Kitu gani kilikushangaza mara baada ya kuingia kwenye ndoa?

Kitu gani kilikushangaza mara baada ya kuingia kwenye ndoa?

I thought I'd be eating papa daily, kumbe ni kujidanganya tu, saivi hata wiki mbili zinakata na wala sioni shida.

I thought it was a bed of roses, kwamba maisha ni mteremko tu kila unachotaka kinapatikana kwa urahisi tu, kumbeeeee!

Kwamba kila siku ni raha tu humo ndani, nilijidanganya sana. Ups na downs ni za kutosha.

Thank goodness, tunaishi na Mungu anazidi kuzibariki ndoa zetu.
Hii comment inatia Moyo ... Barikiwa
 
Mimi nilishangaa kuona cheti cha ndoa kimeandikwa jamhuri ya muungano wa tanzania
wakati niliamini kwa kuwa ni ndoa ya kikristo nitapewa cheti cha kanisa ninalosali.
Kimeandikwa hivyo kutokana na changamoto za kisheria zitakazojitokesha mbele ya safari.......
😃😃😃😃😃😃😃😃😃😃
 
Habari za muda huu wanajamii,

Wahenga wanasema usilolijua ni usiku wa giza, kila mmoja wetu anapotarajia kupata jambo jipya au kuingia kwenye maisha mapya hujawa na shauku na mshawasha.

Ndoa ni taasisi ambayo kabla hujaingia unakuwa na matarajio makubwa yaliyojaa furaha kutokana na jinsi unavyompenda mwenza wako lakini wakati mwingine mambo huwa tofauti na vile ulivyofikiria yanaweza kuwa hasi au chanya.

Je ulipatwa na mshangao gani mkubwa baada ya kuingia kwenye ndoa?

Unaweza uka share na kuwa funzo kwa wengine ambao ni watarajiwa.
tulioana kijeshi maana alikuja akakaa wiki hlf akapotea.
kumbe alienda kwao.
alivyorudi akaja na vitu vyake vingi. ile mara ya kwanza vilikuwa vichache. apo kumbuka hatujaoana.
ule mwezi haukuisha tukawapokea wadogo zake 2 na mamkwe.
Leo apa naandika imeshapita miaka 5. apo kumbuka hatujaoana.
ivi ulisema wenye ndoa ndo wasimulie?
 
Back
Top Bottom