KISUTU: Jamhuri kuleta mashahidi 24, vielelezo 19 kesi ya Mbowe na wenzake

KISUTU: Jamhuri kuleta mashahidi 24, vielelezo 19 kesi ya Mbowe na wenzake

MWALLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2006
Posts
16,952
Reaction score
10,500
Mwenyekiti wa chama taifa Mhe. Freeman Mbowe amewasili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo leo Agosti 23, 2021 kesi Na.63/2020 ya Uhujumu Uchumi yenye mashtaka ya Ugaidi ndani yake itaanza kusomwa kwa hati ya mashtaka na ushahidi kwa hatua ya awali.


UPDATE: Mashtaka
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam wamesomewa maelezo ya mashtaka mbalimbali yanayowakabili ikiwemo la kutaka kudhuru viongozi wa Serikali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.


Upande wa mashitaka unasoma mashitaka kwa kusema kuwa; Halfan Bwire Hassan, Adam Hassan Kasekwa, Mohamed Abdallah Ling'wenya na Mhe. Freeman Mbowe wanatuhumiwa;

1. Freeman Mbowe anatuhumiwa kufadhili vitendo vya Ugaidi kwa kutoa shilingi za kitanzania laki sita ( 600,000). Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa Matumizi ya fedha hiyo ni kama ifuatavyo;
1. Kulipua vituo vya Mafuta
2.kulipua mikusanyiko ya watu
3.Kukata miti na kusambaza barabarani

2. Kula njama na kusabisha majeraha kwa aliyekuwa mkuu wa wilaya Hai, Lengai Ole Sabaya

3. Watuhumiwa wote ambapo wanatuhumiwa kushiriki vikao na Kula Njama za kutenda Ugaidi

4. Mshtakiwa wa pili anashitakiwa kumiliki bastola yenye risasi tatu kwa ajili ya kutenda kosa la ugaidi.

5. Mshtakiwa wa tatu anatuhumiwa kumiliki nguo, begi na koti za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWT) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT.)

-
UPDATE: Mashahidi 24 vielelezo 19 kesi ya Mbowe na wenzake

Mashahidi 24 na vielelezo 19, wanatarajia kutoa ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Miongoni mwa mashahidi hao, yupo aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Boaz.

Hayo yameelezwa leo, Agosti 23, 2021 na upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga akisaidiana na Ester Martin, wakati wakiwasomea maelezo ya mashaidi na vielelezo (Commital Proceedings) washtakiwa hao, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba.

Credit: Mwananchi
 
Mungu mbariki Mbowe

KAMANDA_WOTE_MASHUJAA,_WAPENDA_HAKI,_WAFIA_CHAMA__tukutane_KIsutu_leo_mapema_kwenye_kesi_ya_mw...jpg
 
serikali yako inaendesha kesi hii kisanii na kwa kuviziavizia.. wameona leo wale wanaofadhili serikali hawaji kusikiliza ndio wamemleta. nnji hii kwa usanii ni hatari sana
kwani walikuwa hawajui kuwa leo gaidi anakuja mahakamani? wameshaipuuza wameona gaidi hana cha kujitetea hapo
 
Back
Top Bottom