AMO sio Daktari, ni Daktari msaidizi, na hicho cheo kipo Bongo tu, ila taaluma yao inayotambulika kimataifa ni ile ya U Clinical Officer.
Narudia tena, akitaka udaktari, anaenda kuanza MD 5 yrs, kisha Internship.
Hakuna Equivalency hapo. Na MD si Bachelor's degree tu, ni muunganiko wa Bachelor of Medicine&Bachelor of Surgery, kule Makerere huitwa MBChB, na huku huitwa Degree of Doctor of Medicine(MD).
Na vigezo vya uchaguzi wa RMO, vinasema awe MD(mwenye MPH na uzoefu wa UDMO miaka 7), na hawasemi MD au AMO au Nurse, ila ni MD tu. MPH yeyote aweza soma, ht wenye B. A. Ed wanafanya MPH!
Sasa iweje apewe AMO mwenye MPH na uzoefu, wkt kuna MD wenye MPH na uzoefu wa u DMO?
Vigezo na masharti lzm kuzingatiwa, msitetee uvunjaji kanuni na taratibu, kwa vile tu mna chuki na MD, hivyo ht penye ukweli mnafumba macho.
Wambieni wabadilisha vigezo, waseme RMO anaweza kuwa MD au AMO plus vigezo vingne. Hamtaona mtu analalamika hapa.