Kishindo kingine cha Rais Samia, tunasubiri jina la Waziri mpya wa Jinsia

Kishindo kingine cha Rais Samia, tunasubiri jina la Waziri mpya wa Jinsia

Tumetoka mbali sanaa

Mfano shule za msingi walipochanganya masomo aina 2-3 tofauti na kusema "study za kazi" sayansi ya jamii
Zamani somo la siasa/geographia/sayansi-kimu/historia etc yalikuwa yakijitegemea .... baada ya mda yakajumuishwa baadhi, wengine wakasema sawa na wengine wakasema sio sawa

Huu muunganisho wa wizara kwa nchi nyingi wizara ya afya "ministry of health' inasimama yenyewe. anyway ni mipango ya kiutendaji
Nakumbuka kipindi cha Nyerere, Mwinyi, na Mkapa tulikuwa na wizara ya Afya, hii ilisimama yenyewe. Pia kulikuwa na Wizara ya Ustawi wa jamii, jinsia, wanawake na watoto. Nakumbuka ustawi wa jamii ilikuwa na vyuo vya ustawi wa jamii vingi tu. Pia kulikuwa na uanzishwaji wa vituo vya kulelea wazee. Sikuhizi nahisi wazee wanasahaulika.
Ila ifikie mahala tuwe na wizara muhimu za kudumu, kuliko kila Rais akija ni kubadili hiki ili aone kaanzisha kitu.

Kwa Tanzania unapoanzisha wizara unatumia mabillioni ya shilingi. Ukisikiliza wakati wa bajeti robo tatu ya bajeti uenda katika matumizi ya kawaida. Ni fedha ndogo tu ambayo uenda katika miradi.

Nchi imekaa kimvurugano. Leo hiki kesho kile, kama ulivyosema hata elimu inachezewa tu na waziri katoka usingizini anahamua atakavyo.

Mie nadhani kikubwa ilengwe jamii nzima kuimarisha maisha ya watanzania. Ningefurahi kusikia kuna gharama za matibabu zimeshuka, au mwananchi anaweza pata matibabu kwa bima ya afya kwa watanzania wote ambayo inamalipo nafuu.
Ningefurahi kusikia gharama (Riba) za kukopa ktk mabenki zimeshushwa. Na kuwa mkopo itatolewa kwa haraka. Ni mengi haya machache.

Nahitaji kuona ni nini serikali inafanya na matokeo yake yanamwezesha moja kwa moja mwananchi. Kumfanya mwananchi aishi kwa raha si kuwa na mawazo. Hii ndo kazi au wajibu wa serikali.

Zamani Tanzania baadhi ya mambo ilikuwa kama Ulaya. Matibabu bure, shule, vyuo bure hadi kusafirishwa. Wanafunzi hospitali hutakiwi subiri unaingia moja kwa moja kwa daktari.
Mtaani kulikuwa na magari maalum ya taka. Ajira nyingi zilikuwa viwandani.
Wanafunzi walikula mashuleni hasa wa sekondari.
Haya ndo nasema yanampa unafuu mwananchi ili aenjoy maisha. Siku hizi tunamafisadi tu yanataka yale yenyewe.
 
Mirija ya ulaji inaenda kuongezeka,,, Wizara itahitaji ofisi nchi nzima...

Vijana watapata ajira pia,, au ndio kinatengenezwa cheo ili mtu fulani apate ulaji
Dr. Hamis Kigwangala
 
ka nchi kadogo haka ,eti wizara kubwa,uvivu wa kufanya kazi tu,na kutuongezea garama walipa kodi.kuna ulazma gani wa kuongeza idadi ya wizara!!??,rais ajaye atavunja na kurejesha mahala pake,kuwa na utitili wa mawizara sio ndo kuongeza ufanisi Bali ni kutuongezea garama !!,na hakuna ufanisi wowote utakaoonekana !! mbona enz za mkwere miwizara ilikuwa kibao ,mbona hatukuuona huo ufanisi !?,badala yake tulishuhudia ufisadi wa kiwango Cha 6G.
 
Huu uhuni wa kutenganisha na kuunganisha ndio umekuwa mchezo wa watawala wa kiCCM tangu uhuru, na karibu mara zote yamekuwa mambo yasiyokuwa na tija.

Wataalamu waliwahi kupendekeza haya;

1. Nchi yetu inahitaji baraza la mawaziri lisilokuwa na zaidi ya watu 20 tu (yaani Rais, Makamu wa rais, waziri mkuu, mawaziri kamili wasiozidi 15 na mawaziri wadogo (manaibu) wawili tu. (Kwanini? Kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali, kupunguza urasimu wa kiutendaji na kuongeza uwajibikaji)

2. Kuwe na wizara kumi na tano tu (wizara muhimu za lazima kuwepo ni Fedha, Ulinzi, Elimu, Mambo ya nje, Sheria, Afya, Huduma, Jamii, Uzalishaji)
 
Nini mantiki kuwa na wizara ya watoto, jinsia, wanawake na wazee, halafu kuna wizara nyingine inahusika na vijana na walemavu?
Kwanini kusiwe na wizara ya jamii (Ministry of Society!) ili mambo yote hayo yawekwe kapu moja?

Nini mantiki ya majeshi yetu kuwa kwenye wizara tofauti? Yote yanahusika na ulinzi na usalama lakini yako kwenye wizara tofauti! Yaani Uhamiaji, Polisi na Magereza ziko wizara ya mambo ya ndani, JKT na JWTZ ziko wizara ya ulinzi, TISS ofisi ya Rais nk.

Nini mantiki ya kuwa na wizara ya fedha, wizara ya viwanda na biashara, wizara ya uwekezaji? Kwanini kusiwe na wizara moja tu inayohusika na fedha tu?

Nini mantiki ya kuwa na wizara ya habari ya habari? Ama wizara ya michezo?
 
Kuna wizara zilitakiwa kuunganishwa ili kupunguza mzigo kwa wananchi mfano wizara ya mambo ya ndani na wizara ya ulinzi ingekuwa wizara moja
 
Back
Top Bottom