Kivuli cha Hayati Magufuli kinataka kumtingisha Rais Samia

Watanzania ata kesho ukimuweka ‘Angela Kairuki’ kuwa raisi awatojali ili mradi maisha yawe na unafuu.

Wanajua uwezi watengenezea ajira wote, uwezi zuia mijizi yote serikalini na wala kutatua shida zao zote pamoja na kuwaondolea umaskini...
Watakuelewa watu wachache Sana. Na kwakuwa JPM alikuwa ametofautiana na wanasiasa matajiri ndiyo maana kelele zilipata nguvu Sana.

Kelele za sasa hazipati nguvu kwakuwa zinatoka kwa wanyonge. Matajiri na wanasiasa mambo yao yamenyoka.
 
Hapa ndio nimekuelewa ulianza kumsifia marehemu kumbe kinafiki, kumbe ni mlamba asali.

Leta maji na umeme, wacheni propaganda za kishamba. Kuongoza nchi sio kama kucheza mdako
Yale yale ya marehemu alipokuwa hai. Kutotaka kukosolewa, tatizo ni zile hisia kama za uyanga na usimba kuweka vitu moyoni.

Kumkosoa mtu sio kwamba unamchukia, unataka abadilike mahali fulani kwa faida yake mwenyewe.

Hunijui hivyo huwezi kuniita mlamba asali.
 
Uelewa wangu ni tofauti kabisa. Rais kutolazimika kuwa karibu na media kwa nia ya kutaka kuitawala hakumfanyi akawa dhaifu.

Ni sawa sawa na JK tulivyomuona kama vile hafai kumbe hali ni tofauti kabisa, kukubali kukosolewa na kupokea maoni tofauti na kila upande hakumfanyi rais akawa na sifa ya kuitwa dhaifu,
Udhaifu maana yake ni mtu yeyote anapoacha kuchukua hatua stahiki hasa kwa wateule wake au watu walipo chini yake ambao hawatimizi wajibu wao kikamilifu katika nyadhifa zao walizokabidhiwa !! Ña pili kushindwa kufanya maamuzi magumu kwa maslahi ya Nchi hata kama hayo maamuzi magumu yatawagusa watu walio karibu sana na wewe !! Huo ndio huwa unaitwa udhaifu kwa mtazamo wangu. !!
 
Watakuelewa watu wachache Sana. Na kwakuwa JPM alikuwa ametofautiana na wanasiasa matajiri ndiyo maana kelele zilipata nguvu Sana.
Kelele za sasa hazipati nguvu kwakuwa zinatoka kwa wanyonge. Matajiri na wanasiasa mambo yao yamenyoka.
Huo ndio ukweli

Media bado azimkosoi raisi Samia
Polisi bado wanazuia mikutano
Kila be kitu cha demokrasia kiko vilevile toka enzi za Magufuli.

Tofauti sasa hivi mijizi inapumua na ndio watu wenye uwezo wa kuajiri watu kutukana siku nzima mtandaoni na hoja zao wanazoamini wenyewe.
 
Kuna mikutano ya kusimamiwa na balozi na kuna inayomhitaji rais mwenyewe awepo ili aonyeshe uzito wa hicho ambacho taifa lake linakihitaji.

Kuna masuala kama ya vibali vya kazi, zipo zinazoweza kufanywa kwa umahiri na wataalam kutoka nje, akaanzisha utaratibu kuwa kibali kikimaliza muda wake huyo mgeni aondoke amuachie kazi mzalendo.

Yale yale ya Mugabe na uporaji wa mashamba ya wazungu, waafrika walioachiwa yamewafia mikononi huku wazungu wakiwacheka tu.

Labda nia ilikuwa nzuri lakini inapokosewa katika utekelezaji wake inaleta picha ya serikali nzima kuwa na hulka za kibaguzi.
JK alihudhuria karibia Kila mkutano mpaka iliyofanyika uchochoroni. Cha maana alicholeta ni kipi zaidi ya Symbion, Twiga kuibiwa, zaidi ya the so called wanadiplomasia kujipigia hela kwa kivuli Cha safari za mikutano hiyo.
 
