Kizuwizi cha askari wa Lindi, ni moja ya vizuwizi maharamia na magaidi wanakichukia sana

Mtoa hoja hii ni shetani na katili mno na ni hatari mno maana anatuletea familia iliyojaa ukatili,story iliyosikika hapa ni ya upande mmoja tu,dereva mwenye kisu(sina hakika nalo)ashambulie askari mwenye SMG!huu ni uongo at it's best na elewa dereva huyu amepata ajali!key witness ni abiria waliokuwepo hapo na mimi siamini kabisa story ya rpc,ndio maana nchi inahitaji KATIBA mpya maana itatuletea IPID (kama MPs wa jeshi)na kesi hii ingechunguzwa na hawa IPID,mtoa hoja hii ni mkatili mno na mpenda trigger happy policemen
Kwa hiyo tukiandika katiba mpya hatutakuwa na jeshi la polisi? Hawatakuwa na silaha? Hakutakuwanna vizuizi? Hakutakuwa na wahalifu?
 
Hiyo taarifa ya polisi naitilia mashaka,dereva mwenye kisu atake kuwaua askari 4 wenye siraha?.hapa kuna vitu vingi vimefichwa,Polisi wetu wanajulikana kwa kuficha taarifa ili kulindana.
Nipo Masasi hapa Mkuu kuhusu hiyo ishu wengi hawajui kabisaaa... ukweli ni kuwa hawa polisi wameficha ushahid pia jamaa ameuawa Kwa makusudi Tu na polisi kwasabb ya pesa.

Dereva alikuwa pekeyake ndani ya gari na ameporwa pesa na vitu vingine vya thamani pamoja na documents za oficn kwake,huku Kwenye mitandao watu hawajui lolote zaidi kupata picha ya upande mmoja
 
Mfano ni juzi tu polisi waliuana kule Kilimanjaro kwa visa vya magendo wakatunga uongo kuwa amekufa kwa ajali - nadhani the story went that way. Lakini walipochunguzana baada ya ndugu wa askari aliyekufa kusimama kidete wakagundua kuwa aliuawa na wenzie.
Hii story ya Lindi yapaswa ichunguzwe na upande usio na maslahi na polisi kwani kwa maelezo ya RPC ni ngumu kueleweka - story haijanyooka.
Mimi mwenyewe nipo huku kusini/Masasi hii ishu kumbe ni usanii wa polisi wametunga na wameiba pesa na vitu vingine.
Kumbuka haya Magari wanakuwa na Dereva pekeyake Kwanza polisi walianza kufyatua risasi Kwenye matairi mpaka gari ikahama njia na jamaa alivyoshuka akapigwa risasi
 
Nipo Masasi hapa Mkuu kuhusu hiyo ishu wengi hawajui kabisaaa... ukweli ni kuwa hawa polisi wameficha ushahid pia jamaa ameuawa Kwa makusudi Tu na polisi kwasabb ya pesa.

Dereva alikuwa pekeyake ndani ya gari na ameporwa pesa na vitu vingine vya thamani pamoja na documents za oficn kwake,huku Kwenye mitandao watu hawajui lolote zaidi kupata picha ya upande mmoja
Dereva gani wa lori la cement anayebeba pesa ya kuuawa nazo? Acheni uzushi. Kama ingekuwa hivyo mauaji yangekuwa mengi sana.
 
Kwa hiyo tukiandika katiba mpya hatutakuwa na jeshi la polisi? Hawatakuwa na silaha? Hakutakuwanna vizuizi? Hakutakuwa na wahalifu?
Mambo mengine soma tu Mkuu , maana hawajui waandikayo
 
Dereva gani wa lori la cement anayebeba pesa ya kuuawa nazo? Acheni uzushi. Kama ingekuwa hivyo mauaji yangekuwa mengi sana.
Kwahiyo unaamini kuwa Dereva alienda na kisu kuwashambulia Askari?
Au Dereva alikuwa chizi? Kwa akili ya kawaida inawezekana vipi Dereva aende kuwashambulia Askari huku akiwa Hana hata wembe? Jiulize Kwann gari ilishambuliwa Kwa risasi?
 
