Kitu gani umewahi kuona ukaamini uchawi upo?

Bibi yangu wa mwisho ni wale wabibi waliolewa na wasomi nae anajiona msomi. Msafi sana kwake kuna mkungu basi ukifika kutwa kuokota majani km yuko hotelini.
Sasa pale kwake kuna uwa/fensi alivyoka ndani akamuona jongoo huyu huyu jangoo mweusi mkubwaaa. Akachukua banio la moto na kumbana ili mrushe nje eeenh bwana weeee alimkamata vizuri alivyoanza kumbana ili mrushe nje akashtukia mguu unavunjika, kila akikazana na mfupa nao unavunjika. Yaani unaliaa teh teh teh akafanikiwa kumdodosha lakaini bibi hakuweza teena kutembea tena. Mguu ulivunjika mara kadhaa alilazwa St fransis akawekewa hogo. Mpaka kesho bibi anatembelea magongo. Yule jongoo alizolewa tuu akawekwa nje aendelee na safari yake mwanaharamu yule.
 
🤣🤣🤣🤣Yaani hizi story hata mtoto wa la pili hawezi amini
 
[emoji24][emoji24][emoji24]Aisee nimeguswa sana na hbr hii.Kumbe ajali nyingi ni kiini macho.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 

Mkuu ikiona ivo marehemu anakutokea tokea jua hakikua kifo cha kawaida icho
 
Walimpoteza mdogo wangu mara 3 siku waliompoteza mara ya 3 walimrudisha uchi Hadi leo nguo zake hatujazipata na akili ya kusoma ikapotea kabisa pia sitosahau siku nilipoiona meli imetia nanga uwanja wa mpira usiku Zanzibar nao hawajambo
Pole,mdogo wangu walimpoteza mara moja kipindi yupo darasa la tano, shule akienda mauzauza,kuzimia, yaani family haina amani kwaajili yake,

Kwasasa tunamshukuru Mungu yupo vizuri na anasoma kidato cha kwanza.

Sent from my itel W5002 using JamiiForums mobile app
 
Nilikuwa nasafiri usiku kama saa 9 hivi na Lori niko peke yangu.
Nilipofika maeneo ya michungwani Tanga nikamuona binti mzuri kiasi anasimamisha gari.
Niliamua kutosimama lakini baada ya kufika kwedikwazu nikamuona binti yule yule na ghafla gari ikaanza kukosa nguvu na hatimae ikazima.
Binti akawa analisogelea gari....Sasa huo ni uchawi au ujini????
 
Hilo ni Jini mkuu

Ila hujamalizia stori yako
 
Aisee kuna mpuuzi aliapa kukutoa roho. Ila Mungu alikuwa upande wako
 
Mkuu ikiona ivo marehemu anakutokea tokea jua hakikua kifo cha kawaida icho
Hamna kitu Kama kutokewa na marehemu hivi vitu ni hallucinations tu...mbona watu wenye akili timamu na wenye maisha mazuri hawatokewi na hivi vitu. Elimu tu ndo itakukomboa, hivi vitu ni biology sio kila kitu unachokiona ni Cha ukweli ndo maana unaota ndoto. Ubongo una nguvu kubwa na unaweza kukudanganya vingi, kadri jamii inavyozidi kuwa maskini ndo jinsi inavyozidi kuwa ya kishirikina kutokana na ukosefu wa elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…