Kitendo cha Rais kusimamisha hotuba kisa Adhana ya waislam imakaaje hii kitaifa?

Yesu hajawahi kupambaniwa na mtu! Huyo sio Muhammad mzee! Akisemwa vibaya mnabwatuka! Muhammad alikuja baada ya miaka 600 Kristo alishafanya yake! Ndo akaanza kuototeza vijisentensi kwenye biblia!
Hajui huyo mueleze, yesu alipigwa na watu na juu akatundikwa hakuna raia yeyote aliyempambania
 

Haijakaa chochote. Rais wa Kenya aliwahi kufanya hivyo nadhani hapo hapo Dodoma
 
Umeathirika vipi wewe??? Imani yake inamuelekeza kunyamaza pale anaposkia adhana.

Sawa serikali haina dini ila yeye si anayo dini yake?? Mbona watu mna nongwa sana??

Siyo imani yake tu, Rais Uhuru Kenyatta aliwahi kufanya hivyo hapohapo Dodoma, je muuliza swali alipaswa kuuliza ILIKAAJE!
Kwa ufupi kuna watu ni wadini na wabinafsi sana
 
shule ulizosoma zilikuwa hazina kengele? Walimu wako walikuwa hawana saa za mikononi?…au hukusoma kabisa shule?

Hizo adhana huwa ni kupigiana makelele tu yasiyokua na mpango, kwani kuna asiyejua muda wa kusali?
 
Thailand,
Tatizo kubwa la nchi yetu ni kuwa historia ya ukombozi wa Tanganyika haijawekwa bayana kwa wananchi wote kuifahamu.

Laiti hili lingefanyika Waislam wangeheshimika kwa ajili ya mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kupisha adhana hili ni jambo dogo sana.

Mikutano ya TANU ilikuwa inaanza kwa kusomwa Qur'an pale Mnazi Mmoja kwa kusomwa Surat Fatha msomaji akiwa Sheikh Suleiman Takadir kisha akaomba dua na watu wakiitikia, ''Amin.''

Leo kuna watu wanaghadhibika kwa kitendo kidogo cha kuonyesha heshima na adabu kwa kupisha Adhana wakaona ni jambo kubwa la kulalamikiwa.

Hawa wanajua mchango wa Uislam katika kuwaunganisha watu kupambana na ukoloni na wakimuunga mkono Julius Nyerere kama kiongozi wa Tanganyika nzima?

Hawa wanajua hata jinsi Nyerere alivyofika hapo alipofika kwa msaada mkubwa wa Waislam ambao leo hata kujulikana hawajulikani?

Ndugu zanguni fitna ni kitu kilicholala hapana haja ya kukiamsha.
Angalia picha hizo hapo chini Mwalimu yuko na watu gani?

Hiyo ni mwaka wa 1955 safari ya kwanza ya Mwalimu UNO 1955 na picha ya pili 1957 akiwa na Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Sheikh Suleiman Takadir.

Mbona hamlalamiki kwa nini Mwalimu Nyerere awe kazungukwa na Waislam peke yao nduguze kutoka kanisani walimsusa?

Waislam ni watu waungwana.
Nyinyi hamkuwako wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mama Maria yu hai bado nendeni kwake mkamuulize uungwana, ukarimu na utu wa wazee wetu walivyowapokea yeye na mumewe wakawa bega kwa bega hadi Tanganyika ikapata uhuru wake mwaka wa 1961.


 
Fitna mpaka lini ? Hata angekaa kimya nusu saa kusubiri adhana tatizo ninini ?.Adhana ni mwito wenye heshma sana kwa kila muislam anayeheshimu dini yake na hata wengine ambao siyo waislam walishafanya hivyo kama Rais Uhuru Kenyata.Ndugu zangu nyinyi kila jambo linalofanywa na Muislam akiwa madarakani roho zenu zinakuwa juu juu juu.Jamani Waislam ni binaadam wenzenu na wana haki kama nyinyi.Hamjazuiliwa kukaa kimya au kusimama wakati KENGELE zenu zinawaita kwenda kuabudu.Ni mara ngapi tunaona mpaka majeshini wakubwa kabisa wanatumia fursa wanayoipata kudhihirisha imani zao.ACHENI ROHO CHAFU NA MBAYA.
 
Nampongeza kwa kuheshimu dini, Kama hilo limekukera utakuwa na roho ya nyoka.
 
Shame on you. Hata Mh. Kenyatta alisitisha kwa muda hotuba yake kupisha Azana akiwa Tanzania. Mimi ni Mkristo na niliona ni Sawa kabisa. Leo unamhojije Rais kusitisha? Amefanya vizuri kabisa na msilete mambo ya udini hapa.
 
Duuuh
 

Mtoa Hoja ni mtu mwenye akili ndogo na isiyoona mbali. Asubiri na Waislamu walalamike kwamba nchi hii ilitawaliwa na Wakiristu na hadi leo inaendeshwa Kikristu.

Waislamu watadai siku ya Mapumziko kwao iwe Ijumaa, Wasabato Jumamosi na Wakiristu Jumapili. Waislamu pia watadai Fidia kwa uonevu na ukandamizaji wote waliopata kuanzia Wamisinari kuja na kutawala Kikiristu hadi kuondoka.

Hapa ndiyo suala la Udini litakapoeleweka vizuri
 
kwanza elewa maneno ya Adhana...

Allaahu Akbar – Allah ni Mkubwa kuliko kila kitu.

Ash-hadu An-laa Ilaaha Illal-laah- Ninashuhudia kwamba hapana afaaye kuabudiwa kwa haki ila Allah pekee.

Ash-hadu Anna Muhammadan Rasuulullaah – Ninashuhudia kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah.

Hayya Alas-swalaah – Njooni kuswali.

Hayya Alal-falaah – Njooni kwenye kufaulu.

Asswalaa tu khayrun Minan-nawm – Swala ni bora kuliko usingizi.

Allaahu Akbar – Allah ni Mkubwa kuliko kila kitu.

Laa Ilaaha Illal-laah – Hapana aabudiwaye kwa haki ila Allah.



(1) Tarji’i ni kuyarudia tena matamko hayo kwa sauti ya chini kidogo.
 
Adhana inaheshimiwa dunia nzima, tazama hata huyu muabudu ng'ombe, waziri mkuu wa India, amesitisha hotuba yake alipoisikia adhana, itakuwa Muislam? Fikiri japo kidogo: PM Modi halts his victory speech in between for Azaan
 
Huyu mzee kaanza mambo yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…