nayosemaa,
Ivi unajua sifa mojawapo ya mjinga.... Mjinga huwa anaamini sana yale aliyojifunza na inakuwa ngumu kwake kubadilika kutokana na maarifa mapya yanayokinzana na ujuzi wake wq awali.
Hii si maana ya mjinga,mjinga ni yule asiyejua jambo fulani.
Maana uliyo itoa ni maana ya mpumbavu. Yaani yule anaye jiona anajua na hajui na hajijui kama yeye hajui.
Rekehisha kiti chako kwanza kisha ukipambe.
Socrates alisemwa na oracle hio kale ya ugiriki kama mtu aliye na busara kuliko wote. Jee unajua sentensi inayojumuisha mafunzo yake yote inasemaje...
Inasema hivi " ninachojua kwa uhakika ni kwamba sijui kitu"
Alikuwa sahihi katika hili na kweli alikuwa hajui. Kujua kama wewe hujui ni hatua na wewe ni mwerevu,tena kusema hujui kwa kile ambacho hukijui ni nusu ya elimu.
Na je unajua ugonjwa wa akili upo vipi sifa za wenye ugonjwa wa akili unazifahamu? Nafahamu chache kama kusikia sauti kichwani, kuona vitu ambavyo havipo, na kuwa na mashaka kama kuna kitu kinakwangalia matendo yako na kina kalamu kinaorodhesha, tena mpaka hata chooni bado tu kinakufatilia nyendo hata mawazo kinahesabia,
Kuna namna kadhaa za kutoa maana ya jambo,hapa nagusia namna ya kuarifisha tamko kwa mfano. Nasema mimi,Wakana mungu ni wagonjwa wa akili,sasa ukitaka kumjua mgonjwa wa akili katika aina za ugonjwa wa akili basi watazame wakana mungu.
Sifa nazijua,kuna ugonjwa wa akili na kuna wasi wasi.
Kuhusu proof ngoja nikupe somo kidogo tuu
Jambo linakuwa linathibitishwa pale zaidi ya ushahidi moja unapotolewa
Mfano
Geogre washington ameacha shahidi nyingi sana kuna barua alizoandika, kuna kaburi, kuna story za watu waliokutana,kuna evidence ya vita aliyopigana,
Huu siyo ushahidi wa kuonyesha yeye alikuwepo,tukienda katika misingi ya uhakiki wa habari. Sifa ya masimulizi yawe ya kweli lazima kuwe na mpokezi wa habari hiyo tena awe amemuona au huyo amepewa habari na yule aliyemuona. Kuhusu machapisho hichi si kigezo mpaka ubainike ukweli juu ya wale wali mdiriki tena wawe na sifa ya ukweli.
Story za watu walio kutana naye zimesimuliwa na nani na tunazipata wapi ?
Unao ushahidi kuonyesha ya kuwa hizo barua ameandika yeye ?
Na pia unaongea watu kukimbia maswali huna lolote watalamu wa psychology wanajua tuu hio ni self defence yaani unapakazia wengine madhaifu ambayo unayo
Kwanza suala la wao kukimbia maswali labda wewe umeamua kupoteza muda kwa kuandika uongo.
Pili,suala la wao kukimbia maswali hilo silisemi mimi bali wengi katika wanao jadiliana nao huwa wanasema watu hawa wanakimbia maswali,lakini siyo kwamba wanakimbia kwa kupenda,sababu hawana elimu na hawana cha kutoa,asiyenacho atatoa nini ? Sasa huwezi bishana na ukweli zaidi ya kuumia na kupoteza muda.
Kama una hoja jenga hoja na ujibu maswali yanayo ulizwa humu.
Nikuulize swali je ni kitabu gani cha mkusanyiko wa waandishi ambao hao waandishi sio wao walioandika hicho kitabu?
The History of Andalusia.