Kisutu: Mwendokasi na bodaboda zagongana, wawili wafariki

Amen, amen!
shalom!
 
Bodaboda unampa masharti? Labda kama un ampa na mzigo mwengine ila si hawa "maafisa usafirishaji wa UVCCM"
Mzigo mwingine upi ww bibie?.funguka..nikipanda boda yyt namwambia sitaki anikimbize hilo ni la kwanza kabisa kabla sijapanda..mm ndo natoa nauli...shida nyie mkipandishwa mnaona raha anavyochomekea mbele ya magari na vigauni vyenu vinapepea..
 
Vizuri sana,,, hiyo nayo huwa inasaidia na unatakiwa kumwambia mi sina haraka

Hlf madam Kalpana hivi ujasiri wa kuchati juu ya boda nyie wadada huwa mnautoa wapi?
Nilisahau kugusia hili..yani ukipanda boda weka simu ndani ya mkoba au kipima joto chako..bana kwapani na ww uwe dereva wa pili kuangalia hatari yyt ili uweze kumshtua..maana ukute yuko anaendesha ila mawazo hayako hapo..
Mm sichati naogopa kuangusha simu yangu na siwezi kuona hatari mbele..ila naona kama wanaume wamezidi Bey...
 
Mzigo mwingine upi ww bibie?.funguka..nikipanda boda yyt namwambia sitaki anikimbize hilo ni la kwanza kabisa kabla sijapanda..mm ndo natoa nauli...shida nyie mkipandishwa mnaona raha anavyochomekea mbele ya magari na vigauni vyenu vinapepea..
Unamzuia kukatisha katikati ya magari?
Unamzuia kupita with red lights ?
Unamzuia kuchomekea na kupita service road ambazo hujui nini kitatokea?
 
Unamzuia kukatisha katikati ya magari?
Unamzuia kupita with red lights ?
Unamzuia kuchomekea na kupita service road ambazo hujui nini kitatokea?
zamani nilikuwa nawachukia sana boda, nilikuwa nikiendesha gari nawazuia wasinibugudhi, nilikuwa nawaona ni kadhia. siku nilienda mkoa usio nyumbani kwangu, nikalazimika kupanda boda, inikimbize sehemu moja ya muhimu mno, ilikuwa lazima nikimbizwe. hapo ndio niliona umuhimu wao. siku hizi hata nikiona anataka kunichomekea namwacha tu apite, kwasababu sijui yule aliyepakizwa anakimbizwa wapi,wengine wanaenda hospitali, wengine wanaenda kuokoa maisha ya watu, wengine wanaenda airport, wengine wanaenda sehemu muhimu mno. yafaa tuishi kwa kuvumiliana, na Mungu anataka hivyo.
 
Unamzuia kukatisha katikati ya magari?
Unamzuia kupita with red lights ?
Unamzuia kuchomekea na kupita service road ambazo hujui nini kitatokea?
Mbona unaona kama ni ngumu? Kuna boda wastaarabu au ww unakutana na boda mcharuko hakusikilizi? Kuna boda hizo njia hawazipiti na wanaangalia na mteja..kama uko hoya hoya utapitishwa mpka kwny reli..
 
Mbona unaona kama ni ngumu? Kuna boda wastaarabu au ww unakutana na boda mcharuko hakusikilizi? Kuna boda hizo njia hawazipiti na wanaangalia na mteja..kama uko hoya hoya utapitishwa mpka kwny reli..
hivi mtu akiwa anaenda airport, foleni imesimama, zimebaki dakika chache tu checking in ifungwe, hautamwambia boda apite izo njia mnazoona sio halali yao? umepigiwa simu nyumbani mtoto kaungua moto, au kapata shida ambayo unatakiwa kufika haraka mno, una gari, ila kuna foleni haitembei kabisa, hautapita izo njia uwahi kwenda kwa mtoto wako? tuwavumilie hawa boda hata kama wanavunja sheria. wengine wanakuwa na sababu za msingi.
 
Wangefuata utaratibu kusingekuwa na foleni.
Kila mtu akiwa na haraka ndio foleni inaanza.
Kila mtu akiwa na kimgora wasio nachoi wanakesha barabarani.
Ukiwa na haraka wahi kabla ya muda.
 
Kwanini uchelewe airport, huo ni uzembe uliopitiliza na ndio unaopingwa.
Time management and smartness inaanzia na unavyojipanga.
 
Bado tunarudi pale pale..ni ww unavyotaka ndivyo utakavyopata...sasa umeshasema unataka uwahishwe ndo hivyo sasa utawahishwa..ila kama unataka mwendo wa kistaarabu wahi mapema unakoenda nenda na muda ili uende kwa mwendo wa kistaarabu utakaomwelekeza..
 
Ikiwa unataka kupanda bodaboda chagua boda ambaye ni mtu mzima. Unajua ni kwa nini?

Mtu mzima tayari ana majukumu. Anajua kuna watu wanamtegemea. Ameoa ana familia na familia inamtegemea na bodaboda ndiyo kazi yake.

Hivyo wakiwa barabarani wanakuwa wapo makini zaidi kwa sababu anajua nikivunjika mguu miezi mitatu au minne familia yangu itaishi vipi? Watoto wanahitajika kwenda shule na nyumbani kila siku wale na mahitaji mengineyo muhimu. Wanakuwa makini sana.

Au ukimuona kijana ambaye anaendesha kiustaarabu kuna mawili. Mosi, alipata ajali na kunusurika. Pili, hiyo ndiyo kazi inayomwezesha aendesha familia. Hivyo tutarudi palepale kwenye majukumu.

Ila kwa hawa mayanki habari ni tofauti. Yeye anajiona yupo peke yake hivyo inamjengea kujiona yupo huru kwani hana hatia kuona kuna watu wanamtegemea. Umakini kwake unakuwa mdogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…