Kizuwizi cha askari wa Lindi, ni moja ya vizuwizi maharamia na magaidi wanakichukia sana

Kizuwizi cha askari wa Lindi, ni moja ya vizuwizi maharamia na magaidi wanakichukia sana

Nimesikia tukio la dereva kutaka kuwaua Askari ila wakamuwahi, jambo hili sijalishangaa kwangu naona kuwa ni jambo sasa Serikali kuweka vifaa maalumu pale kwenye kizuwizi kuwasaidia hawa Askari.

Kiufupi ukiwa kusini ukimuuliza dereva au mtu anaye ijua hiyo barabara atakwambia askari wapale Lindi ni hatari why?

Pale ndio stop point, utapita kote utahonga kote ila ukifika na mzigo Lindi kazi unayo pale wale jamaa hata kama watasema wanachukua rushwa minu nadhani itakuwa rushwa sio ya kawaida ila wapo makini hupiti kama una haramu umebeba na huo ndio ukweli.

Kwa wale wataalam wa yale yanayoendelea kusini utakubaliana na mimi Lindi hapawezi kuwa sehemu ya kupenda na maharamia au madereva wanaobeba magendo.

Niwape pole jeshi la polisi na niwatie nguvu kukaza bidii. Kazi na iendelee.
juz kati nikajichanganya huko kusin kununua korosho nilichokutana nacho ckuamin. ni kama nipo kabul afghanistan.
 
Tena hakuna maaskari wala rushwa kama hao waoLindi nuksii!!aunty yangu alikamatwa na pembe za ndovu walimtoa 60mils..mbwa tu hao askari wa Tanzania ni mashetani kabisaa..hayafai
 
Kwahiyo unaamini kuwa Dereva alienda na kisu kuwashambulia Askari?
Au Dereva alikuwa chizi? Kwa akili ya kawaida inawezekana vipi Dereva aende kuwashambulia Askari huku akiwa Hana hata wembe? Jiulize Kwann gari ilishambuliwa Kwa risasi?
Maaskari wa bongo wana roho mbaya Sana'a!ndio maana yanakufa Vito vya ajabu ajabu!
 
Kazi ya upolisi ni dhulma tupu,ndio maana asilimia 95 ya mapolisi baada ya kustaafu wanakuwa madhalili na wanakufa kwa mateso mungu analipa kwanza duniani
Kuna askari wanashirikiana na watuhumiwa na wake za watuhumiwa kuficha baadhi ya Mali zilizopatikana kwa njia ya wizi lengo ni kua wakitoka jela askari wagawane na watuhumiwa hizo nyumba..

Wale jamaa wa Kesi ya kupora mabilioni ya NBC walinunua nyumba za baada ya pale mbali mbali na magari,kilichofanyika mahakamani wameorodhesha magari tu na baadhi ya Mali lakini nyumba hawajaorodhesha lengo ni kua kesi ikiisha zile nyumba wagawane maaskari na Watuhumiwa then jitu linakuja linasema Polish waadilifu...
Maaskari wa Tanzania ni laana tu!wachache sana ndo wàadilifu wengi hovyooo!!
 
Nipo Masasi hapa Mkuu kuhusu hiyo ishu wengi hawajui kabisaaa... ukweli ni kuwa hawa polisi wameficha ushahid pia jamaa ameuawa Kwa makusudi Tu na polisi kwasabb ya pesa.

Dereva alikuwa pekeyake ndani ya gari na ameporwa pesa na vitu vingine vya thamani pamoja na documents za oficn kwake,huku Kwenye mitandao watu hawajui lolote zaidi kupata picha ya upande mmoja

acha upumbavu wewe,usitake watu waandike na vingine visivyohitajika hapa.

kwahiyo baada ya kumpora wakampiga risasi!!nawewe umetuliza jiwe lako hilo juu huko unaona ni sawa kabisa.
 
