Kiranga alikuwa anasali Kanisa Katoliki. Ilikuwaje akaanza kuamini hakuna Mungu?

Inamaana wewe haujui hivyo vitu vimetokeaje? (formation) kwanini unashindwa kunipa jibu.
Unatunga swali bovu halafu bila aibu unalazimisha watu walalie hukohuko kwenye ubovu wako ambao umetokana na ufahamu wako kuwa duni,

Thibitisha kwanza kwamba hivyo vitu vina formation.

Hatutaki hadithi za limited to time kwa kuwa time yenyewe kuna wakati inakuwa haipo,yaani haiko constant kila mahala.
 
Kama majibu unayo niambie mkuu kwanini unazunguka

Wewe ukiniambia bahari imesababishwa na miamba, bila kuniambia kwanza miamba imetokea wapi na imesababisha vipi bahari unanipa wasiwasi. Miamba imetokea tu gafla?
Tuko katika mjadala ambao tunajadili kwa kiswahili

Katikati ya mjadala ukauliza swali kwa sharti kwamba lijibiwe kichina

Nakupatia jibu kwa lugha ya kichina unakuja kuonesha tena kuwa kumbe hicho kichina ulichopendekeza jibu lijibiwe nacho hukijui

Sasa unanipa kazi ya ziada na kunitoa kwenye mjadala mkuu, nikufundishe kichina ukijue halafu tena nije nikufundishe namna ya kulielewa jibu la swali ulilouliza

Watu wanajiuliza...kulikua na ulazima gani wa wewe kuhitaji majibu ya swali lako yawe katika lugha ya kichina ilihali kichina hukijui?? Wewe unakazania tu kusema "nipe jibu"

Kuna haja gani ku-demand majibu ya kisayansi ilihali huijui hata basic ya sayansi yenyewe?
 
Hadi muda huu hakuna mshindi.
Hivyo basi....kila mmoja abaki na anacho kiamini.
UZI UMEFUNGWA
 
Mkuu, umeongea kitu muhimu sana.

Watu wengi matendo yao hayaoneshi kwamba wanaamini Mungu, na ironically, mara nyingine sisi tusioamini Mungu ndio tunaotenda matendo yanayoendana na imani za kuamini Mungu.

Nitakupa mfano mmoja mdogo tu.

Nilikuwa katika kundi moja, mtu mmoja akawa analalamika anaumwa katika hilo kundi.

Wale watu wa kwenye hilo kundi wote wanajinasibu na imani ya Mungu.Kila mmoja akawa anasema "tutakuweka kwenye maombi", na "Mungu atakusaidia".

Mimi siamini katika maombi wala Mungu kumsaidia mtu mwenye matatizo, kwa sababu siamini Mungu yupo. Nakwenda kwa falsafa za kwamba, matatizo ya mtu yatamalizwa na mtu, maombi ni kujiliwaza tu na Mungu hayupo.

Nikaguswa sana na kilio cha yule mtu, ni dada wote tunamjua, hana uwezo, na pale kwenye kikundi kuna watu wana uwezo wa kumsaidia wanajibalaguza kumuombea kwa Mungu.

Mimi nikatembeza muamala chapchap yule dada asaidiwe, nikamtumia rafiki yetu mwingine alikuwa Dar alikuwa na wasaa wa kuweza ku organize mgonjwa apelekwe hospitali.

Kuna rafiki yetu mwingine daktari aka arrange hospitali yule dada apokewe.

Ndani ya muda mfupi ule muamala wangu ukawa umeshawezesha yule mgonjwa akatiwe bima, aanze matibabu.

Huku wengine waliojikita kumuombea mgonjwa kwa Mungu wakawa kama wameona aibu, ukatembea mchango kusaidia mgonjwa.

To make a long story short, wale watu wanaoamini Mungu waliofundishwa usamaria mwema na kusaidia watu wenye matatizo wote walikuwa wanaangaliana wakati mwenzao, rafiki yao waliyemjua kwa miaka mingi anakaribia kufa. Na ninaposema anakaribia kufa si utani.Yule rafiki yetu daktari alikuja kutuambia kwamba pale tungechelewa kidogo tu habari ingekuwa tofauti sana.

Nikatokea gubegube tu hata siamini Mungu yupo, lakini kwa sababu siamini Mungu yupo hilo ndilo limenipa wajibu mimi kufanya kazi ya kusaidia mwenyewe bila kumsukumizia mzigo huo Mungu, kwa sababu najua Mungu hayupo. Nikaanzisha msaada chapchap.

Sasa hapo utaona wasioamini Mungu wanafanya usamaria mwema kirahisi kama vile wanaamini Mungu, wanaoamini Mungu wameendekeza ubinafsi.

Hii dunia kama watu wangekuwa kweli wanaamini Mungu yupo kama wanavyodai, maovu mengi sana yangetoweka.

Watu wanaiba mpaka misikitini. Waziri Mkuu katudanganya msikitini kwamba rais mzima anapiga kazi.

