Kiwango cha uelewa kwa viongozi wetu kiko chini sana

Kiwango cha uelewa kwa viongozi wetu kiko chini sana

Nyie mnaoponda viongozi kama mna akili kwanini hamkugombea hizo nafasi ili muongoze?
Unagombea kwenye nini?

Unagombea mahali ambapo kura haziamui aliyechaguliwa ndio awe mshindi bali mtutu wa bunduki na mapenzi ya mwenyekiti wa CCM??

Wewe mama Samuya kwa muundo wa hiyo mnayoita tume "huru" ingekuwa imeteuliwa na Lissu mngeenda kushiriki uchaguzi?
 
Kwanza elewa kama husomi Vitabu na majarida mbalimbali huwezi kuwa na ubongo unaochemka, na watu wetu wengi ni matunda ya mifumo mibovu ya Elimu yetu ambayo inataa tu maksi sio uelewa wa mambo, kingine ni uchawa ambao mtu hata kama ni kilazq akiwa na hela au cheo anapata watu wanamshangilia kwa ujinga tu.

Watu wasiosoma ni majanga na ndio viongozi wakuu hawajitumi kusoma hawajui hata Dunia inataka nini.. au wafanye nini kutatua kero na shida za hii nchi ...myie hamshangai Waziri kusema watu waandike madokezo kuhusu foleni miji yetu mikubwa?? hivi kweli hawajui chanzo cha foleni?

Ni mtu wa jabu atasema hajui chanzo cha foleni na hii ni mada nyingine kabisa by itself siwezi kuijadili leo ni pana ila kwa ufupi majanga ya kuwa na watu vilaza yanatuingiza shimoni na ndio tunapotea ndio mana hata tukipata Rais mzuri kama Magufuli ataumizwa na mfumo mbovu uliooza sana ambao ni kikundi kidogo cha watu ndio kinaongoza kuiba rasilimali za nchi na kujineemsha wao na familia zao pekee.
Magufuli msimtolee mfano kama kiongozi aliyekuwa na upeo wa juu. Uelewa wake katika masuala ya uchumi na uongozi ulikuwa chini sana. Ndio maana alikimbilia kuunda vikosi vya kuua watu wanaomkosoa badala ya kutafakari na kutoa fact. Alivuruga sekta binafsi ambayo ni mdau mkubwa wa kukua kwa uchumi wa taifa. Vilevile alivuruga mifumo ya utoaji haki hasa mahakama na bunge. Kwa vyovyote vile utawala wa magufuli usingeleta sustainability katika maendeleo ya Tanzania.
 
Nyie mnaoponda viongozi kama mna akili kwanini hamkugombea hizo nafasi ili muongoze?
Nani agombee kwenye corrupted system? Anybody mwenye smart kichwani knows no way atatoboa kwa mfumo uliopo

Umekuwa designed kubeba low Iq people , chawa, na umaarufu kuliko kuchukua watu kwa performance na high IQ zao

Mfumo hautakil smart people , ni known fact
 
Magufuli msimtolee mfano kama kiongozi aliyekuwa na upeo wa juu. Uelewa wake katika masuala ya uchumi na uongozi ulikuwa chini sana. Ndio maana alikimbilia kuunda vikosi vya kuua watu wanaomkosoa badala ya kutafakari na kutoa fact. Alivuruga sekta binafsi ambayo ni mdau mkubwa wa kukua kwa uchumi wa taifa. Vilevile alivuruga mifumo ya utoaji haki hasa mahakama na bunge. Kwa vyovyote vile utawala wa magufuli usingeleta sustainability katika maendeleo ya Tanzania.
Uko sahihi kwa hiki ulichosema kuhusu Magufuli. Alichofanikiwa Magufuli ni kubrainwash wananchi hadi kumuona ni kama malaika, na akafanikiwa kutengeneza vikosi vya kuzuia sauti ya pili dhidi ya udhaifu wake. Hata waliongia mkenge wa sifa za utawala wake ukiwahoji kuhusu mapungufu yake, hawana utetezi wa maana.
baz kaiza Idugunde
 
Matokeo ya mifumo mibovu ya elimu.

Kuruhusu watu duni katika kuchanganua mambo kutuongoza.

Kuruhusu chama kimoja kuwa na uwezo mkubwa kupita serikali na watu wake.

Kuwa na genge la oligarchs, limekuwa na nguvu kuliko the entire government.
Hayo yote yanakuwa summarized na udhaifu wetu sisi wananchi mkuu. Unadhani pangekuwa na miamko mingi kama ya oct 29..hawa jamaa wangeendeleza hayo maujinga?
 
