Kizuwizi cha askari wa Lindi, ni moja ya vizuwizi maharamia na magaidi wanakichukia sana

Kizuwizi cha askari wa Lindi, ni moja ya vizuwizi maharamia na magaidi wanakichukia sana

TumainiEl

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
6,782
Reaction score
12,716
Nimesikia tukio la dereva kutaka kuwaua Askari ila wakamuwahi, jambo hili sijalishangaa kwangu naona kuwa ni jambo sasa Serikali kuweka vifaa maalumu pale kwenye kizuwizi kuwasaidia hawa Askari.

Kiufupi ukiwa kusini ukimuuliza dereva au mtu anaye ijua hiyo barabara atakwambia askari wapale Lindi ni hatari why?

Pale ndio stop point, utapita kote utahonga kote ila ukifika na mzigo Lindi kazi unayo pale wale jamaa hata kama watasema wanachukua rushwa minu nadhani itakuwa rushwa sio ya kawaida ila wapo makini hupiti kama una haramu umebeba na huo ndio ukweli.

Kwa wale wataalam wa yale yanayoendelea kusini utakubaliana na mimi Lindi hapawezi kuwa sehemu ya kupenda na maharamia au madereva wanaobeba magendo.

Niwape pole jeshi la polisi na niwatie nguvu kukaza bidii. Kazi na iendelee.
 
Mtoa hoja hii ni shetani na katili mno na ni hatari mno maana anatuletea familia iliyojaa ukatili,story iliyosikika hapa ni ya upande mmoja tu,dereva mwenye kisu(sina hakika nalo)ashambulie askari mwenye SMG!huu ni uongo at it's best na elewa dereva huyu amepata ajali!key witness ni abiria waliokuwepo hapo na mimi siamini kabisa story ya rpc,ndio maana nchi inahitaji KATIBA mpya maana itatuletea IPID (kama MPs wa jeshi)na kesi hii ingechunguzwa na hawa IPID,mtoa hoja hii ni mkatili mno na mpenda trigger happy policemen
 
Kizuizi kile bila shaka kina watu wengine kutoka taasisi za ulinzi na usalama kutokana na yanayoendelea Msumbiji, ndiyo maana ni ngumu kupokea rushwa.

Lakini askari wetu wanayo historia ya ku abuse nafasi walizonazo kwa kuwapiga watu risasi na kisha kutunga stori ili ku cover uhalifu wao.

Ni wakati sasa tuwe na chombo tofauti cha kuchunguza matukio ambayo raia wanauawa mikononi mwa polisi
 
Usalama wa Raia na Mali zao.....ni baadhi tu ya Polisi wachache hawana uadilifu na inatokana kwa kushirikiana na raia wabaya.
Lakini pia wale traffic waliopo Bagamoyo/ Msata Road siyo askari wazuri,wanadhulumu kwa kutumia crown na uniform zao na pia speed rader ambayo ni mbovu na wana edit speed per km ili wakutoe mapesa.
OMBI....Jeshi la polisi usalama barabarani toeni elimu kuhusu speed raders na muonekano halali unavyokuwa.
 
Nimesikia tukio la dereva kutaka kuwauwa ma askari ila waka muwahi jambo hili sijalishangaa kwangu naona kuwa nijambo sasa serikali kuweka vifaa maalumu pale kwenye kizuwizi kuwasaidia hawa ma askari.
Kiufupi ukiwa kusini ukimuuliza dereva au mtu anaijuwa hiyo barabara atakwambia askari wapale lindi ni hatari why?
Pale ndio stop point utapita kote utahonga kote ila ukifika na mzigo Lindi kazi unayo pale wale jamaa hata kama watasema wanachukuwa rushwa mm nadhani itakuwa rushwa sio ya kawaida ila wapo makini hupiti kama una haram umebeba na huwo ndio ukweli.

Kwa wale wataalam wa yake yana endelea kusini utakubaliana na mimi Lindi hapawezi kuwa sehem yakupenda na maharamia au madereva wanaobeba magendo.
Niwape pole jeshi la polisi na niwatie nguvu kukaza bidii. Kazi na iyendelee.
Polisi wa nchi gani hao wasiopokea mlungula? Juzi nilikuwa natokea Kigoma na Bus la Kampuni fulani, nikawa nimekaa siti ya mbele kabisa na nimeshuhudia askari mpaka mwenye nyota anachukua mlungula wa buku mbili!! Konda alikuwa amezichenji buku mbili mbili kama za elfu 30 hivi, na akawa anazigawa kama njugu ....
 
