Pre GE2025 Kiukweli 2025 simuoni Rais Samia akishinda kwenye Boksi la kura kama upinzani wakiweka mtu mahiri

Pre GE2025 Kiukweli 2025 simuoni Rais Samia akishinda kwenye Boksi la kura kama upinzani wakiweka mtu mahiri

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Habari za usiku wakuu!

Licha ya kuwa Mhe. Rais anajitahidi kwa uwezo wake wote kutoa mchango wake katika kuipa nchi maendeleo lakini bado mwitikio kwa wananchi ni mdogo sana. Bado hajapata nguvu kwa wananchi waliowengi.

Najua wapo wapambe ambao wataukataa huu ukweli kwa manufaa wanayoyajua wao wenyewe. Lakiñi huku mtaani ni dhahiri kuwa Nyota ya Mama bado ipo chini. Hakubaliki.

NI vile upinzani nao upo legelege, haueleweki lakini acha tuone mpaka mwakani huenda mambo yakabadilika.

Akitokea mpinzani mzuri hasa anayetokea Bara nina hakika Samia atakuwa kwenye wakati mgumu kutetea kiti chake kwa njia halali.
Sijui kwa upande wa figisufigisu.

Kingine, Rais Samia kwenye kuongea hasa wakati wa kampeni sina hakika atazungumza kwa namna ipi ili kushawishi wananchi.

Maana uoñgeaji wake haupo kwa namna ya kushawishi. Anawéza akawa anaelezea vizuri lakini sio kueleza katika kiwango cha kumshawishi mtu kitu ambacho kwenye siasa ni kikubwa.

Binafsi nasubiri kwa hamu panapo majaliwa nione hizo kampeni.

Acha nipumzike sasa
Ndio maana Samia ameagiza pikipiki 18,000 kwaajili ya kampeni kwani hata yeye mwenyewe hajiamini.
 
Sasa unadhani Mama Samia alifika hizo ngazi za juu kimiujiza? Hadi mtu awe waziri ina maana lazima awe mbunge kwa mujibu wa katiba. Unajua shughuli ya mwanamke kuupata ubunge wa kuchaguliwa hasa huko visiwani? Ungetafuta kwanza wasifu wa Mama Samia kabla ya kuandika. Umeandika kwa hisia zako tu.

..Mama Abdul tayari ni Rais hivyo uwezo wake na mapungufu yake ni mambo yanayojulikana.

..Kwa maoni yangu Mama amebebwa na mfumo wa Ccm. Mama sio mahiri, wala mpambanaji, na angekuwa ktk chama cha upinzani huku Tanganyika hakuna mtu angemfahamu.

..Wanasiasa wengi wa Ccm hawana uwezo lakini wanafanikiwa kisiasa kwa kupata msaada mkubwa wa dola.

..Mama Abduli atakuwa na wakati mgumu ikiwa atapambanishwa mgombea wa upinzani mwenye fedha na rasilimali za kufanya kampeni nchi nzima.
 
Wenye imani na Mungu japo hata kiduchu tu muwe mnakumbuka kwamba kuiba kura ni dhuluma kama Dhulma nyingine yeyote ile !

Tena huenda hiyo Dhulma ikawa ni kubwa zaidi kuliko ya kuiba mali nyingine kwa sababu kwenye kura utakuwa umewaibia haki zao watu wengi !!
Msiseme mlikuwa hamjui
Sasa mumeshajulishwa 🙄😳👍
Kazi kwenu ! Maisha ni mapito tu 🫀😱
 
Habari za usiku wakuu!

Licha ya kuwa Mhe. Rais anajitahidi kwa uwezo wake wote kutoa mchango wake katika kuipa nchi maendeleo lakini bado mwitikio kwa wananchi ni mdogo sana. Bado hajapata nguvu kwa wananchi waliowengi.

Najua wapo wapambe ambao wataukataa huu ukweli kwa manufaa wanayoyajua wao wenyewe. Lakiñi huku mtaani ni dhahiri kuwa Nyota ya Mama bado ipo chini. Hakubaliki.