Watakuelewa watu wachache Sana. Na kwakuwa JPM alikuwa ametofautiana na wanasiasa matajiri ndiyo maana kelele zilipata nguvu Sana.
Kelele za sasa hazipati nguvu kwakuwa zinatoka kwa wanyonge. Matajiri na wanasiasa mambo yao yamenyoka.
Hakika kabisa 👍
 
Raisi hawezi kusikiliza wala kutaka ushauri kutoka kwa kila mtanzania. hao wanaomshauri huko wanatosha!
hapa hakuna ushauri ni maseng'enyo tu!
JPM atabaki kuwa JPM, SSH/SSH
kazi iendelee
 
Until that day...,
When we the people will know its not who is up there who makes things happen, but rather we the people down here who can make a change...., And not through voting but through demanding day to day what is right, and what should be done, and make our voices heard now and not waiting 5 more years for the chance to vote

Until that day....,
When we will know its us who decides what the person up there should do and not her / his favor to do what's supposed to be done...

Until that day...,
When we will know individuals won't make a dent of change but having strong institutions and knowledgeable citizens who are patriotic...

Before then we will continuing writing and commenting on such threads with nothing to show for it....
Until that day - when we Will get government of the people by the people for the people ?!
 
Ni lazima nikiri wazi kabisa, mimi nilikuwa ni mmoja wa wanaomuunga mkono JPM kwa muda wote aliokaa madarakani. Sikuficha kuunga kwangu mkono, nilisimama nae muda wote. Bahati mbaya Binadamu siku zake chini ya jua huwa zina mwisho hata afanye mema mengi kiasi gani.

Kipindi chote cha msiba wa JPM nilijawa na huzuni kuu, isiyoweza kuandikika. Lakini alipoapishwa Rais Samia kuwa wa sita tangu tupate uhuru sikuona sababu ya kutunza chuki kwake. Nilijua ni kudra ya mwenyezi Mungu anayemuandikia kila binadamu riziki yake na sikuwa nina wasiwasi na utendaji wake kwani alikuwa msaidizi mkuu wa hayati JPM kwa miaka yote ya urais wake.

Naona kama kivuli cha JPM kinataka kitumike kummaliza SSH. Ni wale wale waliokuwa wafuasi kindakindaki wa JPM ndio wanaogeuka maadui namba moja wa awamu ya sita!. Wanataka kumuona SSH akipita njia zile zile alizopita hayati ili wauone urais wake umekamilika.

Na hata akijaribu kurithi njia za kiuongozi za mtangulizi wake bado anacho kikwazo kingine kinachoangaliwa na hawa walioivaa roho mbaya awamu hii. Kigezo cha jinsia yake kudharaulika na kuonekana ni dhalili isiyo stahili kupewa nafasi ya juu ya uongozi. Akili zile zile duni za mfumo dume ndio zinazotawala baadhi ya vichwa.

JPM alikuwa na mfumo wake uliopambana sana kuhakikisha hakosolewi humu jukwaani na hata katika majukwaa mengine ya habari, hakupenda kukosolewa na huo ni udhaifu wake mkubwa.

Hakupenda kupokea ukosoaji kama changamoto ya mtu anayempenda bali alichukua kukosolewa kama ni uadui akiamini kwamba anajua kila kitu kinachoendelea duniani!. Huo ni udhaifu mkubwa sana na nadhani ni hulka aliyokuwa nayo tangu utotoni.

Akawa akitumia mbinu zile zile za ulaya mashariki za kuwa na wapelelezi wa chini kwa chini ili mradi tu Bwana Mkubwa asiguswe nafsi yake kitu ambacho kingemfanya akachukia. Hapa ndio naiona tofauti ya JPM na SSH.

JPM alitumia nguvu kubwa ili utendaji wake uonekane umekamilika kabisa (perfection) wakati SSH anafanya kazi na kuachia uhuru mpana wa maoni ya watu yakosoe kile ambacho wanaona hakiwafai. Wafuasi wa kudumu wa JPM sijui kama wanauona huo ufa wa awamu ya tano kwamba ni tatizo katika utendaji serikalini au upofu wa mahaba ni tatizo lao lisiloweza kutibika.

Naamini serikali ya awamu ya sita inaendeleza yale mema yaliyofanywa na awamu ya tano, kwani wote ni wale wale tu CCM. Na kwa wale wafuasi kindakindaki wa JPM kwao urais wa Samia utakuwa umekamilika iwapo atapita njia zile zile za mtangulizi wake.

Kwamba kama JPM aliwabagua na kuwaletea dharau jamii ya kimataifa na uwakilishi wao hapa nchini basi na SSH nae apite mule mule tu hata kama ni kwa madhara ya uchumi wetu kukosa kukua na kukosekana kwa harmony kwa maana ya uwepo wa uhusiano hasi wa TZ na jamii za nje.