Halafu utaambiwa huyo naye anaamini Mungu.

Ni kweli anaamini Mungu?

Bora hata mimi nimesema siamini Mungu na sijadanganya msikitini kama yeye!
Ila chief una logic aisee, mind yako sio ya mchezo kabisa kuna elimu mtu unapata kupitia maandiko tu hapa vipi kama akipata walau saa moja la kuzungumza ana kwa ana? Hongera sana
 
Unatunga swali bovu halafu bila aibu unalazimisha watu walalie hukohuko kwenye ubovu wako ambao umetokana na ufahamu wako kuwa duni,

Thibitisha kwanza kwamba hivyo vitu vina formation.

Hatutaki hadithi za limited to time kwa kuwa time yenyewe kuna wakati inakuwa haipo,yaani haiko constant kila mahala.
Kuuliza hivyo vitu vimetokeaje tokeaje ni swali bovu? Una conclude vipi ni swali bovu ikiwa bado nahitaji kujua hivyo vitu vimetokeaje kwa uthibitisho unaothibitishika kisayansi. Kama majibu unayajua nijibu.
 
Tuko katika mjadala ambao tunajadili kwa kiswahili

Katikati ya mjadala ukauliza swali kwa sharti kwamba lijibiwe kichina

Nakupatia jibu kwa lugha ya kichina unakuja kuonesha tena kuwa kumbe hicho kichina ulichopendekeza jibu lijibiwe nacho hukijui

Sasa unanipa kazi ya ziada na kunitoa kwenye mjadala mkuu, nikufundishe kichina ukijue halafu tena nije nikufundishe namna ya kulielewa jibu la swali ulilouliza

Watu wanajiuliza...kulikua na ulazima gani wa wewe kuhitaji majibu ya swali lako yawe katika lugha ya kichina ilihali kichina hukijui?? Wewe unakazania tu kusema "nipe jibu"

Kuna haja gani ku-demand majibu ya kisayansi ilihali huijui hata basic ya sayansi yenyewe?
Sawa, baada ya kusoma haya maelezo yako meengi. Sasa nahitaji kujua hivyo vitu vimetokeaje tokeaje (formation) zake
 
unamaanisha Nini ukisema formation?
Namaanisha vimetokeaje tokeaje hivyo vitu, how do they formed? Mfano ili juice ya parachichi iwepo ina formation yake.

Nikihitaji kujua juice ya parachichi imetokeaje, nitakuuliza formation yake.

Unaweza ukaniambia ime-form kutokana na ingredients zifuatazo:- tunda parachichi, maji na sukari. Na ikafanyiwa process ya kusagwa na kupatikana juice ya parachichi.

Sasa nitahitaji kujua kwanza hizo ingredients:- Tunda parachichi, maji na sukari vimetokea wapi kwanza?

Kwanini?
Kwasababu nahitaji kujua kwanza hizo ingredients zimetokea wapi? Hizo ingredients zimetokea tu gafla?

Nahitaji jibu ambalo lipo (Well scientifically proved) na sio jibu la kufikirika, kwamba juice ya parachichi imetokana na tunda parachichi, maji na sukari alafu ukaishia hapo bila kuniambia kwanza tunda parachichi, maji na sukari navyo vimetokea wapi?
 
Hakuna atheist yoyote anayeweza kukupa majibu ya chanzo sahihi cha uhai na viumbe visivyo hai. Wanarukaruka ila mwishowe hawana answers. Kazi yao kubwa ni kukana uwepo wa Mungu.

How did we get in this planet? Why are we here?

Ukiangalia dunia na vyote vilivyomo utagundua kuwa kila kitu kiko carefully planned...na viliandaliwa ili ku support life. Kwa nini uhai uwepo hapa tu na si sayari kama Mars au jupiter?

Ili viumbe viendelee kuishi vinahitaji nishati itokayo kwenye vyakula...na vyakula vipo. Maana yake whoever aliyekusudia kutengeneza vyakula ndiye aliyetu design pia ili tuvitumie.

Wajiulize tena kwa nini tunakunywa maji? Je imagine tungekuwa tunahisi kiu na maji hayapo duniani..ingekuwaje? Nani aliye tu design tutumie maji? Is it by mere chance au we were designed by a super intelligent being?

Ukikaa chini na kutafakari kwa kina upo ushahidi wa uwepo wa Mungu all around us. Mungu yupo.
 
ushahidi upi Sasa, thibitisha. Kuishia tu kusema "ukifikiria sana" hapana usifikirie sana thibitisha.
 
Kuuliza hivyo vitu vimetokeaje tokeaje ni swali bovu? Una conclude vipi ni swali bovu ikiwa bado nahitaji kujua hivyo vitu vimetokeaje kwa uthibitisho unaothibitishika kisayansi. Kama majibu unayajua nijibu.
Aliyekwambia vimetokea tokea nani? Kwa nini usimuulize huyo iwapo alikwambia vimetokea tokea?
 
Back
Top Bottom