Kisarawe: DC Petro Magoti ameutaka Msikiti unaotoa elimu ya dini kwa watoto 96, kuwarudisha walipowatoa sababu ya Mazingira Mabovu ya malazi

Watoto wa Kiislamu ni wengi kwenye baadhi ya mikoa kama Tanga, Pwani, na Zanzibar. Lakini kwa maeneo mengine mengi, wengi ni ama Wakristo au wapagani.

Shule ya Msingi niliyosoma kipindi chetu, katika darasa la wanafunzi 79, Waislamu wa kiume na kike walikuwa hawafiki 10.
 
Hii ni alarming kabisa, naipongeza serikal lakin jambo kama hili lisirudiwe kabisa
Huo ni utaratibu wa kawaida kabisa kwa wanafunzi wa dini wa Kiislam, labda tuseme waboreshewe mazingira ya kuishi.

Muelewe kuwa mpaka wazazi wao wameamua watoto zao wakafundishwe dini, hamfahamu ni mazingira yepi wanaishi walipotokea huko makwao. Utakuta wazazi ni duni, vishawishi vya kuwaingiza njia mbaya ni vingi ndiyo wazazi wakaamua wawapeleke wakaijuwe dini yao.

Hayo yapo miaka na miaka kwa Waislam.

Siyo huko tu, vyuo na misikiti mingi inapokea wanafunzi wa Qur'an namna hiyo.

Huyo Petro asilete mihemko yake, awasikilize kwa utuvu hao walimu, wanafunzi na wazazi wao, asikurupuke kwa sababu hawajuwi Waislam huyo.

Nashangaa hajasema "wanafundishwa ugaidi".
 
Kwani kituo kama kipo kisheria kinavunja sheria ipi?

Kinachotakiwa ifatwe sheria tu kama imekiukwa. Nyingine zote ni porojo tu.
 
Kuna wa historia halafu kuna sasa yaani "the now" hawa wa sasa ni changamoto....
 
Taifa linahitaji fikra huru sana ili watanzania wote wawe/tuwe salama na tuishi kama WATANZANIA nje ya hizi dini zetu.

Watanzania wengi TUNAKUWA wanafiki sana linapofika suala la hizi dini zetu na hata kuuweka UTANZANIA wetu pembeni bila kujali athari dhidi ya watanzania wenzetu.

Elimu ya msingi katika shule za Serikali Ina hali mbaya sana na elimu hii ndio husomwa na watanzania wengi saana huku wachache wakipeleka watoto kwenye hizi International, matokeo yake ni Taifa kubaki na wapumbavu wengi ambao mwisho wa siku wanakuwa exposed kwenye mambo ya hatari kwao naa hata kwa usalama wa Taifa.

Tuboreshe elimu ya msingi na maisha ya watu kila mahala, usawa uwepo kila mahala kila wakati tuache double standards.
 
Mohamed Said & Faiza Foxy njooni mlisemee hili.

Toeni matusi yote, lakn kuna agenda ya siri ndani ya hii miskitini kwa kivuli cha imani ya dini.

Muda utaongea. Pwani, Tanga, DSm ipo siku itafahamika.

Ongezea Tabora, Dodoma , Lindi Mtwara , Arusha
 

Elimu ya mtoto wako unaiweka rehani kwa mtu usiyemjua? Halafu kesho kushinda kuandika jinsi mfumo kristu unavyowapendelea wakristu?
Nina hakika, huyo shekhe hana analolijua. Anawalea na kuwafundisha watoto ubabaishaji tu. If the parent does not want to hold the responsibilities of their own families, who else can bother or care?
 
Huyo mwinyi wako wengine wanaona hakuwa kiongozi mzuri na ndiye aliyeua uchumi wa Tanzania. Anyways, hilo siyo hoja hapa. Hoja ni kujua wanafundishwa nini basi. Halafu mengine ndiyo yafuate.
Auwe uchumi wa Tanzania uchumi wenyewe wa kuuza ulikuwepo!?..hata pesa ya kulipa mishahara hazina haukuwepo,watoto walikua wakifundishwa dini
Huyo mwinyi wako wengine wanaona hakuwa kiongozi mzuri na ndiye aliyeua uchumi wa Tanzania. Anyways, hilo siyo hoja hapa. Hoja ni kujua wanafundishwa nini basi. Halafu mengine ndiyo yafuate.
 
Aliyekwambia kuna usiri ni nani? Nani alienda kuuliza kinachoendelea hakujibiwa? Wazazi hawana uwezo wa kupeleka watoto shule binafsi za sekondari mlitaka wafanye nini? Mtoto asijue dini yake kisa mzazi hana uwezo? Acheni chuki za kipumbavu nyie
 
Binafsi naungana na Mkuu wa wilaya. kituo kama hicho kinatakiwa kiwe kimetimiza matakwa yote ya sheria.

Waislam tunatakiwa tuwe Makhalifa na mfano bora kwa jamii, Waislam kama hao wanaoendesha hicho kituo ndiyo wanautukanisha Uislam.
 
Wanaweza kusafirishwa kimya kimya kupelekwa Somalia kwa njia za Majahazi usiku wa manane ili kwenda kupewa mafunzo ya Kigaidi halafu kurejeshwa kimya kimya.

Kana Yule wa Dodoma mberesero aliekamatwa Kenya chuo cha Garisa , Kwani imeshawahi kujulikana sligikaje pale kwenye uharifu mkubwa ule wa wasomali?
 
Shule za kawaida kusoma ni bure hadi form four, Kwanini hawasomi elimu ya kawaida?
Halafu mje kusema mfumo Kristo na blah blah ?
Pelekeni watoto Shule wasijekuwalaumu.
 
Hatari ya kisarawe ni nini? Huyo mkuu wa wilaya angekuwa na akili asingeweka udini kama wewe, angetaka kujua mafundisho yanayotolewa ya athari gani kwa amani yetu basi,
 
DC Magoti amemtaka Sheikh huyo kufika kituo cha Polisi Kisarawe ili kuandikisha maelezo ya kina kuhusu kilichotokea na kujifunga kuwa anaondoa huduma hiyo.
Petro kuuzungumzia Msikiti!!!
😷😷
 
Mbona DC hakulalamikia mafunzo? DC kasema mazingira ya kulala ndio tatizo na si elimu itolewayo hapo, au bando mzozo?
 
Hatari ya kisarawe ni nini? Huyo mkuu wa wilaya angekuwa na akili asingeweka udini kama wewe, angetaka kujua mafundisho yanayotolewa ya athari gani kwa amani yetu basi,
Kuna sehemu nimeongea udini? nimeongea according to reference nilicho kiona kupitia documentary ya Boko Haram,sababu road map yake ilianza kwa style kama hii ya Kisarawe au unazani Boko Haram iliibuka tu from no where?

Vp unajua content wanazofundishwa?
Vp silabasi wanayo itumia?
Walimu je wanauelewa na wanacho kifundisha kina impact gani kwenye makuzi ya akili ya mtoto?
Vp mzingira ni salama kwa makuzi ya mtoto?
Vp afya zao kimwili na kiakili?

DC anataka kujua zaidi na ndio maana kamwabia aende kituoni kwa maelezo zaidi,ili apaje majibu ya undani zaidi juu ya hayo maswali ya hapo juu.
 
Hata kile cha ukerewe Huwa sielewi dhamira yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…