Hivi hujui kisu kinaweza uwa madazeni ya watu?,soma taarifa mbalimbali duniani,acha ufala koko
Kwa hiyo polisi kadhaa wenye bunduki hawawezi kumdhibiti mtu mwenye kisu kwa kumvunja hata miguu?? Ni kwa nini kila siku tunasikia tuu wameuwawa na hakuna hata siku moja tumeskia amedhibitiwa kwa kuvunjwa miguu???
 
Kuna point moja hapo juu ya mdau nimeipenda, Kunapaswa kuwa na chombo kingine nje ya jeshi la polisi kitakachokuwa kinachunguza matukio yenye sintofahamu dhidi ya jeshi la polisi...

Hii inaweza kuwafunga governor mapolisi na kuitendea haki taaluma yao, lakini pia itasaidia kutoa haki dhidi ya raia kwenye matukio kama haya...
 
Mtoa hoja hii ni shetani na katili mno na ni hatari mno maana anatuletea familia iliyojaa ukatili,story iliyosikika hapa ni ya upande mmoja tu,dereva mwenye kisu(sina hakika nalo)ashambulie askari mwenye SMG!huu ni uongo at it's best na elewa dereva huyu amepata ajali!key witness ni abiria waliokuwepo hapo na mimi siamini kabisa story ya rpc,ndio maana nchi inahitaji KATIBA mpya maana itatuletea IPID (kama MPs wa jeshi)na kesi hii ingechunguzwa na hawa IPID,mtoa hoja hii ni mkatili mno na mpenda trigger happy policemen
Usishangae Sana huyo jamaa alisemaga atampoteza Ben Saa8 na jamaa akapotea kweli.
 
Unanikumbusha Misgiri, pale ukaguzi wa gari hufanywa kwa uhakika, kongole sana
 
Hiyo taarifa ya polisi naitilia mashaka,dereva mwenye kisu atake kuwaua askari 4 wenye siraha?.hapa kuna vitu vingi vimefichwa,Polisi wetu wanajulikana kwa kuficha taarifa ili kulindana.

hv kwel haujui km kisu n silaha hatar
 
Hawa jamaana wanafanya watu wwngine washindwe kupitisha magendo kwwnda msumbiiji..ndo maana jamaa alijitia muhanga..huyo jamaa unaweza kukuta ni gaidi
Apumzike anakostahili. Ukiifuatilia vizuri historia yake, unaweza kukuta ndio wale wale wanaohenyeshwa Msumbiji sasa hivi
 
Hiyo taarifa ya polisi naitilia mashaka,dereva mwenye kisu atake kuwaua askari 4 wenye siraha?.hapa kuna vitu vingi vimefichwa,Polisi wetu wanajulikana kwa kuficha taarifa ili kulindana.
Wenye akili mmebakia wachache sana nchi hii. Siyo kama huyu mleta mada anataka kuwaaminisha watanzania eti askari wa Lindi ni malika.
 
Kizuizi kile bila shaka kina watu wengine kutoka taasisi za ulinzi na usalama kutokana na yanayoendelea Msumbiji, ndiyo maana ni ngumu kupokea rushwa.

Lakini askari wetu wanayo historia ya ku abuse nafasi walizonazo kwa kuwapiga watu risasi na kisha kutunga stori ili ku cover uhalifu wao.

Ni wakati sasa tuwe na chombo tofauti cha kuchunguza matukio ambayo raia wanauawa mikononi mwa polisi
Mfano ni juzi tu polisi waliuana kule Kilimanjaro kwa visa vya magendo wakatunga uongo kuwa amekufa kwa ajali - nadhani the story went that way. Lakini walipochunguzana baada ya ndugu wa askari aliyekufa kusimama kidete wakagundua kuwa aliuawa na wenzie.
Hii story ya Lindi yapaswa ichunguzwe na upande usio na maslahi na polisi kwani kwa maelezo ya RPC ni ngumu kueleweka - story haijanyooka.
 
Back
Top Bottom