GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Watoto wa Kiislamu ni wengi kwenye baadhi ya mikoa kama Tanga, Pwani, na Zanzibar. Lakini kwa maeneo mengine mengi, wengi ni ama Wakristo au wapagani.Watanzania wengi hatuko huru kwenye vichwa vyetu na mara nyingi sana fikra zetu zimefungwa either kwa ushabiki au kwa kuwa na uelewa mdogo.
Mohamed Said hapo juu amegusia jambo fulani nyeti sana ambalo watanzania wote kuna mahala tunapaswa kuwa serious nalo saana.
Shule za Serikali za msingi kawaida kwa kiasi kikubwa ndio zinazoandikiasha wanafunzi wengi sana wa kiislam na wengi sana ndio huhitimu shule hizi elimu ya msingi, kutokana na umasikini kwenye jamii kubwa ya waislamu, vijana hawa wengi huishia darasa la saba na kukosa uelekeo na hujikuta hawana namna zaidi ya kutafuta uelekeo kwenye mafundisho ya dini ambayo kwao hayana gharama zozote.
Tunapotaka kupambana na issue ya za kigaidi kwa kuamini wahusika ni vijana wa kiislam basi hatuna budi pia kuchimba mzizi wa tatizo, kama hawa vijana huachwa wakizagaa baada ya kuhitimu shule za msingi na wengi wao ndio hao waislamu hatuoni kama itakuwa rahisi kutegeka na kuingia kwenye makundi haya?
Shule ya Msingi niliyosoma kipindi chetu, katika darasa la wanafunzi 79, Waislamu wa kiume na kike walikuwa hawafiki 10.