Kituko gani alikufanyia mtoto wa mwenyeji wako ulipokuwa ugenini huwezi kukisahau hadi leo hii?

Kituko gani alikufanyia mtoto wa mwenyeji wako ulipokuwa ugenini huwezi kukisahau hadi leo hii?

Mwaka flani wageni walikuja nyumbani mtoto akamuomba mama ake simu acheze game mama yake akamwambi imezima chaji na hapakuwa na umeme toka asubuhi

Mama wa huyo mtoto akanambia mpe Basi simu yako acheze game maana ataanza sumbua hapa..nikamjibu haina ilioko ni ya kutumia akili sana sio game last kitoto ..mama yake akasema kuliko Alie we mpe ashindwe[emoji848]

Au mpe a download anajua kutafuta game zake...nikamjibu mwache Alie hii sio PS

[emoji23]
 
Nilienda kwa kaka yangu wa tumbo moja.
Nipo sebuleni naangalia TV, mtoto wa bro alitoka shule. Alipofika hata hakunisalimia.
Kakasimama katika ya TV, nikamwambia toka hapo, bado tu. Nikamwambia tena. Kakazima TV kakaingia chumbani.
Nikawasha, nikasubiri kanatoka chumban. Nikakashika, nikakapa kifinyo.
Usiku bro anakuja, kanamwambia. Nimempiga. Bro akasema, huyu akileta ujinga piga.
Wazazi wa sasa, jitahidini kuwalewa watoto wenu katika tabia njema ndiyo maana hata ndoa za siku hizi zinavunjika kwa sababu ya malezi.
Namshukuru sana mama yangu, ametulea katika maadili mema. Sisi nyumbani ukimkuta mgeni lazima umsalimie halafu unaenda kucheza nje. Mgeni aletewe hata soda halafu nawe unataka unywe naye kipigo utakachopata.
Yaani kama ulikafinya,hio safiiii mtoto mdg ahui hata maisha hio tv ajui hata bei yake...

Broo wako, nae ni mtuuuu ataki ujinga
 


Umenikumbusha hii story ya mwamba..........😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆😆
 
Nikiona Mtoto anaedeka au mtundu mtundu hua najitenga nae mbali maana najua sitakawia kumbonda. Nawachukia watoto watundu na mideko, Sikulelewa kimideko so napenda na watoto wengine wawe hivo.

Siku moja nilijisahau nikampa maji Mgeni nikiwa nimesimama baada ya hapo nilikula kichapo sana. Baada ya ya hapo mpaka leo hii na ndevu zangu kama nampa kitu mtu mzima lazima nifanye kama napiga goti moja. Kama ni baba nampa kitu lazima nipige magoti...mwili ushazoea wenyewe unajua nini ufanye nikimpa kitu mtu.
Kumbe wewe ni wa kike..!
 
Nilienda kutembelea ndugu jijini dar es salaam sasa katoto ka sister kakaja tukawa tunapakua msosi nilivyomaliza kukapakulia.nikajipakulia na mimi wacha kashtuke eti khee njomba unakula sana naenda kusema kwa mama😂😂😂😂😂
 
Malezi ya kulea watoto kwapani siwafichi ndugu zangu ndio yanayosababisha kuwe na ongezeko kubwa sana la mashoga siku hizi,hizi tabia za kufumbia macho kila wanachofanya kina Junia ipo siku huko mbeleni tutakuja kujuta..Hii nimewachana jana tu kwenye basi wakati natoka Dodoma kwenda Dar kuna vitoto viwili vilikuwa na wazazi wao basi walikuwa hawatulii kelele wao,mara wapande juu ya siti gari ikiwa mwendo kasi,mara wavute nywele wakubwa halafu wazazi wao wanawaangalia tu nilikaa siti tatu kwa nyuma kutoka kwao si ndio mmoja akajitela bwana kujifanya kuja kwangu ananiuliza maswali kuhusu screen zile zilizopo kwenye siti za Shabiby nikawa namjibu fresh tu huku nikichukua tahadhari maana niligundua ni mtundu,eh!!! si akabonyeza ghafla kitufe kimojawapo cha cha screen nikamsukumia ghafla kuelekea uelekeo wa wazazi wao na mineno juu watu wakaniunga mkono "hawa watoto watundu kweli" hapo ndipo nikaanza kupiga madongo kuhusu malezi ya watoto wazazi wao wakisikia..Sema niligundua hata mzazi wake wa kike pia hana malezi mazuri maana mtu mwenye malezi mazuri hawezi kula hovyohovyo alikuwa na rundo la mivyakula mara miwa,zabibu,mayai,tambi,biscuti,juice,sambusa na vyote alikuwa anakula kwa wakati mmoja
Hapo likipigwa bomu linaua basi zima kwa mchanganyiko huo.
 