NI vile upinzani nao upo legelege, haueleweki lakini acha tuone mpaka mwakani huenda mambo yakabadilika.

Akitokea mpinzani mzuri hasa anayetokea Bara nina hakika Samia atakuwa kwenye wakati mgumu kutetea kiti chake kwa njia halali.
Sijui kwa upande wa figisufigisu.

Kingine, Rais Samia kwenye kuongea hasa wakati wa kampeni sina hakika atazungumza kwa namna ipi ili kushawishi wananchi.

Maana uoñgeaji wake haupo kwa namna ya kushawishi. Anawéza akawa anaelezea vizuri lakini sio kueleza katika kiwango cha kumshawishi mtu kitu ambacho kwenye siasa ni kikubwa.

Binafsi nasubiri kwa hamu panapo majaliwa nione hizo kampeni.

Acha nipumzike sasa
In shaa Allah tukiwa hai, atashinda kwa kishindo.
 
Kushinda ??! Au
Kutangazwa ! 🙌😳
Which is which ??!
😳🫀😳🫀😳🫀 !
 
Naona kuna shida mahali ndio maana wanatumia sana media na mabango kwenye barabara "kumuuza"
 
Upinzani sioni kama wamejiandaa kuchukuwa Urais, labda wajikite kwenye ubunge na madiwani wapatikane wengi waanze kurudisha tena imani kwa wananchi.
Ningeshauri kina Mbowe, Lisu, Mnyika na wengine wote wagombee tu ubunge ili waongeze hamasa, hoja na radha bungeni, kupitia hoja zao nadhani wananchi watavutiwa.
Chadema ya kina Slaa, Zito, Lisu, Mbowe, na wenzao ingeendelea kuwepo hata 2025 Urais wangebeba asubuhi sana ila du!
 
Ukiachilia hayo uliyoyasema, kubwa kabisa ni kwa sababu zifuatazo;

1. Ni raia wa nchi nyingine ya Zanzibar. Tanganyika hatuwezi tena kuongozwa na raia wa nchi ya kigeni, mkoloni!

2. Ni mwanamke. Hii nchi haiwezi kuongozwa na mwanamke abadani. Ni kosa kubwa lilitendeka huyu mama kupewa na nafasi hii. Sasa inatosha. Aondoke na kupotea kabisa!

3. Ni m - CCM. Hawa tayari walisha expire. Hawahitajiki tena. Wasitulazimishe kuwataka. CCM haihitajiki teba

NOTE:
All in all, mpaka Sasa hakuna mtu mwingine katika macho na ufahamu wangu ambaye ni "The Chosen one" kuwa kiongozi mkuu wa Taifa hili toka nje ya CCM isipokuwa TUNDU ANTIPASY MUGWAY LISSU pekee.

Ni lazima mjue kuwa, Mungu alikuwa na kusudi maalumu la kuutunza na kuuhifadhi uhai wa huyu binadamu licha ya kuwa kwa hali ya kawaida zile risasi zile 37 zilikuwa ni lazima afe, lakini Mungu akasema HAPANA, nakuhitaji kwa ajili ya kusudi langu ktk nchi yako ya Tanganyika

Watawala wa CCM hii hawapendi na wasingependa kuona huyu mtu anakuwa kiongozi mkuu wa Taifa hili kwa sababu wanaogopa kulipia madhambi na makosa yao waliyotenda kwa miaka mingi dhidi ya taifa hili na watu wake.

Na Tundu Lissu ni lazima atachukua hatua tu za kisheria dhidi ya uhalifu wa viongozi Hawa na ndiyo maana Mungu ameamua ampe yeye nchi hii.

Bwana Robert Heriel Mtibeli najua huna sababu ya maana juu ya mtu huyu kuwa Rais wa nchi hii. Lakini itakuwa hivyo na waambie wenzako kuwa, ".....for ever action, there's equal and opposite reaction..."

Katika lugha rahisi ni kuwa, hakuna tendo baya au zuri ambalo limefanywa au linafanywa au litafanywa na mwanadamu na lisipate hukumu yake

Kila mtu mtu atapata ujira wa matendo yake. Hii ni kanuni ya asili. Hakuna pa kukimbilia wala pa kujificha!!
 
