Mimi ni Muislam, na huyu ni Shekhe wa pili ananikasirisha kupita kiasi kwa kutumia dini yangu na imani yangu kwa manufaa yao wenyewe. Wa kwanza akiwa yule alosimama mbele ya rais na kusema anaomba dua kwa yesu!
Huyu Ponda sasa anainuka na kusema uongo hapa, Waislamu hatukukaa na kubaliana kuwa tutapiga kura zetu kukipa chama chochote kile. Inasikitisha sana kuona shekhe anasimama katika umati wa watu na kusema yasio ya kweli. Ningelipenda kujua ni vipi alikuja na conclusion kuwa sote tumekubaliana kupiga kura chadema, wapi tulikutana au wawakilishi wetu walikutana na kukubaliana na hayo, na hao waliosema wanatuwakilisha Waislamu wote tanzania walichaguliwa na nani.
Kama nilivyosema mimi ni Muislamu na hakuna mtu alokuja kuniuliza kama Muislamu nitachagua chama gani, ningelipenda kujua waislamu wangapi hapa wamefuatwa na kushawishiwa kisha kukubali kuchagua CHADEMA.
Kuna tafauti kubwa unaposimama na kuwataka watu wa imani fulani wapige kura kuchagua chama fulani na kusema kuwa watu wa imani fulani wamekubaliana kuchagua chama fulani. Waislamu hatujakubaliana kwa pamoja kuchagua chama chochote kile.
Kauli kama hizi za hawa watu wanaojiita viongozi wa kidni zinaweza kuzusha chuki na ugomvi usio na maana kabisa.