Kiuhalisia manunuzi yote ya serikali nje ya nchi hayatumii hata senti moja ya kodi zetu

Sekta ya utalii inaleta fedha ya kigeni, wao katika uendeshaji wanatumia sarafu ipi, na wanazipataje? Sekta ya madini inaleta fedha ya kigeni lakini katika uendeshaji wa ndani wanatumia sarafu ya ndani, je wanaipataje? Sekta ya mafuta inatumia fedha za kigeni na haizalishi fedha za kigeni, ile hasara ya fedha za kigeni inabebwa na nani? Nb. Kuwepo na sheli nyingi ni hasara kwa serikali, kwa sababu mafuta mengi yatanunuliwa kwa fedha za kigeni huku hiyo sekta ikiwa haizalishi fedha za kigeni.​
 
Tuseme serikali inataka kununua v8 500, malipo yote yatafanyika kwa dola na sio tsh, na ili kuipata hio dola ni lazima uuze nje hakuna sehem ingine duniani unaweza kubadilisha tsh na dola zaidi ya nchini tu
Hiyo serekali inazalisha nini hicho inachokiuza nje?
 
swali zuri sana: fedha za kigeni nyingi zinazotokana na shughuli za kiuchumi znatumika kwa ajili ya kulipa madeni ya nyuma ya nchi haswa ya miaka ya nyuma ambayo interest zake zimeshamature!
 
Na hizo fedha zinazotolewa zitalipwa na vyanzo vipi vya mapato kama mdhamini mkuu wa hiyo mikopo?
swali zuri sana: fedha za kigeni nyingi zinazotokana na shughuli za kiuchumi znatumika kwa ajili ya kulipa madeni ya nyuma ya nchi haswa ya miaka ya nyuma ambayo interest zake zimeshamature!
 
swali zuri sana: fedha za kigeni nyingi zinazotokana na shughuli za kiuchumi znatumika kwa ajili ya kulipa madeni ya nyuma ya nchi haswa ya miaka ya nyuma ambayo interest zake zimeshamature!
Hizo shughuli za kiuchumi zinaendeshwa kwa sarafu ipi na zinatoka wapi?
 
Hiyo serekali inazalisha nini hicho inachokiuza nje?
asilimia 80% ya miamala ya nje inafanyika kwa mikopo kutoka kwa washarika kwa mfano IMF, WORLD BANK however inakuja kutokana na matakwa yao, kwa mfano kunaa maamuzi serikali haiiwezi kufanya kwa sababu ya kuepuka kukosa hivi vigezo kwa mfano haki za binadam, mambo ya democracy na kdh
 
Mdhamini ya hiyo mikopo ni kodi za wananchi bwashee
 
Tuseme serikali inataka kununua v8 500, malipo yote yatafanyika kwa dola na sio tsh, na ili kuipata hio dola ni lazima uuze nje hakuna sehem ingine duniani unaweza kubadilisha tsh na dola zaidi ya nchini tu
Akiba ya Dola ya taifa ni mali ya wananchi ila zinasimamiwa na Benki Kuu kwa niaba ya nchi. Chanzo cha dola hizo ni mauzo ya nje kama dhahabu pamba kahawa na korosho kama ulivodai mapato kutoka kwa watalii mikopo ya kigeni, pamoja na uwekezaji kutoka nje. Kwa kuwa maliasili zinazouzwa ni mali ya wananchi, na hata mikopo ya kigeni hutakiwa kulipwa kwa kodi za wananchi maana yake kila dola inayoingia nchini ni matokeo ya nguvu za wananchi na rasilimali zao. Dola hizo zikifika, huhifadhiwa katika akiba ya taifa foreign reserves na hutumika kulipia uagizaji wa bidhaa muhimu kama mafuta dawa na mitambo. Kwa hiyo, serikali si mmiliki wa hizo dola bali ni msimamizi. Tatizo linatokea pale dola zinapotumika kwa matumizi yasiyo na tija, mfano magari ya kifahari kwani mwisho wa siku gharama zinawarudia wananchi kupitia mfumuko wa bei na upungufu wa akiba ya taifa. Lakini zikielekezwa kwenye maendeleo ya moja kwa moja, faida zake huwanufaisha wananchi wote.
 
Safi
 
mauzo yote ya nje hutumika kulipa madeni ya nyuma, hata ivo benki kuu hubeba kiasi kidogo sana cha mapato ya nje kwa ajili ya manunuzi ya mwananchi mmoja mmoja
 
Hiyo serekali inazalisha bidhaa gani inazouza nje ili upate hizo dola za kulipa madeni ( umesema kodi zetu hazitumiki kulipa?)...... Ndoa swali langu hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…