Kitendo cha Rais kusimamisha hotuba kisa Adhana ya waislam imakaaje hii kitaifa?

Kitendo cha Rais kusimamisha hotuba kisa Adhana ya waislam imakaaje hii kitaifa?

ishu inatakiwa iwe inatokea kwa dharula ya mara moja moja ila kwasasa imekuwa destuli hotuba inapangwa isomwe kwa maksudi kipindi ambacho wanajua kabisa itaangukia kwenye adhana. hii imejitokeaza kwa mara ya pili
 
Leo tarehe 1/5/2022 Rais akiwa anawahutubia wafanyakazi Dodoma katika siku muhimu ya wafanyakazi duniani, ilitokea kusitishwa hotuba Kwa dk kama 3 na Rais pale Adhana ya mchana ilipokuwa ikisika kutokea msikitini karibu na uwanja wa Dodoma.

Hivi wadau wa utaifa hili lilipaswa kufanywa na Rais kiongozi mkuu wa Serikali ambaye tuna amini anaongoza SERIKALI ISIYO NA DINI?

Wananchi wakristo inabidi tuendelee kuvumilia tu kama msingi wa dini yetu.
Ungekuwa muungwana ungempongeza sana Mh. Rais kwa utu wake na ucha Mungu huo, nakumbuka the same applies kwa Mh. Rais Uhuru Kenyatta wakati akitoa Salamu za Rambirambi wakati wa maziko ya Hayati Magufuli.

Wengi walimpongeza sana kwa uungwana huo, leo mwenzetu unaponda? Kweli binadamu hatuna jema!!
 
Mambo ya ajabu sana
Mleta mada anahoja ajibiwe kwa hoja. Acheni kumshambulia. Kwanini mnamfunga mdomo why? why? why?. Nyie wote mnaomshambulia hamna tofauti na Ndugai aliyewashambulia wapinzani.
#We're not the same.
 
Tujitahidi kujadili masuala yenye tija kwa taifa - kama uchumi na biashara, amani na umoja wa kitaifa, haki, demokrasia na uhuru wa kutoa maoni, na masuala kama hayo. Rais kama muumini wa dini ya kiislamu na kama kiongozi mkuu wa taifa letu amefanya uamuzi wa busara kusimamisha hotuba yake kwa muda.
JF ya miaka hii ni tofauti kabisa na ya miaka ya 2005. Sasa hivi imevamiwa
 
Hizo adhana huwa ni kupigiana makelele tu yasiyokua na mpango, kwani kuna asiyejua muda wa kusali?
Mbona makanisani kengele huwa zinagongwa kushtua waumini kuwa muda wa kusali umefika? What is wrong?
 
Leo tarehe 1/5/2022 rais akiwa anawahutubia wafanyakazi Dodoma katika siku muhimu ya wafanyakazi duniani, ilitokea kusitishwa hotuba Kwa dk kama 3 na rais pale Adhana ya mchana ilipokuwa ikisika kutokea msikitini karibu na uwanja wa Dodoma.
Hivi wadau wa utaifa hili lilipaswa kufanywa na rais kiongozi mkuu wa serikali ambaye tuna amini anaongoza SERIKALI ISIYO NA DINI?
Wananchi wakristo inabidi tuendelee kuvumilia tu kama msingi wa dini y

Bora angesimamisha hata nusu saa tumsikie Mungu kuliko ahadi zisizotekelezeka.
Makanisa na misikiti ziheshimu privacy za watu. Si jambo la busara unasali wewe unawapigia kelele wengine. Sisi wengine hatuna na wala hatuamini kwa hayo mliyoletewa na wazungu na waarabu. Ebu acheni mambo ya udini hayo, hayatusaidi katika maisha yetu, kama unasali, omba kwa Mungu wako katika sehemu za usiri na zisizo na kelele. Hiyo adhana ya kuitana kwenda kusali au kupiga kengele kwa makanisa ni suala lililopitwa na muda, kwani ukiambiwa sala au swala inaanza saa sita huna saa hadi uitwe na muadhana? au ukijua misa au ibada inaanza saa nne, saa sita na saa nane, huwezi ku-keep time usichelewe swala/sala? Mbona kwenye mabaa na mkisafiri mnawahi sana, sasa leo mnaona shida kuwahi kwenye ibada. Huo mnaosema ni ujinga tena mkubwa na inaonyesha ni primitiveness. Acheni kujipendekeza kwa cheap popularity.
 
Hawa ndo wanafanya wakristo wengine tuonekane wapuuzi,kwa hiyo ulitaka aendelee ???
 
Alichokifanya Rais Samia inaweza ikawa ni sahihi kwa kuwa amefuata misingi ya dini yake.
Ila kwa tukio kama ili haikuwa sawa kufanywa na Rais Uhuru, maana alitumia busara tu japo ni kwa kitu kisichomhusu yeye na dini yake.

Pia hoja nyingine ni kuwa Serekali haina Dini. Hivyo ukiwa kwenye majukumu ya kiserekali sio budi kujihusisha na mambo ya taratibu za dini.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji51][emoji849]Dini hiyo hiyo inasema mwanamama hatakiwi kuwa kiongozi mwenye mamlaka ya juu kabisa ila anaweza kuwa kiongozi wa chini chini tu what a shame.
Shame kwako wewe
 
Kuheshimu dini ya mtu ata kama ukiwa huna dini au mnautofauti si kosa. Huwezi nyanyuka ukiwa na akili zako timamu ukaenda kula kitimoto mazingira ya msikitini kisa huko huru kufanya hivyo hapana.
Yeye ataheshimu dini yako inayoruhusu kula kiti Moto. Wanawaua nguruwe ukifuga karibu nao hata Kama wamekukuta unafuga wao wakiwa wageni
 
Back
Top Bottom