Kwa aunt analmtoto 5years wa kiume,yaani anawasha gesi inshot ana mambo ya hatari sana,muharibifu,binti wa kazi anakoma,

Nilikuwa zangu jikoni nimepika nikatoka,nikasimama dinning natizama nje,

Yule mtoto sijui alipita muda gani kuelekea jikoni,nashtuka nimebandikwa na kisu cha moto mkononi aisee nilitamani ardhi ipasuke,,,,,alidundwa na mama yake na Mungu akamlaani siku ya pili alikuwa anachezea moto wa mkaa akaukanyaga kwa miguu yote miwili,aliungua vibaya sana,

Siku naondoka kananiambia usiondoke mie nitabaki na nani,aunt nikikumisi utakuja kuniona huku kanalia,

Sijaendaga tena,wanaishia tu kuniambia utakuja lini,

Maana aunt analalamika adumu na wasichana wa kazi,,nikagundua shida ni tabia za mwanae maana mwenyewe yupo poa tu

nahisi inasababishwa pia na malezi ya mama pekee
 
Kuna kale katabia nadhani asilimia kubwa tulikuaga nako utotoni home kipindi hicho wakipika wali unachukia kinyama kwanini mgeni kaja atamaliza wali wenu [emoji16][emoji16][emoji16] pia kuna baadhi ya wamama nishawachora wengi mgeni akija hasa mda wakuandaa wali mezani

Hamli hadi mgeni asepe zake [emoji16][emoji16][emoji23] daaahh!! Noma jamani nikikumbuka nacheka kinyama...

Au mfano unacheza na mtoto mwenzio kwao wakapika ugari kwenu wali kama huwa mnatabia ya kila mmoja kwenda kula kwa mwenzake akikuzingua tu unamchimba biti "usije kwetu kula"[emoji16][emoji16]

Nakumbuka siku moja kwa uroho wangu nilienda kula nyumba moja hivi jirani na kwetu walipika wali na ndondo ukicheki home kuna nguna baada ya kumaliza michezo na wale watoto wa ile nyumba si wakanikalibisha njoo ule bana...

Basi mara ya kwanza nikagoma mara pili nikasogea japo kwa uoga maana bibi wa watoto wa ile nyumba alikuwaga mchawi na bi mkubwa alishanipiga stop kula kwa watu especially ile nyumba.

We sinikafwatwa na dada wa kazi wakanitetea kwamba nimalize kula ntaenda yeye arudi tu nilivomaliza kula narudi home sitosahau nichezea stickkkk![emoji16][emoji16][emoji23] tangu siku hiyo sijawahi tena kula kwa watu.
 
Ila haya malezi ya sasa haki vile wengI wetu tutakuja kujibu mbele za Mungu.
Na wengi tunaojikosha hapa ukute ndo sisi sisi tunawalea akina junya huko nyumban sema tu ni vile hatujuani

Mungu aturehemu kiukweli
Mkuu we acha tu, kuna anti yangu mmoja ni kauzu kwelikweli kwa sisi wengine ila watoto wake anavyowalea ni kichefuchefu
 
Sasa na weye unaendaga kula kwa watu ili iweje?
Hujui kama mafuta yamepanda bei?
Sometimes baadhi ya wazazi humtuma mtoto akaropoke maneno kwa mgeni ili ajiongeze maisha magumu mjini[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hili swali lilinishangaza maana sijawahi kula kwenye huo mji.
 
Back
Top Bottom