Kwamba kama JPM alifukuza wakurugenzi na mawaziri kwa habari ambazo hakuwa na uhakika nazo basi na SSH nae apite mule mule tu, wawepo mawaziri na wateule wengi waliofukuzwa kazi huku wakiendelea kulipwa mshahara wa bure.

Kwamba kama JPM aliikuza chuki kati ya wanyonge na matajiri akiamini kuwa umaskini wa mnyonge chanzo chake ni utajiri wa tajiri basi na SSH aendeleze mateso kwa matajiri tena yale ya kihisia tu!.

SSH ameelewa umuhimu wa kujichanganya kimataifa, anajua ni kwa namna gani binadamu hajaumbwa aishi kama kisiwa hivyo amehakikisha sekta ya mahusiano na mataifa mengine inakuwa na watendaji nguli na wenye uzoefu nayo.

JPM alifanya mema lakini awamu yake isipewe sana utakatifu ambao haikuwa nao. Na SSH asipewe sana ushetani akionekana kama vile anakosea pale anapokwenda tofauti na mawazo au itikadi za mtangulizi wake.

Wote wawili kwa wakati wao wamebarikiwa kuwa marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Umejificha kwenye ujinga ili utufanye na sisi wajinga!
Hakuna wafuasi wa JPM bali kuna wafuasi wa kupenda maendeleo, kuchukia wizi, wapenda maendeleo kwa kasi ya JPM
Kama unafurahia
Wizi unapofanyika
Madini yanayotoroshwa
Wanavyuo kukosa mikopo
Miradi kukwama
Huduma za umeme na maji hakuna
Mfumuko wa bei kutisha
Tozo za ajabu ajabu
Nk nk
Kama bado ni mfuasi wa Samia ukapimwe akili
 
Yale yale ya marehemu alipokuwa hai. Kutotaka kukosolewa, tatizo ni zile hisia kama za uyanga na usimba kuweka vitu moyoni.

Kumkosoa mtu sio kwamba unamchukia, unataka abadilike mahali fulani kwa faida yake mwenyewe.

Hunijui hivyo huwezi kuniita mlamba asali.
Kwanini huyu anafanya blanda asikosolewe? Maji na umeme ni vitu vya anasa
 
Kama haelewi Hilo watammaliza ila Kama anaelewa lazima ajipambanue kitofauti..

This time around Sukuma gang wameungana na Chadomo japo kwa maslahi tofauti..

Chadomo wanatafuta upenyo wa madaraka na Sukuma gang wanapigania Ligacy na Kutaka Mambo yaendelee Kama awali..

But Kama walishindwa mapema kabisa enzi za kina Jobo naona hiyo Ni nafasi ndogo kwao ila Chadomo ndio wanapuliza Sana..

Samia hawezi pita njia ya uovu maana kwa vigezo vyote iwe kwa namba au ufanisi Samia keshawafunika,Ni vile hapa Kuna Mambo ya dini,jinsia na Uzanzibari nothing else..

Kuliko Sukuma gang kurudi Madarakani Bora Nchi iende kwa Chadomo..

Sijawahi mkubali Mwendazake Wala siasa za CCM ila awamu hii Niko na SSH.

JF Admin

Inakuwaje naona post za huyu binadamu?

Wakati nilimblock!

Naomba ufafanuzi
 
Ni lazima nikiri wazi kabisa, mimi nilikuwa ni mmoja wa wanaomuunga mkono JPM kwa muda wote aliokaa madarakani. Sikuficha kuunga kwangu mkono, nilisimama nae muda wote. Bahati mbaya Binadamu siku zake chini ya jua huwa zina mwisho hata afanye mema mengi kiasi gani.

Kipindi chote cha msiba wa JPM nilijawa na huzuni kuu, isiyoweza kuandikika. Lakini alipoapishwa Rais Samia kuwa wa sita tangu tupate uhuru sikuona sababu ya kutunza chuki kwake. Nilijua ni kudra ya mwenyezi Mungu anayemuandikia kila binadamu riziki yake na sikuwa nina wasiwasi na utendaji wake kwani alikuwa msaidizi mkuu wa hayati JPM kwa miaka yote ya urais wake.

