Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

[emoji3][emoji3][emoji3]sawa kiranga mwingine
Ukiwaangalia kwa makini watu hao wana ugonjwa wa akili.

Wewe muulize tu swali rahisi,kama ana amini George Washington aliwahi kuwepo hapa duniani,kipi kimemfanya aamini je kuna mtu yeyote anasimulia katika mapokezi aliyemuona George Washington tena amesimulia kwa kuanza na tamko hili "Nilimuona George Washington akisema kadha wa kadha..".

Ukitaka kujua namna gani walivyo wajinga watu hawa,waulize swali halafu komaa nao mpaka wajibu,sababu wanakwepa sana maswali hii nahisi washajua madhaifu yao. Sasa akianza kujibu ndiyo utafurahi,juzi hapa nilikuwa najadiliana na Kiranga sehemu,nikambana ajibu maswali yangu akawa ana dai amejibu,mwisho wa siku akakiri hajajibu sasa alivyo anza kujibu ilikuwa kizaa yaani vituko,analeta vitabu kama ushahid ambavyo havihusiani na kadhia husika. Hakurudi tena. Hawa wabaneni katika kujibu maswali ni weupe mno.
 
Nimesoma na nimejua kua chanzo si muhimu

Au nimekuelewa vibaya ulimaanisha chanzo ni muhimu?
Si kweli utakuwa umesoma kwingine sababu nimekuonyesha ulazima wa Mola kutokuwa na chanzo na nimekuuliza swali hujajibu.
 
Yeye amedai kwamba mmeshindwa kuthibitisha kuwa Mungu hayupo,, kwa maana hiyo yawezekana mmeleta hoja ambazo sio za ukweli.
Na ndio maana nikamuuliza kua ni hoja gani ambazo wewe ukiletewa zitakushawishi kujua kua mungu hayupo. Au ni mbinu gani zinazotumika kuthibitisha visivyopo havipo?
 
Ushahidi gani ambao ulitarajia sisi tungekuwepo nao ambao ungekushawishi wewe kua tumeweza kuthibitisha Mungu hayupo?
Siyo lazima unishawishi sababu hata uongo unashawishi na kumfanya mtu akaamini uongo kwamba ni kweli. Wewe andika yaliyo ya kweli basi.

Maana yake unaposema Mola hayupo ni kwamba unajua hayupo na unao ushahidi wa kuonyesha kwamba hayupo.
Au nimekuelewa vibaya ulimaanisha chanzo ni muhimu?
Ili ujue umenielewa vibaya au la,jibu swali nililo kuuliza.
 
Kutokuwepo kwa imani, sio kuwepo kwa imani
Unaamini kama Mola hayupo au kama Mola hayupo ?

Kutokuwepo kwa imani ni kuamini juu ya kutokuwepo kwa imani.
ko ya pili kua "ipo" itakua na contradiction
Hakuna contradictions sababu kauli uangu ya pili ina ithibati juu ya kinyume chake.
 
Unaweza kuthibitisha miungu mingine inayoabudiwa na dini zingine zilizo kinyume na Mungu wako kua haipo?
Naweza na hili ni rahisi,sababu naenda kufukua misingi ya Miungu hiyo. Mathalani wapo Wakristo wanao amini katika Mungu mmoja na Yesu ni mwana wa Mungu na wale wanao amini Yesu ni mungu,hawa wote wamekufuru na kosa lao lipo katika kubadilisha mafundisho ya nabii Yesu. Hawa tunasema wamekufuru ila wanakubali katika uwepo wa Mola. Tukija katika wale ambao wanaabudu ng'ombe,maana yake anayeombwa msaada ni mwenye uwezo na mkamilifu kwa yale ambayo mwanadamu hayawezi kuyafanya na mnyama pia. Sasa unapochonga sanamu wewe mwenyewe kisha ukaliomba huu ni wendazimu sababu hilo kuwepo kwake limetegemea kwako. Au ng'ombe,ng'ombe ambaye usipo mpa chakula anakufa wewe unamuomba msaada,huu ni uhayawani. Kwahiyo usahihi unarudi katika asili.
 
Hio haikupi nafasi utegemee majibu yake kwanza... Wewe kama mpingaji wa uwepo wa Mungu inabid uwe na hoja zako za ukweli,, ukishindwa kuzitetea hio haikupi nafasi ya kutegemea hoja zake...
Vinginevyo kutakuwa na walakini katika logic mnayotumia.
Hoja za ukweli hazitegemei kwa namna ambayo yeye anazikubali au lah

Kwa hiyo mtu ukimuambia kua 1+2=3 halafu yeye akasema hakubalisni na jibu je hoja hiyo ya kusema 1+2=3 itakus ya uwongo kwasababu fulani amesema ni uwongo?

Kwanini swala la huyo mtu kusema hoja fulani ni ya uwongo kusihusishwe na ufinyu wake wa kulielewa jibu?