Hiyo taarifa ya polisi naitilia mashaka,dereva mwenye kisu atake kuwaua askari 4 wenye siraha?.hapa kuna vitu vingi vimefichwa,Polisi wetu wanajulikana kwa kuficha taarifa ili kulindana.
Yaani polisi wanatuhumiwa lakini wao ndiyo wanajichunguza
 
Mfano ni juzi tu polisi waliuana kule Kilimanjaro kwa visa vya magendo wakatunga uongo kuwa amekufa kwa ajali - nadhani the story went that way. Lakini walipochunguzana baada ya ndugu wa askari aliyekufa kusimama kidete wakagundua kuwa aliuawa na wenzie.
Hii story ya Lindi yapaswa ichunguzwe na upande usio na maslahi na polisi kwani kwa maelezo ya RPC ni ngumu kueleweka - story haijanyooka.
Huo ndiyo ukweli
 
Mtoa hoja hii ni shetani na katili mno na ni hatari mno maana anatuletea familia iliyojaa ukatili,story iliyosikika hapa ni ya upande mmoja tu,dereva mwenye kisu(sina hakika nalo)ashambulie askari mwenye SMG!huu ni uongo at it's best na elewa dereva huyu amepata ajali!key witness ni abiria waliokuwepo hapo na mimi siamini kabisa story ya rpc,ndio maana nchi inahitaji KATIBA mpya maana itatuletea IPID (kama MPs wa jeshi)na kesi hii ingechunguzwa na hawa IPID,mtoa hoja hii ni mkatili mno na mpenda trigger happy policemen
Tafuta hela usikariri mambo ya katiba haimlishi mama yako wala familia yako.
 
hv kwel haujui km kisu n silaha hatar
Punguza undezi weweee yaani unisogelee na kisu huku nina SMG au Pistol nakuangalia tuu mpaka unanifikia? Hivi huko chuoni CCP Moshi huwa wanasoma nini hasa?
 
Mfano ni juzi tu polisi waliuana kule Kilimanjaro kwa visa vya magendo wakatunga uongo kuwa amekufa kwa ajali - nadhani the story went that way. Lakini walipochunguzana baada ya ndugu wa askari aliyekufa kusimama kidete wakagundua kuwa aliuawa na wenzie.
Hii story ya Lindi yapaswa ichunguzwe na upande usio na maslahi na polisi kwani kwa maelezo ya RPC ni ngumu kueleweka - story haijanyooka.
Exactly, hivi mkuu lile sakata la akina Zombe na mapolisi wenzake kama JK asingeunda ile tume si watanzania tungekuwa tumelishwa matango pori kwamba wale vijana wa Mahenge wauza madini walikuwa ni majambazi? Can you imagine jinsi polisi wanavyoweza kudhulumu roho za watu sababu tuu ya fedha??
 
Kwa hiyo tukiandika katiba mpya hatutakuwa na jeshi la polisi? Hawatakuwa na silaha? Hakutakuwanna vizuizi? Hakutakuwa na wahalifu?
Katiba mpya inaweza kuunda chombo cha ku oversee mapolisi, kwa sasa police anaweza kufanya lolote na asiwajibishwe. Katiba mpya inaweza kuja na mapendekezo ya IGP kupatikana kupitia chombo maalumu, tena kwa interview, halafu majina mawili ya walioshinda akapelekewa rais kuchagua mmoja na kuapishwa. Katiba mpya inaweza kuleta mfumo mpya wa uanzishwaji wa hizi check points iweje na iwe ni lazima zote kuwekwa CCTV camera...
 
Nipo Masasi hapa Mkuu kuhusu hiyo ishu wengi hawajui kabisaaa... ukweli ni kuwa hawa polisi wameficha ushahid pia jamaa ameuawa Kwa makusudi Tu na polisi kwasabb ya pesa.

Dereva alikuwa pekeyake ndani ya gari na ameporwa pesa na vitu vingine vya thamani pamoja na documents za oficn kwake,huku Kwenye mitandao watu hawajui lolote zaidi kupata picha ya upande mmoja
Mkuu hili wengine tulishahisi kwa sababu tunajua issues za hawa mapolisi wetu...
 
Polisi kwa magendo wameshindikana hiyo hata wakuu wao wanajua bayana njaa mbele pesa mbele kama tai...
Sasa traffic anachukua rushwa wa buku mbili mpaka tano, ndiyo akute dereva katoka Kigoma au Katavi huko kabeba mizigo ya njiani mpaka anafika Lindi ana milioni yake moja au mbili na amedinda kuitoa ni nini kitafuata hapo unafikiri??
 
Nipo Masasi hapa Mkuu kuhusu hiyo ishu wengi hawajui kabisaaa... ukweli ni kuwa hawa polisi wameficha ushahid pia jamaa ameuawa Kwa makusudi Tu na polisi kwasabb ya pesa.

Dereva alikuwa pekeyake ndani ya gari na ameporwa pesa na vitu vingine vya thamani pamoja na documents za oficn kwake,huku Kwenye mitandao watu hawajui lolote zaidi kupata picha ya upande mmoja
Wengi hawajui lakini wewe umejua mkuu
 
Back
Top Bottom