Naona kama kivuli cha JPM kinataka kitumike kummaliza SSH. Ni wale wale waliokuwa wafuasi kindakindaki wa JPM ndio wanaogeuka maadui namba moja wa awamu ya sita!. Wanataka kumuona SSH akipita njia zile zile alizopita hayati ili wauone urais wake umekamilika.

Na hata akijaribu kurithi njia za kiuongozi za mtangulizi wake bado anacho kikwazo kingine kinachoangaliwa na hawa walioivaa roho mbaya awamu hii. Kigezo cha jinsia yake kudharaulika na kuonekana ni dhalili isiyo stahili kupewa nafasi ya juu ya uongozi. Akili zile zile duni za mfumo dume ndio zinazotawala baadhi ya vichwa.

JPM alikuwa na mfumo wake uliopambana sana kuhakikisha hakosolewi humu jukwaani na hata katika majukwaa mengine ya habari, hakupenda kukosolewa na huo ni udhaifu wake mkubwa.

Hakupenda kupokea ukosoaji kama changamoto ya mtu anayempenda bali alichukua kukosolewa kama ni uadui akiamini kwamba anajua kila kitu kinachoendelea duniani!. Huo ni udhaifu mkubwa sana na nadhani ni hulka aliyokuwa nayo tangu utotoni.

Akawa akitumia mbinu zile zile za ulaya mashariki za kuwa na wapelelezi wa chini kwa chini ili mradi tu Bwana Mkubwa asiguswe nafsi yake kitu ambacho kingemfanya akachukia. Hapa ndio naiona tofauti ya JPM na SSH.

JPM alitumia nguvu kubwa ili utendaji wake uonekane umekamilika kabisa (perfection) wakati SSH anafanya kazi na kuachia uhuru mpana wa maoni ya watu yakosoe kile ambacho wanaona hakiwafai. Wafuasi wa kudumu wa JPM sijui kama wanauona huo ufa wa awamu ya tano kwamba ni tatizo katika utendaji serikalini au upofu wa mahaba ni tatizo lao lisiloweza kutibika.

Naamini serikali ya awamu ya sita inaendeleza yale mema yaliyofanywa na awamu ya tano, kwani wote ni wale wale tu CCM. Na kwa wale wafuasi kindakindaki wa JPM kwao urais wa Samia utakuwa umekamilika iwapo atapita njia zile zile za mtangulizi wake.

Kwamba kama JPM aliwabagua na kuwaletea dharau jamii ya kimataifa na uwakilishi wao hapa nchini basi na SSH nae apite mule mule tu hata kama ni kwa madhara ya uchumi wetu kukosa kukua na kukosekana kwa harmony kwa maana ya uwepo wa uhusiano hasi wa TZ na jamii za nje.

Kwamba kama JPM alifukuza wakurugenzi na mawaziri kwa habari ambazo hakuwa na uhakika nazo basi na SSH nae apite mule mule tu, wawepo mawaziri na wateule wengi waliofukuzwa kazi huku wakiendelea kulipwa mshahara wa bure.

Kwamba kama JPM aliikuza chuki kati ya wanyonge na matajiri akiamini kuwa umaskini wa mnyonge chanzo chake ni utajiri wa tajiri basi na SSH aendeleze mateso kwa matajiri tena yale ya kihisia tu!.

SSH ameelewa umuhimu wa kujichanganya kimataifa, anajua ni kwa namna gani binadamu hajaumbwa aishi kama kisiwa hivyo amehakikisha sekta ya mahusiano na mataifa mengine inakuwa na watendaji nguli na wenye uzoefu nayo.

JPM alifanya mema lakini awamu yake isipewe sana utakatifu ambao haikuwa nao. Na SSH asipewe sana ushetani akionekana kama vile anakosea pale anapokwenda tofauti na mawazo au itikadi za mtangulizi wake.

Wote wawili kwa wakati wao wamebarikiwa kuwa marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunashukuru sasa umeamua kuachana na marehemu rasmi kuja kulamba asali. Tulikuwa tunakutizama tu tunajua nazi haishindani na jiwe. Karibu sana upande huu. Sasa unaweza rasmi nawe ukaanza kuelezea mabaya ya magufuli. Mama anafungua nchi na tujajenga nchi huku tukilamba asali. Usiache kuonekana huku sasa ukitupia nyuzi hapa na pale...
 
maji na umeme ni kikwazo kikubwa ukijumlisha na mfumuko wa bei za bidhaa bila kusahau tozo na bando!
 
Back
Top Bottom