Tumetoka mbali sanaa
Mfano shule za msingi walipochanganya masomo aina 2-3 tofauti na kusema "study za kazi" sayansi ya jamii
Zamani somo la siasa/geographia/sayansi-kimu/historia etc yalikuwa yakijitegemea .... baada ya mda yakajumuishwa baadhi, wengine wakasema sawa na wengine wakasema sio sawa
Huu muunganisho wa wizara kwa nchi nyingi wizara ya afya "ministry of health' inasimama yenyewe. anyway ni mipango ya kiutendaji
Nakumbuka kipindi cha Nyerere, Mwinyi, na Mkapa tulikuwa na wizara ya Afya, hii ilisimama yenyewe. Pia kulikuwa na Wizara ya Ustawi wa jamii, jinsia, wanawake na watoto. Nakumbuka ustawi wa jamii ilikuwa na vyuo vya ustawi wa jamii vingi tu. Pia kulikuwa na uanzishwaji wa vituo vya kulelea wazee. Sikuhizi nahisi wazee wanasahaulika.
Ila ifikie mahala tuwe na wizara muhimu za kudumu, kuliko kila Rais akija ni kubadili hiki ili aone kaanzisha kitu.
Kwa Tanzania unapoanzisha wizara unatumia mabillioni ya shilingi. Ukisikiliza wakati wa bajeti robo tatu ya bajeti uenda katika matumizi ya kawaida. Ni fedha ndogo tu ambayo uenda katika miradi.
Nchi imekaa kimvurugano. Leo hiki kesho kile, kama ulivyosema hata elimu inachezewa tu na waziri katoka usingizini anahamua atakavyo.
Mie nadhani kikubwa ilengwe jamii nzima kuimarisha maisha ya watanzania. Ningefurahi kusikia kuna gharama za matibabu zimeshuka, au mwananchi anaweza pata matibabu kwa bima ya afya kwa watanzania wote ambayo inamalipo nafuu.
Ningefurahi kusikia gharama (Riba) za kukopa ktk mabenki zimeshushwa. Na kuwa mkopo itatolewa kwa haraka. Ni mengi haya machache.
Nahitaji kuona ni nini serikali inafanya na matokeo yake yanamwezesha moja kwa moja mwananchi. Kumfanya mwananchi aishi kwa raha si kuwa na mawazo. Hii ndo kazi au wajibu wa serikali.
Zamani Tanzania baadhi ya mambo ilikuwa kama Ulaya. Matibabu bure, shule, vyuo bure hadi kusafirishwa. Wanafunzi hospitali hutakiwi subiri unaingia moja kwa moja kwa daktari.
Mtaani kulikuwa na magari maalum ya taka. Ajira nyingi zilikuwa viwandani.
Wanafunzi walikula mashuleni hasa wa sekondari.
Haya ndo nasema yanampa unafuu mwananchi ili aenjoy maisha. Siku hizi tunamafisadi tu yanataka yale yenyewe.