Kiranga na jamaa zake wanaweza wasionekane kwenye thread mbalimbali lakini uzi wowote unaomsifia Mungu huwakosi

Kiranga na jamaa zake wanaweza wasionekane kwenye thread mbalimbali lakini uzi wowote unaomsifia Mungu huwakosi

Huwa najiuliza sana kwanini huyu Kiranga na wengine wengi huwa wanajitokeza kwenye uzi wowote ule unao muhusu Mungu na lengo ni kupinga uwepo wake.

Haijarishi hujamu mention dk1 ni nyingi hawa hapa.

Ni kwamba wakuu msipopita kimyamya tu mkatuacha sisi tunaokubali na kuamini uwepo wa Mungu tuendelee na mjadala huwa mnapungukiwa kitu?

Huyu Bush Dokta Kaja kwa kasi sana kwenye kupinga uwepo wa Mungu.Ninaomba mwe mnatuchie mjadala sisi tunao amini uwepo wa Mungu asee huwa mnatuvuruga sana maana mnajua wazi majibu hatuna hivi ni vitu vya Imani sasa imani utaithibitisha vipi? Ni sawa na kuambiwa nenda kaniletee upepo.

RAMADHAN KAREEM
According to Kiranga

Yupo sawa kwa sababu hili jukwaa ni huru ambalo kila mtu anachagua

Ku comment au ku react kwenye thread yoyote ambayo yeye anaona ana uelewa nayo au imemvutia kiufupi

Yupo sawa
 
Hili ni jukwaa huru Kila mmoja anao Uhuru wa kukubaliana ama kutokukubaliana na Jambo Fulani as long as hatukani mtu wala kumkosea heshima. Just ignore them kama unaona wanachoandika hakiendani na wewe
😄😄😄Though umeonyesha hawa watu wakikaza kukushawishi unaweza kushawishika
Watu wanaogopa kuacha dini zao mkuu?

Mimi siko hapa kumbadili mtu imani yake.

Mtu kuamini anavyotaka, au kutoamini anavyotaka, ni haki ya kikatiba na kibinadamu iliyoainishwa katika katiba na "Universal Declaration of Human Rights" tangu December 10 1948.

Hii ni sehemu ya "freedom of conscience".

Kwenye jambo la imani, ambalo kimsingi ni jambo la faragha, nitatetea watu kuwa na haki ya kuamini wanavyotaka, hata kama mimi si mtu wa imani.

Mimi sijadili imani ya mtu. Mimi naongelea falsafa, mantiki, uhakiki, uthibitisho, ushahidi.

Imani ina faragha yake, angalau ukiifanya kwenye faragha yake. Ukiileta hapa JF public square, umealika public scrutiny, inquiry, discussion, critique, mpaka ridicule.
 
Huwa najiuliza sana kwanini huyu @Kiranga na wengine wengi huwa wanajitokeza kwenye uzi wowote ule unao muhusu Mungu na lengo ni kupinga uwepo wake.
Kwenye nyuzi zangu alijitokeza tokeza, "nikampasua kwa moto na nyundo ivunjayo miamba vipande vipande huyo shetani aliye nyuma yake." Amechukia sana mpaka ameamua kuniweka kwenye ignore list 🙂. Namuombea Mungu amhurumie na kumuokoa. Tumsamehe tu bure, hajui alitendalo. Hata sisi kabla Yesu hajatuokoa, tulikuwa kama yeye.

Na wewe tumia nyundo hii:
Yeremia 23:29 BHN
Neno langu ni kama moto; ni kama nyundo ipasuayo miamba vipandevipande.
 
Kazi ya kupinga uwepo wa Mungu ni kazi endelevu.
Pole sana kwa kukubali kushirikiana na shetani. Kwa taarifa yako hiyo kazi unayoifanya ina mwisho. Usifikiri utaendelea kumpinga Mungu milele. Siku inakuja ya hukumu ambapo wote wasiomwamini Mungu watatupwa pamoja na shetani katika ziwa liwakalo moto na kiberiti. Tubu haraka kabla neema haijafungwa.
Ufunuo 21:8 SRUV
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
 
Huwa najiuliza sana kwanini huyu Kiranga na wengine wengi huwa wanajitokeza kwenye uzi wowote ule unao muhusu Mungu na lengo ni kupinga uwepo wake.

Haijarishi hujamu mention dk1 ni nyingi hawa hapa.

Ni kwamba wakuu msipopita kimyamya tu mkatuacha sisi tunaokubali na kuamini uwepo wa Mungu tuendelee na mjadala huwa mnapungukiwa kitu?

Huyu Bush Dokta Kaja kwa kasi sana kwenye kupinga uwepo wa Mungu.Ninaomba mwe mnatuchie mjadala sisi tunao amini uwepo wa Mungu asee huwa mnatuvuruga sana maana mnajua wazi majibu hatuna hivi ni vitu vya Imani sasa imani utaithibitisha vipi? Ni sawa na kuambiwa nenda kaniletee upepo.

RAMADHAN KAREEM
Popo mbili za vuka mto unazani hii kauli ni kweli shtuka
 
Kazi ya kupinga uwepo wa Mungu ni kazi endelevu.

