Thailand,
Tatizo kubwa la nchi yetu ni kuwa historia ya ukombozi wa Tanganyika haijawekwa bayana kwa wananchi wote kuifahamu.
Laiti hili lingefanyika Waislam wangeheshimika kwa ajili ya mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Kupisha adhana hili ni jambo dogo sana.
Mikutano ya TANU ilikuwa inaanza kwa kusomwa Qur'an pale Mnazi Mmoja kwa kusomwa Surat Fatha msomaji akiwa Sheikh Suleiman Takadir kisha akaomba dua na watu wakiitikia, ''Amin.''
Leo kuna watu wanaghadhibika kwa kitendo kidogo cha kuonyesha heshima na adabu kwa kupisha Adhana wakaona ni jambo kubwa la kulalamikiwa.
Hawa wanajua mchango wa Uislam katika kuwaunganisha watu kupambana na ukoloni na wakimuunga mkono Julius Nyerere kama kiongozi wa Tanganyika nzima?
Hawa wanajua hata jinsi Nyerere alivyofika hapo alipofika kwa msaada mkubwa wa Waislam ambao leo hata kujulikana hawajulikani?
Ndugu zanguni fitna ni kitu kilicholala hapana haja ya kukiamsha.
Angalia picha hizo hapo chini Mwalimu yuko na watu gani?
Hiyo ni mwaka wa 1955 safari ya kwanza ya Mwalimu UNO 1955 na picha ya pili 1957 akiwa na Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Sheikh Suleiman Takadir.
Mbona hamlalamiki kwa nini Mwalimu Nyerere awe kazungukwa na Waislam peke yao nduguze kutoka kanisani walimsusa?
Waislam ni watu waungwana.
Nyinyi hamkuwako wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mama Maria yu hai bado nendeni kwake mkamuulize uungwana, ukarimu na utu wa wazee wetu walivyowapokea yeye na mumewe wakawa bega kwa bega hadi Tanganyika ikapata uhuru wake mwaka wa 1961.
View attachment 2207927
View attachment 2207931