INAHUZUNISHA, hata hao bodaboda hapo alikuwa kwenye utafutaji, ana watoto, na pengine alimbeba mtu asiye bodaboda (abiria) aliyekuwa na haraka sana kukimbilia kipato au interest fulani. hakujua kama anaenda kufa siku hiyo, hakuna ajuaye siku wala saa ndo maana tunatakiwa kukesha, tujiweke tayari kwa kutengeneza mambo yetu na Mungu ili tukifa tufe katika Bwana twende mbinguni na kama tukiishi basi tuishi hapahapa duniani tukiwa na Mungu.
UFUNUO 14: 13 INASEMA: Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, andika, heri wafu wafao katika Bwana tangu sana. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
wengi wa wanaosoma hata huu ujumbe hapa, aidha mtaishi au mtakufa muda wowote, leo, kesho, mwakani, au siku msiyoijua, siombei mfe, ila ukweli mchungu ndio huo, cha muhimu ni kwamba mkiishi, andaeni maisha yenu ili muishi na Mungu, ama la mkifa basi muwe mmekufa mkiwa mikononi mwa Mungu (mkiwa mmeokoka) ili mwenda mbinguni badala ya kuzimu. mwenye dhambi akifa anaenda motoni, kwasababu alishupaza shingo yake kwa mahubiri kama hayahaya ya kawaida tu haya, akagoma kuokoka. kwa sasaivi dunia yote labda kasoro North Korea tu ambako hata internet haipo, watu wachache sana hawaelewi kitu kinachoitwa "KUOKOKA" hapa Tanzania ukitaja kuokoka tu mtu anaelewa nini anatakiwa kufanya, ila anafanya shingo yake kuwa ngumu, na anakufa na dhambi zake, na anaenda motoni.
msidanganyike na mapadre na viongozi wengine wa dini wanaowadanganya na kuwaweka mateka kwamba mkifa wao watawaombea maiti zenu na mtasamehewa dhambi hukuhuko maitini. mstari nimeweka hapo juu unasema ukifa matendo yako yatafuatana nawe. utaenda na matendo yako. nafasi ya kutubu ni hii ukiwa mzima, tubo acha dhambi, okoka kwa lugha nyingine yaani, ishi, ili ukifa ufe katika Bwana, ukiishi uishi katika Bwana.
haya sasa, unajua utaishi hadi lini? kama upo kazini, utasafiri hadi kufika nyumbani bila kugongwa na gari? nani anakulinda? huyuhuyo unayemkataa? anayekuelekeza uokoke lakini unashupaza shingo yako? wengine wanakufa kwa kupiga chafya tu baada yakunywa maji. Michael jackson aliweka hadi watu watakaojitolea viongo akipata shida ili aishi miaka mingi ila alikufa kama panya tu. Nakushauri okoka. OMBA SALA HII PAMOJA NA MIMI ILI UOKOKE.
sema: BWANA YESU, MIMI NI MWENYE DHAMBI, NAAMINI YESU KRISTO ALIKUFA KUWA KAFARA LA WOKOVU WANGU, NINATUBU DHAMBI ZANGU ZOTE (ZITAJE KAMA UNAZIJUA), NAOMBA UNISAMEHE, KUANZIA SASA NIWE MALI YAKO, KWA JINA LA YESU KRISTO NINAOMBA, AMEN.
kirahisi tu hivi, kama utakuwa umeomba sala hiyo kwa kumaanisha moyoni, umeshaokoka, Mungu amekusamehe, sasa ili uukulie wokovu, jiunge na wale wanaoamini wokovu kama wewe. simaanishi hao wauza mafuta au maji au keki, namaanisha walokole wa kweli. kuolokoka/kuokoka ni lazima ili umwone Mungu wala usione aibu kuamua au kuonekana umeokoka. Mungu akusaidie.