KITAAOLOJIA: Namna ya kusurvive hapo hapo ulipo, VETA sio suluhisho, pesa ipo hapo hapo ulipo

KITAAOLOJIA: Namna ya kusurvive hapo hapo ulipo, VETA sio suluhisho, pesa ipo hapo hapo ulipo

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
5,315
Reaction score
13,269
Hellow wakuu

Huu ni uzi wa namna ya kujikimu kimaisha kwa mwana JF, Mtanzania sehemu yeyote alipo

Ipo hivi..

Hapo hapo ulipo kuna watu wana njaa ila hawataki kupika, kuna watu wanahamu na makande wanayapenda ila hawana mahindi na mkaa

Kuna wachaga wengi ila hawana pa kujumuikia kupata mbege

Mtaani maji ni ya shida kila mtu analalamika kuyapata mpaka atembee kilometer 8 kuyafuata

Kijiji hakina umeme, watu wanaishi gizani


Hapo hapo ulipo kuna watu wanapenda mpira ila hawana TV

Hapo hapo ulipo kuna watu wanapenda maziwa ila hawajui pakiyapata kiurahisi

Hapo hapo ulipo kuna watu wanapenda pombe ila hawana pesa ya kutosha


Fursa nyingi mtaani zinapatikana kwa kufikiria kwa mtindo huo hapo juu, au kutizama kitu kinacho miss sehemu ulipo watu wengi hukimbilia kufanya jambo kwa kuiga bila kuangalia sehemu alipo kuna kitu gani kina sumbua au kumiss hapo mtaani alipo

Unashangaa mtu anamtaji ila hajui cha kufanya

Mbaya zaidi wengine sasa hivi wanakimbilia VETA kusomea ujuzi wowote bila kujua alipo kuna kitu gani kina miss au kusumbua!


Kuna watu wanataka vitu vya ndani kama vile TV, sofa, vyombo n.k ila hawana pesa za kutosha za kununua vitu vipya n.k

Kuna watu wanapenda kupikia kuni ila hapo walipo hazipatikani


Kama mtu atatumia vizuri mapungufu au kitu kinachosumbua au kumiss hapo alipo basi hataweza kulala njaa


VETA sio suluhisho suluhisho ni kitu gani kinasumbua hapo ulipo


Nawasilisha
 
Back
Top Bottom