Kitendo cha mabeberu kufungasha na ongezeko la utitiri wa kodi

Hii inaashiria vyanzo vya mapato vilivyomo nchini vikilinganishwa na miradi tunayoanzisha nakusimamia vinakinzana.
1. Huu ni ukweli na tatizo liko hapa. Vyanzo vya mapato ni vilevile na wanadhani suluhisho la kupata fedha kwa ajili ya uendeshaji wa nchi/serikali ni kuongeza kodi humohumo kila mwaka na kila wakati badala ya kufukiri juu ya maeneo (vyanzo) vingine ya mapato...

2. The best way ya nchi kuongeza mapato ili kupata fedha za kutosha za kuendesha shughuli za serikali na nchi kwa ujumla ni kuinua na kuilea sekta binafsi (private sector) i - perform hadi kwa kiwango chake cha juu kabisa...

3. Very unfortunately kuwa serikali hii chini ya CCM na Rais wao Magufuli, inachojua yenyewe ni kumkamua ng'ombe tu mpaka atoe damu badala ya maziwa huku wakiwa hawana taimu kabisa kumlisha chakula ili na kesho kutwa waendelee kupata maziwa..

4. Hebu ona tu sasa hivi kinachofanyika. Rais John Pombe Magufuli huku CCM ikimtazama tu bila kumrejesha kwenye mstari anatamani apeleke jeshi (JWTZ) kwenda CHAN kama "TAIFA STARS" ili wakacheze mpira kwa kigezo kuwa hawa raia hawawezi...

Kilichomo kwenye kichwa cha Magufuli ni kutamani serikali imiliki njia zote za uchumi. Anatamani wizara ya madini waanzishe na kumiliki migodi yao. Anatamani turudi miaka 1980 zama za siasa ya ujamaa na kujitegemea kwa serikali kumiliki mpaka biashara za maandazi, Michele, Sabuni na sukari nk nk

Ndiyo maana akaliingiza Jeshi la wananchi (JWTZ) kwenye biashara ya kununua korosho na matokeo yake mission ikafeli spectacularly na ikawa mwendelezo au mwanzo wa nchi kuanza kukosa mapato ya kigeni tokana na mauzo ya korosho nje...

5. Mimi nina hakika kabisa kuwa wataalamu wetu wa uchumi serikalini wanajua kuwa, hii nchi haiendi popote kiuchumi kwa sera hizi za ndugu yetu huyu "Jiwe" ambazo analazimisha zisimamiwe na kutekelezwa hivyo hivyo bila kujali matokeo yake..

Na kwa kuwa anawatishia kuwafukuza kazi na kuwanyima haki zao wanapobishana naye, basi wataalamu hawa wanalazimika kutekeleza hivyo hivyo huku wakijua kabisa nchi inakwenda kutumbukia shimoni kiuchumi...

Ya nini kama mtu hataki ushauri na anataka mambo yafanyike tu atakavyo yeye? Acha kabisa bwana, na sisi tuna watoto na familia eti. Hayo mengine shauri lake yeye na chama chake...!!

6. Kwa mfano, hili la kodi za magari used kupanda maradufu na ili kupata mapato, ndo kusema kuwa, serikali imeji - conspire yenyewe kwa kulazimisha magari yote yakaguliwe hapa hapa nchini wakidhani watapata fedha nyingi, bila kujua kuwa mambo yatakwenda nje ya matarajio kwa 100%...

Na hii maana take no kuwa, kinachokwenda kufanyika ni hiki, kwamba, watu watapunguza spidi ya kununua magari kwa sbb ya bei (gharama kuwa kubwa)...

Na ikiwa hivi, maana yake ni kuwa, aidha kiwango cha mapato kinabaki kilekile kabla ya kupandisha kodi au kushuka kabisa kwa sbb demand imepungua...

Unaweza kuona kuwa, kumbe hii ni mbinu mbovu kabisa ya kiuchumi kutoka kwa watu pengine wasiojua uchumi kabisa...!!
 
Hakuna deni linauma kulipa kama deni ambalo hukusababisha wewe😣😣😣
Acha tu kwa sababu sasa hivi simu zimesajiliwa ni bora wawe wana mpigia mwenye leseni wambambie tunafungia leseni yako au njoo ulipe deni!
 
Hawa wanao kaa maofisini walikuwa wanaona kama wafanyabiashara wote ni wezi. Ila kwa jinsi yanavyoenda tumeshanyooka
 
Jee wanaolipa kodi wana haki ya kuuliza kodi zao zinafanywaje? Mbona tunaona pomp za waku kutembea msafara wa magari 50 halafu unakuja hapa kutuambia pumba. Weee inaonesha wazi hulipi kodi.
Wewe unalipa kodi kiasi gani? Unafikiri rais anatembea na gari moja kama wewe!
 
Weka ushahidi! Majungu peleka kwenye udaku.
 
Mkuu huo mlundiko unaosema ni upi? Kodi zote hizo zipo kwa mujibu wa sheria, unaweza ksema hilo lundo unalolipigia chapuo?
 
Kwani zote zikiwa kwa mujibu wa sheria haziwezi bado kuwa ni mlundikano?
Mkuu huo mlundiko unaosema ni upi? Kodi zote hizo zipo kwa mujibu wa sheria, unaweza ksema hilo lundo unalolipigia chapuo?
 
