Kishindo kingine cha Rais Samia, tunasubiri jina la Waziri mpya wa Jinsia

Napata wasiwasi kama kuna kufikiria gharama zitakazoongezeka. Bila kusema kuwa kwa namna zilivyo Sasa, zimefifishaje utekelezaji wa majukumu, basi kutenganisha tena ni namna tu ya kumuandalia mtu wake nafasi ya kula.

Kwa sababu Idara ya Kuu ya Maendeleo ya Jamii ina Katibu wake Mkuu, Dr. John Jingu, na ina vote yake.i e ina bajeti yake na majukumu yake yanayojitegemea, kadhalika Idara kuu ya Afya ina Katibu Mkuu wake, Prof. Abel Makubi na Vote yake.

Sioni hata logic ya kuona hili suala nalo kama la msingi. Kwa kuwa hakuna namna yoyote muunganiko huo unaathiri utekelezaji wa majukumu ya Idara zote mbili.

Au anataka kutuaminisha kuwa Waziri ameshindwa kuzihudumia, au ndo anataka kumpandisha Mzenj, Mwanaidi kuwa Waziri kamili, na kuleta mtu mwingine ambaye anaona amemsahau ili waendelee kutafuna vya wanyonge?

Kuzitenganisha tena ni kuongeza matumizi tu maana muunganiko wa sasa hauathiri chochote katika utekelezaji wa majukumu.
 
Atuondolee yule bi mdashi shemeji ya Bishop wa Ubungo. Afya apewe mtu mwingine tena asiwe Dr by profession.
 
Rais Samia Suluhu Hassan, anaendelea kutakata na kuitakatisha Tanzania. Amejibu ombi la muda mrefu la watu wengi, kuhusu kuitenganisha Wiazara ya Afya na idara nyingi zilizokuwa chini yake.

Rais amesema sasa Wizara ya Afya itashughulika na Afya pekee, kisha Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto vitapelekwa kwenye Wizara yake.

Jambo hili litafanya Wizara ya Afya iongeze nguvu zaidi kwenye kuhudumia Afya za Watanzania, huku ustawi wa Jamii na masuala ya wanawake, watoto na wazee vikipewa uzito unaostahili.

Jambo hilo limepokelewa vyema na watu waliokuwa ukimbini, huku pia likipokelewa kwa shangwe na watu wema kupitia mtandaoni.

hakika MAMA YUKO KAZINI
Hii wizara ya maendeleo ya wanawake, na, na, na amteue Zitto Kabwe mbunge na amfanye waziri wa hiyo wizara
 
Napata wasiwasi kama kuna kufikiria gharama zitakazoongezeka. Bila kusema kwa namna zilivyo zimefifishaje utekelezaji wa majukumu basi ni namna tu ya kumuandalia mtu wake nafasi ya kula.

Kwa sababu Idara ya Kuu ya Maendeleo ya Jamii Katibu wake Mkuu, Dr. John Jingu, na ina vote yake.i e ina bajeti yake na majukumu yake yanayojitegemea, kadhalika Idara kuu ya Afya ina Katibu Mkuu wake, Prof. Abel Makubi na Vote yake.

Sioni hata logic ya kuona hili suala nalo kama la msingi. Kwa kuwa hakuna namna yoyote muunganiko huo unaathiri utekelezaji wa majukumu ya Idara zote mbili.

Au anataka kutyaminisha kuwa Waziri ameshindwa kuzihudumia, au ndo anataka kumpandisha Mzenj, Mwanaidi kuwa Waziri kamili, na kuleta mtu mwingine ambaye anaona amemsahau ili waendelee kutafuna vya wanyonge?

Kuongeza matumizi tu lkn muunganiko huo hauathiri chochote katika utekelezaji wa majukumu.
Don't be myopic madam Lugumya !! Hizi wizara hazijawahi kuwa pamoja toka Uhuru mpaka Mwendazake alipoziunganisha mwaka 2015.

Jina la wizara linaitwa "Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto."

