Malezi ya kulea watoto kwapani siwafichi ndugu zangu ndio yanayosababisha kuwe na ongezeko kubwa sana la mashoga siku hizi,hizi tabia za kufumbia macho kila wanachofanya kina Junia ipo siku huko mbeleni tutakuja kujuta..Hii nimewachana jana tu kwenye basi wakati natoka Dodoma kwenda Dar kuna vitoto viwili vilikuwa na wazazi wao basi walikuwa hawatulii kelele wao,mara wapande juu ya siti gari ikiwa mwendo kasi,mara wavute nywele wakubwa halafu wazazi wao wanawaangalia tu nilikaa siti tatu kwa nyuma kutoka kwao si ndio mmoja akajitela bwana kujifanya kuja kwangu ananiuliza maswali kuhusu screen zile zilizopo kwenye siti za Shabiby nikawa namjibu fresh tu huku nikichukua tahadhari maana niligundua ni mtundu,eh!!! si akabonyeza ghafla kitufe kimojawapo cha cha screen nikamsukumia ghafla kuelekea uelekeo wa wazazi wao na mineno juu watu wakaniunga mkono "hawa watoto watundu kweli" hapo ndipo nikaanza kupiga madongo kuhusu malezi ya watoto wazazi wao wakisikia..Sema niligundua hata mzazi wake wa kike pia hana malezi mazuri maana mtu mwenye malezi mazuri hawezi kula hovyohovyo alikuwa na rundo la mivyakula mara miwa,zabibu,mayai,tambi,biscuti,juice,sambusa na vyote alikuwa anakula kwa wakati mmoja