Kwani zote zikiwa kwa mujibu wa sheria haziwezi bado kuwa ni mlundikano?
Twambie basi huo mlundikano? Mfano double taxation etc. Huwezi kulalamika mlundikano bila kutolea ufafanuzi kuonyesha kwamba kuna kodi hii ambayo haitakiwi au ipo kimakosa etc kutokana na issue hii au ile? Wacha kamba? Usilalamike tu bila kutoa solution ambayo itasaidia kuboresha hizo kodi.
 
Mwaka 2021 umeanza kwa kutangazwa kodi au tozo ambazo awali hazikuwepo. Tumesikia ukaguzi wa magari, garama za kuagiza magari zimepanda mara mia, tozo katika bidhaa nyingi za nje nk.
Hujawahi kuagiza gari ndio Mana unaanzisha thread za kulia Lia
Ukiagiza gari japani,kwenye bei Kuna gharama za ukaguzi,ambazo baadae zinapelekwa Tbs
Tbs wameamua kukusanya wenyewe,ulichokua unalipa japan utalipia Tanzania shida ipo wapi?
 

mihemuko???soma Tena maana wewe ni kilaza ndo uje na upupu wako apa

Ndo tatizo la waafrica.hata tume huru ya uchaguzi mnafikiri ni hisani ya nyinyiemu.mawazo mgando kabisa haha.
 
Mkuu huo mlundiko unaosema ni upi? Kodi zote hizo zipo kwa mujibu wa sheria, unaweza ksema hilo lundo unalolipigia chapuo?
Sheria za kutungwa kila siku kwa ajili ya kuwakamua watu?hata Leo watakuwa wanabuni sheria mpya ya kumnyonya mwananchi,
Ukitaka kujua uhondo wa ngoma ingia ucheze
 
Uendeshaji wa serikali yoyote unategemea kodi. Tatizo kubwa kwetu ni namna ya ukusanyaji wa kodi. Bidhaa au shughuli moja inawekewa kodi nyingi katika hatua mbali mbali, na zingine ni kero na kupoteza muda. Jana nimenunua mkate wa sh 1000 nikaambiwa nisubiri stakabadhi. Ilinichukua zaidi ya dakika 3 kupata hiyo risiti. Hakuna mwenye kujua thamani ya muda katika watunga sera na wanasiasa wetu. Hawana utashi wa kuona ni vipi muda utumike vizuri kwa maendeleo ya nchi.
 
Mkuu huo mlundiko unaosema ni upi? Kodi zote hizo zipo kwa mujibu wa sheria, unaweza ksema hilo lundo unalolipigia chapuo?

Then, tunaweza kusema sasa bila shaka yoyote kuwa, kumbe tatizo linaanzia kwenye sheria yenyewe ya kodi...

Kama sheria yenyewe ya kodi ni mbaya, maana yake hata hicho kilichoko kwa mujibu Wa sheria hiyo hakiwezi kuwa kizuri...!!

Sijui kama utakuwa umeelewa...
 
Hii nchi maajabu hayaishi kamwe,wanaosisitiza wenzao kulipa kodi wao hawalipi mfano Rais ambaye ndiyo Kiongozi wa Nchi halipi Jodi. Je,huyo siyo Mwananchi Mzalendo?
 
Kumbe hujui umuhimu wa wafanya biashara. Wewe mfanyakazi unakatwa 5% ya mshahara wako kwa ajiri ya akiba yako ya uzeeni na serikali inakuongezea 15% , Askari hawakatwi hata centi na uzeeni wanalipwa pensheni. Malipo hayo ni kodi za wafanya biashara ambao hawana pensheni uzeeni na wanakufa wakiwa kazini.
 
Upo sahihi kabisa. Mbali na hao wanaobadirisha biashara, wapo wanao badirisha majina ya umiliki. Tra kila mwaka wanapandisha kodi, bila kujali kama biashara hiyo imepanda. Miaka 10 ndani ya biashara ya kiduka au biashara yoyote ya kawaida, utalipa kodi kumzidi anae anzisha biashara ya jumla mwaka huu.
 

I see...

This means, one can easily predict what is coming next...

Wakimaliza GARAGE na parkings + yards zote, maana yake wataanza kutafuta Magari kwenye majumba ya watu bila kujali ni bovu ama linatembea...

Na wakitoka hapo wataenda hatua inayofuata ambayo ni mbaya na ya hatari zaidi ya kuanza kubambikizia wananchi "road traffic offences" na kisha kuandikiwa "traffic fines" bila mwenye gari kujua alifanya kosa gani na wapi...

Hii tabia imeshaanza Mwanza kwa kasi sana. Kawaulize madereva wa City Commuter buses (hiaces & coaster) jijini Mwanza...

Bahati mbaya sana ni kuwa, hizi fedha haziendi serikalini. Huu ni mradi wa polisi tu kuanzia RPC hadi vijana wake anaowaweka barabarani...!!

Wameona hili ndilo eneo (watu wanaomiliki vyombo vya moto eg Magari, pikipiki nk) ndipo mahali rajisi pa kujipatia fedha kwa urahisi...

Na wasichokujua serikali ni hiki, fedha nyingi inayokusanywa kwa njia hii wala hata haingii kwenye mfuko wa serikali bali inakwenda kwenye mikono ya watu tu (ufisadi/rushwa/wizi)...!!

Kama nchi kupitia serikali, ni muhimu kubuni na kutengeneza mazingira ambayo watu wenyewe watalipa kodi kwa HIARI na KWA MOYO WA KUPENDA...

Hili likifanyika, pesa yote itakuwa inaingia kwenye fuko la serikali na wezi watakosa cha kuiba..

Lakini aina hii ya ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kuviziana na kukimbizana kama paka na panya, is always not friendly and sustainable...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…