Kizazi cha 1978-1985 hatuzeeki. Je, unajua sababu?

Kizazi cha 1978-1985 hatuzeeki. Je, unajua sababu?

Tuliozaliwa 1978- 1985 tunarange kuanzia miaka 39-46, tumegoma kuzeeka, sijui kama mnafahamu sababu.

Iko hivi, kipindi hicho nchi ilipitia changamoto za kiuchumi, tulikuwa na vita ya iddi Amin hata baada ya vita hali haikuwa shwari, tuliendelea kufunga mikanda, uzalishaji wa chakula haukua vizuri, kama nchi tuliagiza chakula nje ya nchi, mnaukumbuka ugali wa Yanga??

Ni mpaka Mwinyi alipochukua nchi tukaanza kula vizuri, asikwambie mtu afya ya mtoto hutegemea genes za wazazi na chakula, hayo mambo mawili ndio huamua muonekano wa mtu ukubwani.

Tuliozaliwa miaka hiyo kuna virutubishi tulikosa matokeo yake tukatengeneza hybreed ya watu fulani, sio magiant sio wafupi, ni kuanzia futi 5 na inchi 4 mpaka futi 5 na inchi 8 wengi tuko humo.

Kukuta kijana wa 1980 ananyimwa shikamoo anapewa wa 1990 ni kawaida sana.
Orodha ya watu mashuhuri wanaoangukia humo ni kama hii
Dully Sykes, 45
Ridhwan Kikwete, 45
Mwana FA, 45
Queen Daren, 44
Single Mtambalike, 47
Ben Kinyaiya, 46
Maulid Kitenge, 48
Haji Manara, 50
Mange Kimambi, 46
Juma Nature 44
Ray kigosi 47.
Joti 45
Mpoki 47

Njoo kwa wadogo zetu sasa,binti miaka 25 kama veterani wa vita ya pili ya dunia,kijana miaka 30 ni kama mpigania uhuru,

Hawa ni watu ambao either nimesoma nao au nawafahamu kiundani tangu utotoni miaka ya rary 80's

Uzi huu hauwausu walioharibu afya zao kwa pombe kali na starehe zingine
Huyu
Bina Chumchang Changchum unaitwa huku. 😂
Kapatia lkn kidogo vitunguu vimezidi chumvi 😅😅😅
 
ila hata hivyo wazee wa 1990 ni masela sana na mvi zao zilizojaa jaa sana kidevuni 🐒

kabinti kakisalimia shikamoo... kanaitikiwa vizuri tu markhabah na Mzee wa 1990, lakini Lazima katapigwa na ile salamu ya mambo vip uko poa....
ili kutengeneza mazingira ya uflat na kumuondoa mtoto hofu 🐒

Vizee vya 1990 ni visela nuksi sana aise dah 🐒
Kumbe wa 90 nao niwazee? Sikujua
 
Chakula asilia, mazoezi ya kiasi, kuwa free stressed, kupumzisha mwili, kuwa Mcha Mungu huchelewesha sana uzee.

Ubinadamu ni kazi The humanity is a work.View attachment 2984487
8885e7e6e3599d57dcf0f87dc2089fe6.jpeg
 
Pesa ndio kila kitu, nyie wenye 45 mmetokea kipindi ambacho fursa zilikuwa wazi. Sahizi mnaweza ishi healthy lifestyle unalipa GYM, Una kazi nzuri au biashara kubwa kubwa. Una mke mtulivu kakuzalia watoto mnaishi kifamilia. Hapo kwanini usiwe na nuru.

Kijana wa 90 anapambana na harsh reality kwamba anatakiwa aendeshe maisha kwa boda boda au kuchoma mahindi ilihali ana cheti kizuri cha chuo. Wengi wanajificha kwenye udalali wa simu na vinginevyo ilimradi maisha yaende walau kuficha identity zao. Utaacha kuzeeka kweli, huku wimbo ni tafta helaaaa...Kazi huna lazma uchanganyikiwe
 
Back
Top Bottom