. Waziri Mkuu katudanganya msikitini kwamba rais mzima anapiga kazi.
Halafu utaambiwa huyo naye anaamini Mungu.
Ni kweli anaamini Mungu?
Bora hata mimi nimesema siamini Mungu na sijadanganya msikitini kama yeye!
Atheism ni lack of beliefsSi kweli.
Kwahiyo unataka kutuambia kutokujua na kukataa uwepo wa mungu hivi viko sawa ns ndiyo "Atheism" hii ?
Sasa kama hata kutofautisha kati ya kutokujua na kukana unashindwa inakuwaje una mkana Mungu ?
Hivi unaelewa maana ya contradiction ?Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani hakuna contradiction.
Kwa sababu.
Mabaya kutowezekana si contradiction kwa Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Mabaya kuwezekana ndiyo contradiction.
Umeelewa hilo somo?
Kiranga hawachelewi kukuambia wewe ndio msaada uliyeletwa na Mungu baada ya maombi yao.. [emoji38][emoji38]
Religious people huwa wajinga sana
Amin amin nawaambiaKama ulikuwepo vile, kuna cousin wangu mmoja huyo ukimsaidia anasema "Bwana amekutumia".