Wakuu,
Mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Rais Samia amevuka matarajio ya watanzania walio wengi. Ameonyesha mwanga na nuru pale ambapo hapakuwa na nuru wala mwanga
Ni miaka minne pekee imetosha kuuonesha umma wa Watanzania kuwa wanawake wanaweza.
Nakushukuru sana Rais wangu Samia kwa kueneza huduma za jamii hasa maeneo ya vijijini ambavyo huduma hizo katika awamu zingine zilikuwa ni ndoto kufika huko.
Huduma muhimu za jamii hasa afya,elimu,ushafiri(barabara) na umeme vyote vimeenea Tanzania nzima
Leo nimekiri wazi kuwa Mama Samia hana tunachomdai yeye ndiye anayetudai
Leo mapema asubuhi nilitembelea hospitali mpya ya wilaya,nimejionea jinsi gani Rais wangu alivyo na uchungu wa kuiletea maendeleo Tanzania, kumejengwa majengo makubwa na yakisasa,madaktari wanatibu vizuri huku huduma za mama,mtoto pamoja na wazee zikitolewa bure.
Kwa upande wangu Mama Samia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sina ninachokudai.
Wewe ndiye unaenidai kura yangu kwako
Holoholo: kwa sasa Tabora