Nilimsikia kamanda wa polisi akielezea lile tukio aisee mpaka hasira zilinishika yaan haina tofauti na jinsi mombasasa alivyokuwa anaelezea tukio la kutekwa Mo yaan haingii akilini kabisa, hilo tukio inawezekana polisi wamemuua huyo dereva Bila kuwa na hatia inatakiwa lichunguzwe
 
Kwahiyo unaamini kuwa Dereva alienda na kisu kuwashambulia Askari?
Au Dereva alikuwa chizi? Kwa akili ya kawaida inawezekana vipi Dereva aende kuwashambulia Askari huku akiwa Hana hata wembe? Jiulize Kwann gari ilishambuliwa Kwa risasi?
Una uhakika ana akili timamu? Kwanini hakusimama baada ya kupigwa mkono? Waliokuwa eneo la tukio ndio wanajua hali halisi. Kwanini auawe yeye na sio wengine? Kama aliamua kukimbia, kwanini hakuondoka moja kwa moja?
 
Kwa hiyo polisi kadhaa wenye bunduki hawawezi kumdhibiti mtu mwenye kisu kwa kumvunja hata miguu?? Ni kwa nini kila siku tunasikia tuu wameuwawa na hakuna hata siku moja tumeskia amedhibitiwa kwa kuvunjwa miguu???
Nilihitaji nihoji hivo sema umeniwahi. Kwa kukazia polisi wanajipotezea ushahidi wenyewe kwani tukio kama LA huyo jamaa wangeweza kumvunja hata miguu ili awasaidie katika uchunguzi zaidi. Jeshi letu linajitahidi ila maadili na taratibu za kazi yao ni kama zimesahaulika kwa baadhi yao.
 
Una uhakika ana akili timamu? Kwanini hakusimama baada ya kupigwa mkono? Waliokuwa eneo la tukio ndio wanajua hali halisi. Kwanini auawe yeye na sio wengine? Kama aliamua kukimbia, kwanini hakuondoka moja kwa moja?
Umeambiwa matairi ya gari yalipigwa risasi gari ikapoteza muelekeo sasa ulitaka aondoke moja kwa moja na makalio yako!?
 
Nipo Masasi hapa Mkuu kuhusu hiyo ishu wengi hawajui kabisaaa... ukweli ni kuwa hawa polisi wameficha ushahid pia jamaa ameuawa Kwa makusudi Tu na polisi kwasabb ya pesa.

Dereva alikuwa pekeyake ndani ya gari na ameporwa pesa na vitu vingine vya thamani pamoja na documents za oficn kwake,huku Kwenye mitandao watu hawajui lolote zaidi kupata picha ya upande mmoja
Kwa hiyo masasi ndio eneo la tukio ,acha kuzungumza Mambo usiyoyajua
 
Kwa hiyo polisi kadhaa wenye bunduki hawawezi kumdhibiti mtu mwenye kisu kwa kumvunja hata miguu?? Ni kwa nini kila siku tunasikia tuu wameuwawa na hakuna hata siku moja tumeskia amedhibitiwa kwa kuvunjwa miguu???
Kwanini uwavamie polisi kwa lengo la kuwapora silaha?
 
Mimi mwenyewe nipo huku kusini/Masasi hii ishu kumbe ni usanii wa polisi wametunga na wameiba pesa na vitu vingine.
Kumbuka haya Magari wanakuwa na Dereva pekeyake Kwanza polisi walianza kufyatua risasi Kwenye matairi mpaka gari ikahama njia na jamaa alivyoshuka akapigwa risasi

Huyo jamaa unafikiri alikuwa amebeba shilingi ngapi kiasi cha kuwatoa udenda hao mapolisi... Maana ni kama gari ya Dangote inarudi mtwara basi lazima ilikuwa tupu kwa maana ilipeleka cement mahala na ilikuwa inarudi....

La msingi kwa serikali kidhibiti haya matukio inapaswa kuunda chombo ndani ya serikali kitakachokuwa mahususi kwa ajili ya hizi sintofahamu...
 
Polisi wa Tanzania anaweza kukupiga risasi kwenye paji la uso wakasema alijaribu kukimbia tukapiga risasi juu hakusimama tukapiga nyingine juu ikapinda ikaenda kumpiga usoni.
 
Back
Top Bottom