Kila siku wanazaliwa watoto wapya wanapewa mafundisho ya uongo kwamba Mungu yupo.

Sasa tutaridhika vipi tukae kimya ikiwa uongo huu unafundishwa kila siku?

Ulishaona makanisa yanaridhika yanasema tusifundishe tena watu habari za uongo huu wa kuwapo Mungu?

Ulishaona misikiti inaridhika na kusema sasa tumeridhika kusema habari za uongo kwamba Mungu yupo?

Sasa kama hawa wasema uongo wa makanisani na misikitini na wengine wengi kama wao hawaridhiki kusema uongo, unapata wapi uhalali wa kutuambia sisi tunaonyoosha mambo na kuhoji uongo huo turidhike?

Jibu hoja, acha kushambulia watoa hoja.

Kushambulia mtoa hoja badala ya kujibu hoja ni logical fallacy.

Ni tabia ya watu wasio na hoja.

Ni ad hominem logical fallacy.

Unajua logical fallacy ni nini?
Kwa mtazamo wako,binadamu walitoka wapi mkuu?
 
Kwa mtazamo wako,binadamu walitoka wapi mkuu?
Kwanza kabisa hakuna binadamu. Unless one of your ancestors aliitwa Adam.

Neno "binadamu" lina mzizi wa ki etimolojia wa "bin Adam", kusema kwamba watu wote ni uzao wa Adam.

Huyo Adam hakuna ushahidi kwamba alikuwapo. Wasomi wa Biblia ya kiyahudi (Old Testament) wanasema huyo Adam hakuwapo, hiyo ni hadithi yabkuelezea mabadiliko ya jamii ya Kiyahudi tu.

Kasome kitabu cha Dr. James Kugel aliyefundisha masomo ya Biblia mpaka Harvard kinaitwa "How To Read The Bible : A Guide To Scripture Then And Now". Professor Kugel kaandika vizuri sana kuhusu habari hii.

Sasa, unless baba yako au ancestor wako mmoja anaitwa Adam, na wewe ni bin Adam kwa maana ya kwamba ni mtoto wa huyo baba/ babu anayeitwa Adam, jina "binadamu" ni misnomer.

Pili, kwa kujibu swali la "watu walitoka wapi", naweza kuwa sina jibu kamili la watu walitoka wapi lakini nikajua kuwa hawakuumbwa na Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.

Swali la watu walitoka wapi ni kubwa, ni gumu, linahitaji maelezo mengi, maelezo ya kitaalamu, utaalamu ambao pengine sina, na hata ule ambao ninao mwingi una controversy, na mimi sipendi kujadili masuala argumentative ambayo siwezi kuyatatua kwa truth table.

Hapa kuna ujinga mwingi, kuna wajinga wengi, watu hawajui evolution tu ni nini, na mimi sina haja wala appetite ya kutoka kwenye reli ya mada yangu ya msingi.

Mada yangu ya msingi ni hii.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Swali la watu walitoka wapi si langu. Kwa sababu sijawahi kudai kuwa najua watu walitoka wapi. Hili ni swali la kila mtu.

Swali langu ni hili.

"Unasema Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo, unahakikishaje Mungu huyo si chanzo cha maisha ya watu?".

Swali hili ndilo langu. Kwa sababu linauliza kuhusu Mungu ambaye mimi nimesema hayupo.

Kama unaniuliza swali hilo, niko tayari kukujibu.

Lakini swali la mtu kaanza vipi naweza kukutafutia vitabu vya wanazuoni tusome wote tuelezane hapa aya kwa aya. Sitaki kukupa jibu kwa sababu hata mimi mwenyewe najaribu kujifunza zaidi kuhusu swali hili.

Lakini, kabla ya kujua jibu sahihi najua jibu si Mungu.

Umenielewa?
 
Huwa najiuliza sana kwanini huyu Kiranga na wengine wengi huwa wanajitokeza kwenye uzi wowote ule unao muhusu Mungu na lengo ni kupinga uwepo wake.

Haijarishi hujamu mention dk1 ni nyingi hawa hapa.

Ni kwamba wakuu msipopita kimyamya tu mkatuacha sisi tunaokubali na kuamini uwepo wa Mungu tuendelee na mjadala huwa mnapungukiwa kitu?

Huyu Bush Dokta Kaja kwa kasi sana kwenye kupinga uwepo wa Mungu.Ninaomba mwe mnatuchie mjadala sisi tunao amini uwepo wa Mungu asee huwa mnatuvuruga sana maana mnajua wazi majibu hatuna hivi ni vitu vya Imani sasa imani utaithibitisha vipi? Ni sawa na kuambiwa nenda kaniletee upepo.

RAMADHAN KAREEM
Huu ni uchokozi wa wazi kwa uliowataja. Au unawaita kinamna?
 
Wewe hupendi wakionekana kwenye hizo nyuzi,,,,? Well kila mtu ana mtizamo na imani zake khs mambo flani flani ,,, ! Sio uhaini mimi kuamini kitu ambacho wewe haukiamini
Waambie wasisumbue watu masikini na vispika VYAO kusunbua watu.Kwani makanisa majengo hayawatoshi.
 
Wajulishe kuwa hata AI Chatgpt amesilimu.
Tupate wadhamini kidogo
 
Back
Top Bottom