Safi kabisa,sasa tuambie huu ulimwengu na sisi binadamu imekuwaje tukawa hivi tulivyo,je tumejiumba wenyewe au tumetokea pasi na chochote ? Hili swali huwa unalikimbia.
Embu tupe uwezekano au tuonyeshe kwamba Mola si muhusika wa huu ulikwengu na utuonyeshe uwezekano wa uwepo wa kitu pasi na msanifu wake,mwenye kujua,mwenye maarifa na mfano wake.
Omyesha ukichaa wake uko wapi ?
Kadhalika mpaka visivyo onekana vinamtengenezaji wake. Roho,njaa,maumivu,majonzi na mfano wake vyote vinatoka kwa Allah.
Vipo visivyo onekana ila vinauashiria wake kwa vinavyo onekana kuonyesha uwepo wake. Akili huioni wewe ila mwenye akili unamuona na asiyekuwa na akili unamuona kadhalika. Yaani Allah haonekani Ulimwenguni ila kuna muda tutamuona kama vile tunavyo jua la utosi,lakini kwa kuwa kwa sasa haonekani ila kuna ishara zinaonyesha uwepo wake akili,mazingira,ufunuo na mfano wa hivi huonyesha uwepo wake.
Kwahiyo kufikiri kwa aina hiyo unavyofikiri wewe ufinyu wake ni kama umefungiwa ndani ya chumba kidogo chenye kidirisha kidogo,kisha ukatazama nje ukahitimisha juu ya kile ulichokiona ndiyo kitu kizima wakati uhalisia ni kitu kidogo sana kwenye kile kitu kizima.
Kadhalika visivyo onekana vinamtengenezaji wake na yeye ni Allah mtukufu na akasema yeye ndiyo mjuzi wa yale ya dhahiri na yale yaliyofichikana.
Quantum Physics ni nadharia tu ambazo hata wakubwa zako hawakuweza kuzithibitisha.
Hakuna kinacho vunja "cause" and "effect" wakati kuna msanifu na kuna malighafi na kuna kile kinachotarajiwa. Labda nikupe kazi utuonyeshe kwa namna gani (hili najua huwezi kuonyesha ila naonyesha ujinga wako ulipo mili) Quantum Physics ina vunja "cause" na "effect" katika uwepo wa kiti mathalani, kilichotengenezwa kwa malighafi ya mbao (Material cause), msanifu (first cause) na kiti(effect) chenyewe. Kwahiyo kwa vyovyote vile Quantum Physics haiwezi kubatilisha (disprove) Causality.
Hivi ushawahi kufundishwa somo la ukosoaji maana hapa hujagusa hata kile alichokiandika uliye "mquote" mwisho wake una dai kwamba umeonyesha ujinga wake ? Kwenye nini mantiki au falsafa au hiyo Quantum Physics ?