Jina lenyewe tu ni pasua kichwa!! Hakuna Wizara nyingine yenye jina refu namna hiyo. Maamuzi na tija yanachelewa sana hususan kwa upande wa Jinsia Wazee na Watoto kwa vile Mawaziri wengi wamekiwa na affiliation ya Afya

Kuhusu gharama, inayoongezeka ni gharama za Waziri na ofisi yake tu
 
Labda kama ulikusudia kunitukana hapo ni sawa au una chuki tu binafsi na Lugumya, Mimi tusi lako nimelipokea.

Lakini tukienda kwenye hoja, unapoegemea kwenye urefu wa Jina na muda eti tangu uhuru, utetezi unakosa mantiki. Ulifikiri ni intellectual lakini kwa utetezi wako, kidole Cha myopic kimerejea upande wako. Urefu wa Jina au kutobadilishwa kwa jina la Wizara tangu uhuru hakuna uhusiano wowote na utendaji wenye tija.

Hivyo, hizo si sababu za Msingi za kufanya zitenganishwe tena Bi Stuxnet. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, yaweza kuwa ina jina refu, au haijabadilishwa tangu uhuru kama unavyohisi, lakini je ni nini kimeharibika kutokana na kuunganishwa?

Je, Ufanisi na tija kwenye Idara kuu zote mbili (Afya na Maendeleo ya Jamii) vimeshuka ukilinganisha na kipindi ambacho hazikuunganishwa? Je, mahitaji ya kuwahudumia viongozi yameongezeka au yameshuka baada ya kuunganishwa?

Fikiria vizuri dada Stuxnet na ujikite kwenye hoja ndugu yangu, badala ya kukanyaga gia bila kujua uelekeo! Naomba unisaidie kujua muunganiko umeathiri nini kiutendaji na utengano utaimarishaje/kufukiaj mashimo yaliyosababishwa na muunganiko?

Focus iwe kutumia rasilimali ndogo bila kuathiri malengo. Vinginevyo kama vipaumbele havifikiwi kutokana na kuunganisha mi sina Pingamizi, lkn kama sababu ni zile hoja zako za urefu na umri basi una shida ya kifikra!
 
In the longrun inabidi iwekwe kwenye katiba wizara za serikali na haiwezekani kubadili mpaka katiba ibadilishwe au pawepo na dharura na bunge liridhie. Haya mambo ya kuunda, kuunganisha, kisha kuunda upya ni gharama kwa fedha za walipa kodi
Hili swala la Katiba kwa nchi yetu ni sawa na mtu mwenye upara aliyebebeshwa gunia la mbigiri kichwani anashauriwa alitue zihamishiwe kwenye mfuko wa plasitiki anakataa. Damu zinamchuruzika kichwani lakini anaendelea kutembea nalo kwa sababu tu kaahidiwa malipo?
 
Labda kama ulikusudia kunitukana hapo ni sawa au una chuki tu binafsi na Lugumya, Mimi tusi lako nimelipokea.

Lakini tukienda kwenye hoja, unapoegemea kwenye urefu wa Jina na muda eti tangu uhuru, utetezi unakosa mantiki. Ulifikiri ni intellectual lakini kwa utetezi wako, kidole Cha myopic kimerejea upande wako. Urefu wa Jina au kutobadilishwa kwa jina la Wizara tangu uhuru hakuna uhusiano wowote na utendaji wenye tija.

Hivyo, hizo si sababu za Msingi za kufanya zitenganishwe tena Bi Stuxnet. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, yaweza kuwa ina jina refu, au haijabadilishwa tangu uhuru kama unavyohisi, lakini je ni nini kimeharibika kutokana na kuunganishwa?

Je, Ufanisi na tija kwenye Idara kuu zote mbili (Afya na Maendeleo ya Jamii) vimeshuka ukilinganisha na kipindi ambacho hazikuunganishwa? Je, mahitaji ya kuwahudumia viongozi yameongezeka au yameshuka baada ya kuunganishwa?

Fikiria vizuri dada Stuxnet na ujikite kwenye hoja ndugu yangu, badala ya kukanyaga gia bila kujua uelekeo! Naomba unisaidie kujua muunganiko umeathiri nini kiutendaji na utengano utaimarishaje/kufukiaj mashimo yaliyosababishwa na muunganiko?

