Ralph Tyler
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 2,828
- 3,579
Kuchanganya Wizara ya Afya na hizo sekta nyingine kumeathiri sana kwa kudhoofisha vipaumbele vya sekta zote husika. Kwa mfano kipaumbele cha Afya kikiwa ni corona au malaria ujue vipaumbele vya jinsia na kaya masikini vinafifia kwa sababu waziri mbeba sera ni yuleyule. Tujifunze kwa nchi zilizoendelea, hazichanganyi wizara za kisekta na mambo mengine.Napata wasiwasi kama kuna kufikiria gharama zitakazoongezeka. Bila kusema kuwa kwa namna zilivyo Sasa, zimefifishaje utekelezaji wa majukumu, basi kutenganisha tena ni namna tu ya kumuandalia mtu wake nafasi ya kula.
Kwa sababu Idara ya Kuu ya Maendeleo ya Jamii ina Katibu wake Mkuu, Dr. John Jingu, na ina vote yake.i e ina bajeti yake na majukumu yake yanayojitegemea, kadhalika Idara kuu ya Afya ina Katibu Mkuu wake, Prof. Abel Makubi na Vote yake.
Sioni hata logic ya kuona hili suala nalo kama la msingi. Kwa kuwa hakuna namna yoyote muunganiko huo unaathiri utekelezaji wa majukumu ya Idara zote mbili.
Au anataka kutuaminisha kuwa Waziri ameshindwa kuzihudumia, au ndo anataka kumpandisha Mzenj, Mwanaidi kuwa Waziri kamili, na kuleta mtu mwingine ambaye anaona amemsahau ili waendelee kutafuna vya wanyonge?
Kuzitenganisha tena ni kuongeza matumizi tu maana muunganiko wa sasa hauathiri chochote katika utekelezaji wa majukumu.
Mifano ya wizara za kisekta ni Afya, Elimu (zote chekechea hadi PhD), Kilimo (mambo yote yanayosomwa SUA yaani agriculture, livestock, forestry, fisheries0, Ulinzi, Fedha (hazina, uchumi, mipango humohumo), Miundombinu (yote pamoja na ya mawasiliano), Viwanda (Industry, siyo Factory. Industry ni pana inahusisha biashara zote ), Mambo ya ndani, Ardhi , Mambo ya Nje na Sheria. Kila moja ya sekta hizi inafaa kuwa na waziri kamili na idara zake.
Wizara za uratibu ni kama Tamisemi, Utawala Bora, Sera. Hizi zinafaa kuwa katika ofisi inayoratibu shughuli za serikali ambayo ni ofisi ya waziri mkuu, na hapa mawaziri wawili tu wanatosha: mmoja TAMISEMI na mwingine aratibu yote yaliyobaki.
Wizara za mambo mtambuka ni kama hizo za maendeleo ya jamii, jinsia, mazingira, kazi (na ajira), michezo, habari, utamaduni. nk. Hapa unaweza kuchanganya mambo ya jinsia, utamaduni na michezo ukaweka kwenye wizara moja ya maendeleo ya jamii. Kazi inaweza kusimama pekee. Mazingira inaweza kuchaganywa na ardhi kwa sababu planning yake inaweza kufanywa na kusimamiwa pamoja. Utalii iwekwe kwenye biashara. Maliasili ichanganywe kwenye mazingira na ardhi. Madini iende kwenye industry. Nishati na vitu vilivyobaki vya geology iwe pamoja na maji.