Uchaguzi 2020 Kishindo: Sheikh Ponda atoa neno kwenye mkutano wa Lissu Dodoma, Uwanja walipuka kwa shangwe

Uchaguzi 2020 Kishindo: Sheikh Ponda atoa neno kwenye mkutano wa Lissu Dodoma, Uwanja walipuka kwa shangwe

Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo Wanaomuunga Mkono Tundu Lissu wanavyojitokeza na kuzidi kuongeze

View attachment 1603481

Suali kidogo, huyu jamaa hapo ni kwa nini amavaa balacava katika mkutano wa hadhara? Anafanya mambo gani ya sirisiri kiasi kwamba hatakki kujulikana? Pia kuna jamaa amevaa fulana yenye bendera ya USA kwa trump na binden nao wanagombani hadi tanzania?
 
Suali kidogo, huyu jamaa hapo ni kwa nini amavaa balacava katika mkutano wa hadhara? Anafanya mambo gani ya sirisiri kiasi kwamba hatakki kujulikana? Pia kuna jamaa amevaa fulana yenye bendera ya USA kwa trump na binden nao wanagombani hadi tanzania?
Kuna madhara yoyote?
 
Sakata la uamsho linakurupukiwa kama sakata la mkulima. Kuna mengi hapa sema mihemko ya kutafuta kura imetawala. Umeshasikia mauaji yanayoendela mtwara?wakikamatwa wale kesho na kesho kutwa watu mtalalamika na kuona wameonewa.

Kama mmeamua kumtumia ponda basi msijelalamika wenzenu wanapowatumia viongozi wa dini maana wote mnapita njia zile zile
Huwezi kua upande wa oppressor alafu useme njia ni ile ile , hakuna kitu kama hicho
 
Hivi kumtumia Sheikh Ponda kufanya kampeni ndio kupata ushindi?

Sheikh Ponda ana ushawishi gani kwa waislamu kiasi cha kuona atawapatia kuraza waislamu?

Kama Chama makini Chadema ingetafakari kutumia mtu ambae anataka kuwaletea kura za waislamu. Maana Bakwata hawamkubali Ponda, na wakristo je?
 
Mimi ni Muislam, na huyu ni Shekhe wa pili ananikasirisha kupita kiasi kwa kutumia dini yangu na imani yangu kwa manufaa yao wenyewe. Wa kwanza akiwa yule alosimama mbele ya rais na kusema anaomba dua kwa yesu!

Huyu Ponda sasa anainuka na kusema uongo hapa, Waislamu hatukukaa na kubaliana kuwa tutapiga kura zetu kukipa chama chochote kile. Inasikitisha sana kuona shekhe anasimama katika umati wa watu na kusema yasio ya kweli. Ningelipenda kujua ni vipi alikuja na conclusion kuwa sote tumekubaliana kupiga kura chadema, wapi tulikutana au wawakilishi wetu walikutana na kukubaliana na hayo, na hao waliosema wanatuwakilisha Waislamu wote tanzania walichaguliwa na nani.

Kama nilivyosema mimi ni Muislamu na hakuna mtu alokuja kuniuliza kama Muislamu nitachagua chama gani, ningelipenda kujua waislamu wangapi hapa wamefuatwa na kushawishiwa kisha kukubali kuchagua CHADEMA.

Kuna tafauti kubwa unaposimama na kuwataka watu wa imani fulani wapige kura kuchagua chama fulani na kusema kuwa watu wa imani fulani wamekubaliana kuchagua chama fulani. Waislamu hatujakubaliana kwa pamoja kuchagua chama chochote kile.

Kauli kama hizi za hawa watu wanaojiita viongozi wa kidni zinaweza kuzusha chuki na ugomvi usio na maana kabisa.
 
Labda waibe kama walivyozoea, ila NEC wakitenda haki CCM kwisha.
Ni kazi yetu SISI wananchi kuhakikisha kuwa hatuchezewi tena na NEC wala wachumia tumbo wengine.
SASA BASI
1603008827510.png
 
Sheikh ponda akimpigia Lissu kampeni ni sawa ila sheikh wa bakwata akipigia ccm kampeni ninkosa wote hao wanamakosa kwani hawana haki ya kuwasemea waumini wa dini zao
 
Hii kuchanganya mambo ndio ninapouona ujinga wa upinzani, yaani mtafanya chochote alimradi kwenu ni hayo madaraka tu.

Yaani hata kama Mtu umeichoka ccm lakini Upinzani wamekosa kabisa Watu wenye hekima wa kuchuka nafasi, Lisu ni Mwanaharakati si Mwanasisasa.
Ubongo wako umeoza
 
Shekh Ponda angewamaliza waislam kumchagua lissu, kwa kuwaambia akipita lissu, mashekh walofungwa waachiwe huru
 
Wanasiasa wetu wamekosa hoja kabisa, sasa wanatumia dini kama kigezo kwamba waislamu wamchague Lissu, halafu wakristo wamachague nani.

Kwani hapo tunachagua kiongozi wa dini. Viongozi wetu wa dini wangebaki neutral na vyama vinavyojielewa visingejiingiza kwenye huo utaratibu wa kuombewa kura na viongozi wa dini.

Kiongozi anasema Waislamu tuta kana kwamba Waislamu wamekaa kikao wakatoa hayo maamuzi.

Mungu awajalie viongozi hekima sana. Unaposema hivyo kiongozi wa dini unasababisha huyo unaemnadi aonekane ni mdini na ametumwa na dini yako kwa maslahi ya dini hiyo hivyo wapiga kura wa dini zingine hawahusu na hawana maslahi nae.

Sent from my Infinix X603 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom