Kizazi cha leo kisingeweza kumtoa mkoloni nchini,Tanzania ingekuwa ya mwisho kupata Uhuru

Kizazi cha leo kisingeweza kumtoa mkoloni nchini,Tanzania ingekuwa ya mwisho kupata Uhuru

Kwahiyo baada ya vita hizo ulizo zitaja ndipo Tanganyika ikapata uhuru?

Nimeanza kuwaelewa wazee wa zamani, "Darasa la 6 wa miaka ya 70-80s ni sawa na Masters sasa hivi ".

Mitoto ya sikuhizi hamuna akili kabisa, ndio maana wanasiasa wanaweza kuwashikieni akili zenu.

..mkoloni wetu, kwa maana MJERUMANI, aliondolewa na wakoloni wenzake.

..kwa hiyo Tanganyika tukawa chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa, ambao walitukabidhi kwa Waingereza "watulee" mpaka tutakapoweza kujitawala.

..Na kweli Waafrika tulipopeleka petition kwamba tunaweza kujitawala Umoja wa Mataifa na Waingereza wakaachia ngazi.

..Mazingira hayo ya kihistoria ndio yaliyowezesha tupate uhuru bila kumwaga damu.

..Ukiangalia historia ya kudai uhuru wa Tanganyika, na harakati za kudai demokrasia ya ukweli, utaona kwamba ilikuwa rahisi mno kudai uhuru.

..Mwalimu Nyerere, viongozi wa Tanu, na wanachama, hawakupitia hata robo ya unyama na udhalimu wanaopitia wapinzani ktk zama hizi za kudai demokrasia ya kweli.
 
Kwa tanzania ya miaka hii ya kizazi cha machawa, mkoloni wala hata asingepata shida kutawala, tena angewatumia wasomi kama mwigulu,Kabudi,Makamba, kuitawala hii nchi na kuifanyia exploitation kadri anavyotaka bila bugudha yoyote.
 
Viongozi wa sasa wasingeonyesha motive / vision ya faida ya kumtoa mkoloni, hivyo hata hao mababu zetu wasingeamini wasemayo walamba asali...

Viongozi wa sasa ni Makasongo wa kale walikuwa visionaries ambao objectives zao zilikuwa smart...
  • Specific,
  • Measurable,
  • Achievable,
  • Relevant,
  • Time-bound.
By the way hata wananchi walichodhani watapata na walichopata wengi walisikitika..., ndio maana kuna vitabu kama Not Yet Uhuru
 
Mkoloni Tanganyika hakutolewa kwa mapigano, acheni kuipotosha history ya nchi yetu, kwa vitu vyenu vya kipuuzi.
Hakuna aliyesema mkoloni katolewa kwa mapigano...
 
Vipi na Hawa wazee wa zamani waliopigania uhuru ndio wamekua mafisadi wakubwa wanao ingia mikataba mibovu hata hawanauchungu na hii nchi?
 
Kwahiyo baada ya vita hizo ulizo zitaja ndipo Tanganyika ikapata uhuru?

Nimeanza kuwaelewa wazee wa zamani, "Darasa la 6 wa miaka ya 70-80s ni sawa na Masters sasa hivi ".

Mitoto ya sikuhizi hamuna akili kabisa, ndio maana wanasiasa wanaweza kuwashikieni akili zenu.
Ukiwemo na wew pia
 
Bora tunge endelea kutawaliwa na mkoloni, kuliko haya yanayo endelea kutenda na utawala huu
 
..Waingereza hawakuwa wakatili na madhalimu kama Ccm na askari wao.

..hakuna mahala popote katika historia panapoonyesha kwamba wanachama wa Tanu walifanyiwa fujo na kujeruhiwa na vyombo vya dola.
 
Hakuna mwafrika aliyemtoa mkoloni. Yeye ndo aliamua kwenda.
Hata mimi huwa nawaza tu, Africa ilikuwa na silaha gani za kumuondoa mkoloni ikiwa vita inategemea uchumi na sisi uchumi wetu walikuwa wameshika wao. Mimi huwa nadhani walibuni mbinu nyingine ya kututawala hivyo wakaamua kutuacha tuwe masoko ya bidhaa zao maana kama ni mali walishazichuma na chumi zao zilishakua na ndio maana wale wakoloni waliokuwa na uchumi mdogo kama Ureno walisumbua kweli kutoka. Ukichunguza kwa makini utagundua kuwa Africa haikupewa full independence kuna maeneo bado tunapangiwa hata namna ya kutumia rasilimali zetu.
 
Back
Top Bottom