Sababu ni rahisi sana, ni rahisi kwa Mkenya ambaye ni jirani yetu kutuhujumu kuliko Mmisri anayetoka mbali kutufanyia hujuma kwa sababu Kenya ni mshindani wetu wa kibiashara; mfano Kenya wanatabia ya kujaza ndugu zao kwenye vitengo vyote, na hii ni kwa sababu wapo karibu na sisi hivyo wanapenyezwa tu. Ila mtu wa Misri ni ngumu kujaza ndugu zake maana kwanza hata muonekano wao ni tofauti na watu watashtuka kuina waarabu wamejazana, ila waKenya ni weusi kama sisi na hakuna atakaeshtuka akiwaona. Kikibwa, Kenya ni mshindani wetu kiuchumi, na lazima tu watatufanyia hujuma kama za General Tyre