Kwanza elewa kama husomi Vitabu na majarida mbalimbali huwezi kuwa na ubongo unaochemka, na watu wetu wengi ni matunda ya mifumo mibovu ya Elimu yetu ambayo inataa tu maksi sio uelewa wa mambo, kingine ni uchawa ambao mtu hata kama ni kilazq akiwa na hela au cheo anapata watu wanamshangilia kwa ujinga tu.

Watu wasiosoma ni majanga na ndio viongozi wakuu hawajitumi kusoma hawajui hata Dunia inataka nini.. au wafanye nini kutatua kero na shida za hii nchi ...myie hamshangai Waziri kusema watu waandike madokezo kuhusu foleni miji yetu mikubwa?? hivi kweli hawajui chanzo cha foleni?

Ni mtu wa jabu atasema hajui chanzo cha foleni na hii ni mada nyingine kabisa by itself siwezi kuijadili leo ni pana ila kwa ufupi majanga ya kuwa na watu vilaza yanatuingiza shimoni na ndio tunapotea ndio mana hata tukipata Rais mzuri kama Magufuli ataumizwa na mfumo mbovu uliooza sana ambao ni kikundi kidogo cha watu ndio kinaongoza kuiba rasilimali za nchi na kujineemsha wao na familia zao pekee.
nonsense
 
Uko sahihi kwa hiki ulichosema kuhusu Magufuli. Alichofanikiwa Magufuli ni kubrainwash wananchi hadi kumuona ni kama malaika, na akafanikiwa kutengeneza vikosi vya kuzuia sauti ya pili dhidi ya udhaifu wake. Hata waliongia mkenge wa sifa za utawala wake ukiwahoji kuhusu mapungufu yake, hawana utetezi wa maana.
baz kaiza Idugunde
Unachotaka kumaanisha ni nini?
 
Siyo siri kwa sasa hivi, kiwango cha uelewa na kufikiri kwa mantiki kwa viongozi wetu kimepungua sana miaka ya karibuni.
Sioni kiongozi THINKER, na mwenye uwezo wa kuufikiria umma wa kawaida.

Watu kama Mwalimu Nyerere, watu wenye uwezo wa kufikiria mifumo kama ya kijamaa kwa ajili ya umma wote, watu hao waliondoka na hawapo kabisa.

Uelewa kwa maana ya vichwa vilivyojaa data zinazoweza kutumika kwa manufaa ya nchi , umekuwa adimu kwa viongozi wetu. Ni mshangao kukuta kuna viongozi hawajui hata zile basics za sayansi ya jamii na matamanio ya wananchi.

Tumebaki na viongozi wanasiasa wanao endeleza survival politics, watu wa kujineemesha.

Watu kama hawa wanasiasa wa sasa wapo zaidi kujitetea na kutumia dola kuhakikisha maslahi binafsi ya utawala unalindwa kwa gharama yoyote.

Nini maoni yako?
Viongozi wetu kwa namna yoyote huwezi kuwatenganisha na wananchi wao.

Jamii iliyo na idadi kubwa ya wajinga hakuna namna inaweza kuwa na viongozi wasio wajinga.
Kwa hiyo tusiseme viongozi wana uelewa mdogo bali taifa letu lina wananchi wenye uelewa mdogo. Ndio maana zinaibuka issue za kijinga kama watu kusema nyeti zao zimepotea na inakuwa bonge la topic mitandaoni.
 
Kujipachika kwa mtutu sio hoja, kama kuna watu werevu wengi wangeweza kuwa na mkakati bora wa kuweza kuwa outsmart hao wenye mitutu.
Hao viongozi hawajachaguliwa katika hizo nafasi, wamejipachika kwa mtutu wa bunduki. Pia hata ukiwa na wapiga kura wengi wajinga watawachagua wajinga wenzao tu wawaongoze.
 
Nakuunga mkono kwa asilimia zote. Watu hupenda kukwepa uwajibikaji kwa kurushia lawama au mapungufu yao kwa viongozi wakati huo unakuta mtu huyo hakuna alicho kianzisha na ku achieve maishani mwake.
Kiwango cha uelewa wa hao viongozi kina reflect hali halisi ya kiwango cha uelewa wa jamii inayowazaa

Tunapata viongozi tunaowastahili, kama unataka viongozi wenye uwezo kama wa Mwalimu Nyerere, lazima kwanza upate umma wenye ujasiri na uelewa wa aina ya wale waliomweka Nyerere madarakani.
 
Back
Top Bottom