Zaidi utajikuta unaingia kwenye uwanja wa kutoa uthibitisho kwanini huo uthibitisho uliopewa sio uthibitisho na ni kitu ambacho najua huwezi kuthibitisha
 
Si kweli utakuwa umesoma kwingine sababu nimekuonyesha ulazima wa Mola kutokuwa na chanzo na nimekuuliza swali hujajibu.
Mola si anaingia katika list ya vilivyopo?

Sasa unanikanushaje kua hoja yangu kusema chanzo si lazima kwa vilivyopo haipo clear wakati kuna kitu umedai kipo?
 
Naweza na hili ni rahisi,sababu naenda kufukua misingi ya Miungu hiyo. Mathalani wapo Wakristo wanao amini katika Mungu mmoja na Yesu ni mwana wa Mungu na wale wanao amini Yesu ni mungu,hawa wote wamekufuru
Sasa hapa ndo umethibitisha mungu hayupo?

Au ndo ulikua unaanza?
 
Tukija katika wale ambao wanaabudu ng'ombe,maana yake anayeombwa msaada ni mwenye uwezo na mkamilifu kwa yale ambayo mwanadamu hayawezi kuyafanya na mnyama pia. Sasa unapochonga sanamu wewe mwenyewe kisha ukaliomba huu ni wendazimu sababu hilo kuwepo kwake limetegemea kwako. Au ng'ombe,ng'ombe ambaye usipo mpa chakula anakufa wewe unamuomba msaada,huu ni uhayawani. Kwahiyo usahihi unarudi katika asili.
Hivi unaelewa hujathibitisha mungu wa dini hizo kua hawapo bali umekanusha kwa kuonesha sio wa kweli kwa kulinganisha na madai ya dini yako? (na ni kazi ambayo mimi sijakutuma uifanye)

Though hiyo miungu nayo kwa mujibu wake ina principle zake ambazo zinabidi zifatwe ili uweze kujua ukweli. Hujaonesha kutumia hizo principle kujua ukweli, umetumia principle za dini yako kutafuta ukweli kwa dini zingine (huku ukielewa kua haiwezekani)

Kumbuka nimekutaka uthibitishe miungu tofauti na wako haipo
 
Kwanini unashindwa kutetea hzo hoja kama ni za ukweli...

Vp kama amezikataa kwa kukupa hoja thabiti ?

Inatakiwa na ww uendelee kuitetea hio hoja yako,, ukishindwa kuitetea, hio itamaanisha nn ?
Kwani ili mtu aonekane kaweza kutetea hoja zake ni lazima oppoent akubali kua hoja hizo ni za kweli?

We unataka nizitetee kwa namna gani ambayo itakushawishi ukakubaliana nazo?

Na unajuaje kua hoja hiyo ni thabiti na sio kibwagizo tu

Mathalani mtu ambaye kapinga 1+2=3 atahitaji hoja gani thabiti kuonesha kua 1+2 sio sawasawa na 3?
 
Mola si anaingia katika list ya vilivyopo?

Sasa unanikanushaje kua hoja yangu kusema chanzo si lazima kwa vilivyopo haipo clear wakati kuna kitu umedai kipo?
Ndiyo maana nilikwambia usome na ujibu nilicho kuuliza,nilijuonyesha kutowezekana na Mola kuwa na chanzo,na nikakuuliza swali uonyeshe kutokuwa na ulazima wa chanzo hasa katika ulimwengu tulio nao,hili hujalifanya.
 
Sasa hapa ndo umethibitisha mungu hayupo?

Au ndo ulikua unaanza?
Hiyo nimekuonyesha ya kuwa hilo nawezana tunarudi kwenye asili,sababu ukivunja msingi ndiyo umeangusha jengo.

Lakini ulitakiwa uainishe ya kuwa unazungumzia ng'ombe au ?Ng'ombe yupo ila naongelea ubatili wa ng'ombe kufanywa mungu.
 
Sababu amekupa uwezo wa kuyaepuka na hiyo si kazi tena.
Kwa maana hiyo mabaya sio mambo mema mpaka niyaepuke?

Kama jibu litasema "ndio" utabidi ujibu kwani aumbe visivyo mema ilihali yeye ni mungu msafi?

Kama jibu liasema "Hapana" itabidi ueleze kwanini aliumba
 
Hivi unaelewa hujathibitisha mungu wa dini hizo kua hawapo bali umekanusha kwa kuonesha sio wa kweli kwa kulinganisha na madai ya dini yako? (na ni kazi ambayo mimi sijakutuma uifanye)

Though hiyo miungu nayo kwa mujibu wake ina principle zake ambazo zinabidi zifatwe ili uweze kujua ukweli. Hujaonesha kutumia hizo principle kujua ukweli, umetumia principle za dini yako kutafuta ukweli kwa dini zingine (huku ukielewa kua haiwezekani)

Kumbuka nimekutaka uthibitishe miungu tofauti na wako haipo
Mungu tofauti ipo ila naongelea kuwafanywa kuwa miungu ndiyo tatizo.

Kwa mfano mungu ng'ombe principle anazitoa ng'ombe au ng'ombe anawekewa sheria na mwenye ng'ombe ?
 