Focus iwe kutumia rasilimali ndogo bila kuathiri malengo. Vinginevyo kama vipaumbele havifikiwi kutokana na kuunganisha mi sina Pingamizi, lkn kama sababu ni zile hoja zako za urefu na umri basi una shida ya kifikra!
Focus kwenye jinsia, wazee na watoto imepungua. Nadhani unasikia kila wakati malalamiko ya Kambi za kulelea wazee za Kolandoto, Sukamahela namna ambavyo wazee wanateseka.

Hapa Dar es Salaam nadhani mwaka Jana mwishoni tuliina watu waiojiweza wanavyoletwa kutoka mikoani nankutumikishwa kama omna omna. Nakupa hayo machache kwanza
 
Hilo si tatizo la Wizara kuungana ndugu yangu, huo ni utashi wa Kamishina wa Ustawi wa Jamii na Katibu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutotoa kipaumbele kwa hayo uliyoyataja! Hata kabla ya kuunganishwa hali haijawahi kuwa nzuri katika maeneo yote uliyoyataja! Kwa hiyo tatizo si kuunganishwa, tatizo ni kutoliwekea mkazo suala hilo.

Na napenda nikupe ukweli kwamba kwa mazingira ya Makao ya Wazee (Makambi) kwa Sasa yameboreshwa kiasi fulani ukilinganisha na miaka sita nyuma kabla ya kuungana. Kolandoto ambayo ilikarabatiwa hivi karibuni kwa kutumia chuo Cha Ufundi Misungwi iko vizuri kuliko ya miaka 6 nyuma kabla ya kuungana.

Shule za Maadilisho pia walau kwa Sasa zimeamka ukilinganisha na kipindi Cha nyuma, hata Ujenzi wa makao ya watoto Kikombo ni hivi karibuni, Wizara zikiwa zimeungana.

Leo uje useme kwamba chanjo hazifiki kwa wakati kwa sababu Wizara zimeungana? Inakuja akilini kweli?

Sukamahela, Bukumbi, Kolandoto, Nyabange ya Sasa si sawa na zile za kipindi cha Sofia Simba, Anna Makinda, au Rose Migiro wakiwa Mawaziri. Kipindi Cha Ummy zikiwa zimeungana ndo mabadiliko makubwa yametokea Afisa Ustawi! Fuatilia vizuri, utagundua kuwa ni gharama tu zinaongezeka hasa hiyo ofisi wanayoenda kuiongeza. Lakn kwenye utendaji nothing [emoji682]
 
Rais Samia Suluhu Hassan, anaendelea kutakata na kuitakatisha Tanzania. Amejibu ombi la muda mrefu la watu wengi, kuhusu kuitenganisha Wiazara ya Afya na idara nyingi zilizokuwa chini yake.

Rais amesema sasa Wizara ya Afya itashughulika na Afya pekee, kisha Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto vitapelekwa kwenye Wizara yake.

Jambo hili litafanya Wizara ya Afya iongeze nguvu zaidi kwenye kuhudumia Afya za Watanzania, huku ustawi wa Jamii na masuala ya wanawake, watoto na wazee vikipewa uzito unaostahili.

Jambo hilo limepokelewa vyema na watu waliokuwa ukimbini, huku pia likipokelewa kwa shangwe na watu wema kupitia mtandaoni.

hakika MAMA YUKO KAZINI
Ni jambo jema.
 
Unashangilia wakati gharama mpya hizo wakati ndugu zako kule kijijini wakiendele kuishi chini ya Dolla moja? Huu ujinga utatutoka kweli?
 
Yaani tunavyokuwa serious kulilia uwepo wa wizara fulani, utadhani kuna mambo yatabadilika vile...

Wizara ilipaswa tu kuitwa Afya na Ustawi wa Jamii, hizo makololo sijui maendeleo ya wazee, watoto etc zilikuwa zinarefusha tu jina...

Mbona wizara ya Afya kwa ujumla imefanya poa, kuna mabadiliko mengi sana makubwa kwa miaka ya karibuni yameonekana...
 
In the longrun inabidi iwekwe kwenye katiba wizara za serikali na haiwezekani kubadili mpaka katiba ibadilishwe au pawepo na dharura na bunge liridhie. Haya mambo ya kuunda, kuunganisha, kisha kuunda upya ni gharama kwa fedha za walipa kodi
Kama United States of America. Hata Kenya hapo tu

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom