Huyu mzee kaanza mambo yake
Babu...
Huwa mara nyingi nasoma huu utambulisho wangu wa ''mzee.''
Hakika mimi ni mzee.
Mwezi Februari nimefikisha miaka 70.
Lakini hapa hoja si umri wangu.
Kunitambulisha kwa ,''Huyu mzee,'' wewe unadhani unanikebehi na kunifanyia kejeli.
Mimi sihamaki kwa kuitwa mzee.
Nikifanya hivyo nitakuwa mpuuzi kwani kuishi hadi unafikia uzeeni ni jambo la kushukuru vinginevyo Allah angenichukua kijana na nisingefika umri huu wa uzee.
Nilikuwa kijana na kijana khasa.
Alhamdulilah pengine wewe hujapitia hata kwa mbali ujana niliopitia mimi.
Tuje sasa kwenye maudhui.
Nimeeleza kuwa huu Uislam unaokughadhibisha wewe hii leo kwa kusikia Adhana ndiyo ilikuwa silaha iliyomtoa mkoloni Tanganyika.
Ilikuwa kila tatizo lililokumba harakati za kudai uhuru TANU ilikuwa ikirejea kwa Allah kutafuta msaada.
Nyerere kafariki akilijua hili na akishiriki kwa kila dua iliyofanywa.
Kuna dua aliyofanyiwa Rashid Ali Meli 1955.
Rashid Ali Meli alitoa fedha za Dar es Salaam Municipal Council (DMC) kuwakopesha TANU ili Nyerere awahi safari ya kwanza UNO 1955.
Rashid Ali Meli alikuwa Bwana Fedha wa DMC.
Historia ya Ali Meli iko hapa JF fanya search utaiona.
Kuna dua aliyofanyiwa Abdul Sykes 1955.
Abdul Sykes alishutumiwa kwa kutumia ofisi yake ya Market Master Kariakoo Market kuuza kadi za TANU.
Kisa hiki kipo hapa JF fanya search.
Kuna dua alifanyiwa Nyerere Lindi na Sheikh Yusuf Badi 1956.
Kisa kipo hapa kitafute.
Kuna dua aliyofanyiwa Nyerere Mnyanjani, Tanga 1958.
TANU ilikuwa imezongwa na tatizo la Kura Tatu.
Kisa kipo hapa JF.
Yote haya yakifanywa na Waislam ndani ya TANU na Wakristo hawakulalamika kwa nini Waislam wanamtukuza Mungu katika kutafuta uhuru?
Haya ndiyo mimi nakuomba utoe majibu.
Haya ndiyo mapenzi yaliyokuwapo nchini petu.
Tusiuvuruge udugu huu kwa chokochoko.
Historia hii ingesomeshwa na ikafahamika watu kama wewe wangeelimika.
Mtaa wa Muhammad Yusuf Badi Lindi