nimefanya kazi na wakenya nimeenda Kenya mara mia uzoefu wangu!
1. Wakenya wana mfumo mzuri wa elimu ya kibepari (capitalist) ambayo wahitimu hujiajiri na kwa vile wanasoma kwa English tangu chekechea kila mtu ni tour guide, anajiuza nje na ndani ya nchi, na wageni hujazana Kenya sababu ya communication, hata mama ntilie anaongea English!
2.Wakenya hutuzidi kwa kuchangamkia fursa yoyote ndani na nje ya Kenya,
3.Wakenya huapply kazi wasiyoijua wakiitwa kwa interview wanajifunza kabla ya kwenda na wakiajiriwa wanakazana kujifunza kwa wenyeji namna kazi inavyofanyika na kuongeza ya kwao
4. Wakenya wanapenda kuwa smart mda wote na kuficha umaskini na hata position iwe kubwa wanaapply tu na kwenda kujuana mbele kwa mbele!
5. wakenya wako up to date na dunia inavyokwenda na wanahaha kutafuta fursa na kuiba popote duniani ikibidi
6. wakenya wanatuzidi confidence na kila mtu anashindana maendeleo na mwenzake
7. wakenya wanatuzidi wizi na ufisadi!!
my take
Tayari Tanzania imeipita Kenya kwa ukuaji wa kiuchumi mwaka jana 6.8 versus 5.6 na hata mwaka huu wao wamefungiwa sie tunapeta tu , wakenya wanatuogopa mno kwasasa!
Tunahitaji kufanya mambo mawili tu kuwapita mbali wakenya ambao ni nchi ya pili duniani kwa ufisadi
1. Kuandika upya mtaala wenye mrengo wa kibepari ambao huhamasisha watu kujiajiri na kuwa matajiri
2.kufundisha shule kuanzia chekechea kwa English ili tuungane na dunia nzima kibiashara na kimahusiano