Kwa maana hiyo mabaya sio mambo mema mpaka niyaepuke?
Uwe unasoma ulicho kiandika. Sijakuelewa.

Kama jibu litasema "ndio" utabidi ujibu kwani aumbe visivyo mema ilihali yeye ni mungu msafi?

Kama jibu liasema "Hapana" itabidi ueleze kwanini aliumba
Ndiyo maana tunasema Mola ni mjuzi wa yote.

Ameumba maovu na ameyaruhusu yatokee ili aone wale watakao shukuru au kukufuru.
 
Una akili ndogo sana,mabaya yana athari hasi ndiyo maana lazima yaepukwe. Kitu kinacho dhuru wewe kiakili au kimaana au kihisia,hicho ni kibaya kwako vipi huwa unakiepuka au unazembea ? Unauliza maswali ya kitoto sana.
Kama yana athari mbaya maana yake hayakutakiwa kuwa sehemu ya viumbe vyake.

Ushawahi kuhoji masheikh wako kwanini mabaya hayo yeye hayamfiki, tutakua na imani gani kua hawezi kua mtu mbaya endapo ataishi katika mazingira haya ilihali kazuia mabaya yasiweze kumpata?

Ushawahi kujiuliza wewe ungepata power ya kuzuia mabaya ungewezaje kuwa mbaya au kufanya mabaya?

Bila shaka utagundua kua kupitia vitabu vyenu yeye huyo mungu alikuumba ukiwa na weakness yakukaribiwa na mabaya, weakness ya kuweza kuyafanya mabaya, weaknesss ya kuwa mbaya. Na ndio masema hakuna binadamu mkalifu maana yake hiyi ni imperfection

Sasa mungu anategemeaje kutokuona makosa katika kazi yake aliyoiwekea ubovu?
 
Vp kama opponent akikupinga kwa hoja zenye mantiki kisha ww ushashindwa kuzitetea ? Hizo hoja zako zitakuwa za kweli ?

Hilo swali unaniuliza mm tena ? Ina maana hujui jinsi ya kutetea hoja zako na kumshawishi mtu kukubaliana nazo... Sasa kuna haja gani ya kujadiliana ?
Nipe hoja ya kimantiki inayoonesha 1+1 jibu sio 2
 
Ukiwaangalia kwa makini watu hao wana ugonjwa wa akili.

Wewe muulize tu swali rahisi,kama ana amini George Washington aliwahi kuwepo hapa duniani,kipi kimemfanya aamini je kuna mtu yeyote anasimulia katika mapokezi aliyemuona George Washington tena amesimulia kwa kuanza na tamko hili "Nilimuona George Washington akisema kadha wa kadha..".

Ukitaka kujua namna gani walivyo wajinga watu hawa,waulize swali halafu komaa nao mpaka wajibu,sababu wanakwepa sana maswali hii nahisi washajua madhaifu yao. Sasa akianza kujibu ndiyo utafurahi,juzi hapa nilikuwa najadiliana na Kiranga sehemu,nikambana ajibu maswali yangu akawa ana dai amejibu,mwisho wa siku akakiri hajajibu sasa alivyo anza kujibu ilikuwa kizaa yaani vituko,analeta vitabu kama ushahid ambavyo havihusiani na kadhia husika. Hakurudi tena. Hawa wabaneni katika kujibu maswali ni weupe mno.

Cheki ulivyo na confidence, kama vile unajua unayosemaa,
Ivi unajua sifa mojawapo ya mjinga.... Mjinga huwa anaamini sana yale aliyojifunza na inakuwa ngumu kwake kubadilika kutokana na maarifa mapya yanayokinzana na ujuzi wake wq awali.

Socrates alisemwa na oracle hio kale ya ugiriki kama mtu aliye na busara kuliko wote. Jee unajua sentensi inayojumuisha mafunzo yake yote inasemaje...
Inasema hivi " ninachojua kwa uhakika ni kwamba sijui kitu"

Na je unajua ugonjwa wa akili upo vipi sifa za wenye ugonjwa wa akili unazifahamu? Nafahamu chache kama kusikia sauti kichwani, kuona vitu ambavyo havipo, na kuwa na mashaka kama kuna kitu kinakwangalia matendo yako na kina kalamu kinaorodhesha, tena mpaka hata chooni bado tu kinakufatilia nyendo hata mawazo kinahesabia,

Kuhusu proof ngoja nikupe somo kidogo tuu
Jambo linakuwa linathibitishwa pale zaidi ya ushahidi moja unapotolewa
Mfano
Geogre washington ameacha shahidi nyingi sana kuna barua alizoandika, kuna kaburi, kuna story za watu waliokutana,kuna evidence ya vita aliyopigana,

Na pia unaongea watu kukimbia maswali huna lolote watalamu wa psychology wanajua tuu hio ni self defence yaani unapakazia wengine madhaifu ambayo unayo

Nikuulize swali je ni kitabu gani cha mkusanyiko wa waandishi ambao hao waandishi sio wao walioandika hicho kitabu?
 
Back
Top Bottom