Katika harakati za maisha mwaka jana nilizunguka baadhi ya vijiji kadhaa. Nilishangaa sana kusikia wanavijiji wa ndani ndani huko wakionyesha chuki za wazi kabisa kwa Rais Samia.

Wengi wa Watanzania hawampendi kabisa na mbaya zaidi Wanawake wenzake ndio kabisaa hawataki kumsikia.

Tatizo la upinzani wa Tanzania hawako makini. Mpaka sasa hakuna "mpinzani" anayeweza kuitikisa nchi kama alivyofanya marehemu L Mrema au E Lowasa.

Ikiwa mmoja kati ya WanaCCM atajitoa CCM na kugombea Urais kwa tiketi ya upinzani nina hakika atashinda.

Mtu kama William Lukuvi bado yupo ndani ya mioyo ya Watanzania wengi. Akizicheza karata zake vizuri anaweza kuwa Rais wa awamu ya saba kwa tiketi ya upinzani.
 
Katika harakati za maisha mwaka jana nilizunguka baadhi ya vijiji kadhaa. Nilishangaa sana kusikia wanavijiji wa ndani ndani huko wakionyesha chuki za wazi kabisa kwa Rais Samia.
Hili ni kweli. Huku kwetu Shinyanga na Simiyu hata usiseme, hakubaliki. Hawajui hata kama nchi Ina Rais anaitwa Samia!
Wengi wa Watanzania hawampendi kabisa na mbaya zaidi Wanawake wenzake ndio kabisaa hawataki kumsikia.
Absolutely. Tundu Lissu na CHADEMA kwa ujumla ndiyo wanazidi kumdidimiza kabisa na kumpaka mavi. Ananuka balaa;
Tatizo la upinzani wa Tanzania hawako makini. Mpaka sasa hakuna "mpinzani" anayeweza kuitikisa nchi kama alivyofanya marehemu L Mrema au E Lowasa.
Hapa umechemka. Hujui unawaza nini na pengine hujui kuwa hujui
Hivi Tundu Lissu unaweza kulinganisha na Edward Lowassa wewe?
This guy ni kitu kingine. He's a "chosen one" for this nation!
Ikiwa mmoja kati ya WanaCCM atajitoa CCM na kugombea Urais kwa tiketi ya upinzani nina hakika atashinda.
Unaharibu kila wazo lako. Unaleta ujinga mtupu hapa. Unasema mwana CCM? Nani? Samia huyu?
Stop that nonsense!
Mtu kama William Lukuvi bado yupo ndani ya mioyo ya Watanzania wengi. Akizicheza karata zake vizuri anaweza kuwa Rais wa awamu ya saba kwa tiketi ya upinzani.
Hakuna kitu hapo. Labda hukohuko CCM ili apitishwe kwa mtutu wa bunduki.

Hakuna mtu anajua huyu. Huku Simiyu na Shinyanga na Mwanza ukitaja jina hili, watakuuliza ndicho kitu gani hicho?

Mtu ambaye ni very famous kwa Sasa kuliko wote Tanzania ni Tundu Lissu peke yake whether uwe unataka au hutaki, unampenda au humpendi lakini this is undeniable fact!

Huyu akisimama kwenye u - Rais hata akikaa nyumbani tu, anajulikana si kwa sura tu bali pia kwa usafi wa kimaadili na maisha yake. Na kukiwa na uchaguzi huru na wa haki Tundu Lissu anamshinda yeyote kura zaidi ya 90%

Unataka ku - prove hili?

Muulize John P. Magufuli alifanya nini mwaka 2020. Muulize kura za u - Rais Jimbo kwa Jimbo ziko wapi mpaka Sasa. Ni kwa sababu alipigwa na Tundu Lissu mpaka aibu hata hawawezi kuzitoa kura hadharani na pamoja na jitihada za kujaribu kughushi, yote yalishashindikana!!!

Kwa heri🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️🚶🏼‍♀️
 
Back
Top Bottom